Mkuu post/reply zako nyingi naona huwa zinakaa ki-udini udini na ubaguzi wa rangi ila huwa unaziandika kwa ujanja wa hali ya juu ili usionekane kama wewe ni mdini au mbaguzi wa rangi. Nimeona comment zako jinsi zinavyokuwa negative (hata zile ambazo ni positive huwa unaziandika kama positive lakini zikitoa taswira ya negative) kwa wakristo, na kinyume chake.
Kwa nini umemtaja mkapa hali mambo mengi ambayo wananchi wanalalamikia sasa yametokea kipindi cha awamu ya nne wakati mkapa amemaliza muhula wake mfano hili la Dowans. (Hapa simaanishi kipindi cha mkapa hapakuwa na maovu).
Unapozungumzia masuala ya rangi, wewe kuwa mwarabu kunakusaidi nini na mwingine kuwa mweusi kunakukera nini?
Kuhusu suala la mgawo wa umeme ni kwamba taifa limeingizwa katika matatizo hayo na hao waasia ambao unasema hawawezi kufanya madudu (may be rushwa siyo madudu). Kuhusu kuathirika wao hawayapati hayo madhara kwa sababu wana standby units zinazowazalishia umeme majumbani mwao huku wamatumbi wakitaabika mitaani.
Pamoja tushirikiane kujenga nchi na si kubaguana.