Ibrahim masoud 'maestro' atua E FM 93.7

Ibrahim masoud 'maestro' atua E FM 93.7

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
[h=1]
[/h]

Aliyekuwa Mtangazaji wa vipindi vya Michezo wa redio Clouds Dar es Salaam,Ibrahim Masoud 'Maestro' (pichani kushoto) leo amekamilisha usajili wake wa kujiunga na Kituo maarufu hivi sasa cha radio hapa jijini Dar es Salaam cha E FM 93.7.

Maestro ameungana na magwiji wengine katika utangazaji wa vipindi vya michezo nchini Maulid Kitenge na Omary Katanga ambao wapo katika radio hiyo inayokuja kwa kasi jijini.

Pichani Maestro akitambulishwa rasmi na Mkuu wa kipindi cha michezo cha E. sports cha E FM 93.7 Maulid Baraka Kitenge leo.

Chanzo:Michuzi
 
Nadhani sasa wapanue huduma na kufika mikoani, japo wapo kwa mtandao kama tune in.com kwangu mimi wa mkoani nilie na shida ya internet ntakosa utamu wa uchambuzi wa habari za michezo
 
Tatizo hii radio mwisho wake ni Dar tuu
 
  • Thanks
Reactions: ram
Hilo Si Tatizo bali ni changamoto mkuu, hata mawingu walianza hivyo wakiwa wame jibanza pale mjini

Wanatakiwa kufanya haraka wajipanue hata mkoa mmoja mwaka huu hakika nimepata wasaha wa kusikiliza hii radio nikiwa dar ...hii ni radio moto kabisa na wakijipanua watawatetemesha Clouds na Earadio ..
 
Kwa kuondoka huyu ni pigo....zaidi ya kuwa mtangazaji lakini ni producer mzuri wa vipindi hivyo hapo jamaa wamebeba mtangazaji na producer mahiri.....
 
Nikiwa Dar ni tune masafa gani kuwapata hao jamaa.?
 
Duh walishindwa muongezea hela au ndo kubadili mazingira
 
hii redio iko chini ya nani? maana kufikia level ya kuwapora Cloudz mtangazaji si jambo dogo
 
Kwa kuondoka huyu ni pigo....zaidi ya kuwa mtangazaji lakini ni producer mzuri wa vipindi hivyo hapo jamaa wamebeba mtangazaji na producer mahiri.....

Siku za karibuni alikua anaonekana kama hana amani pale kwenye kipindi cha michezo hata ikifika nafasi ya kuchangia lile jitu jeusi lwambano lilikua kama linampotezea flani tofauti na zamu ya dauda. Niliona kbs huyu jamaa anaweza kufanya maamuzi magumu! Matokeo yake ndio hayo sasa kipindi cha michezo pale clouds kimebaki na majitu meusi matupu!..
 
watu mna maneno
 
Wanatakiwa kufanya haraka wajipanue hata mkoa mmoja mwaka huu hakika nimepata wasaha wa kusikiliza hii radio nikiwa dar ...hii ni radio moto kabisa na wakijipanua watawatetemesha Clouds na Earadio ..

So far clouds wamesha tetemeka maana jamaa wanachukua cream tu. Inaonekana wamejipanga otherwise wasingeweza kuchukua watangazaji wazuri.

Ila ulilosema ni sahihi kabisa inabidi wawe fast kwenye kupanuka maana watu wenye akili zetu tumeshaona clouds ni watu wa fitina tu
 
Back
Top Bottom