kitalolo
JF-Expert Member
- Dec 4, 2006
- 1,827
- 708
Heshima mbele kamanda.
Acha nikupe darasa.
Hii kesi itamtumbukia William Ruto nyongo maana katika watuhumiwa wote, yeye na yule Sang ndo
wanakazi kubwa kinoma. Ushahidi dhidi yao ulitoka serikalini na Kibaki mwenyewe alinukuliwa akisema
katika zile 'Wikileaks' kwamba anaamini fika kua Ruto ndiye aliyekua incharge ya kuua wakikuyu mitaa
ya Rift Valley. Kipindi hicho hawakua washkaji na Uhuru. Kwa hivyo phone records na taped conversations
pamoja na witness kadhaa waliwasilishwa na serikali ya Kibaki. That is fool proof evidence coming from
the Govt.
Hata hivyo kutoa ushahid dhidi ya Uhuru na Muthaura ilimsumbua sana bwana Ocampo na huyu Fatou nd'o
maana hii kesi ya Muthaura imeshindankana.
Sipendi kutoa utabiri wa hizi kesi lakini ukiniuliza nitakwambia Uhuru Kenyatta anaweza kuepuka lakini Ruto
na Sang watabaki tu!...Huyo Sang wanaye kwenye Redio kipindo hicho aliopkua mtangazi wa KASS FM. Alikua
anawaita wakikuyu 'Madoadoa' na 'magugu'...hawakupaswa kua Rift Valley na baada ya hizo kura tuliona matokeo
yake.
Kaeni mkao wa kula maana hii songombinde nd'o mwanzo inatoa uhondo!
Mkuu Ab-Titchaz pia unaweza kutusaidia hapa kuna swali watu wengi wanauliza ikiwa Raisi Kibaki ndiye alikuwa mgombea wa uchaguzi na Bw. Raila Na baada ya Raila kudai kuwa ameibiwa kura tuliona mambo yaliyojitokeza hata raisi kujiapiasha haraka haraka vichochoroni na baada ya hapo machafuko yakatokea Key suspect walipaswa wawi hawa watu wawili then kila Uhuru, ruto na hawa jamaa wengine wafwatie kwa mbali kutokana na kauli zao zilizochochea vugugu hizo, kwamfano huyu mtangazaji ni wazi kuwa kauli zake kupitia vvyombo vya habari zilichochea watu kujitokeza mitaani na kupigana.
Kama ilivyokuwa kwa Lora bagbo au kuna double standard??
Last edited by a moderator:

