KERO ICD ya Bravo Mabibo imegeuza barabara kuwa maegesho ya malori; TASAC, Halmashauri ya Ubungo mpo?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest

Bandari Kavu (ICD) ya Bravo Ubungo, inayotumika kama kituo cha kuhudumia mizigo ya makontena, iliyopo Mabibo Kisiwani, katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, nyuma ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), imekuwa kero kwa watumiaji wa barabara zilizopo pembezoni mwa eneo hilo.

Kwa sasa, malori yanapaki hadi barabarani na mengine kukaa hapo kwa siku nzima. Hali hiyo imeifanya barabara hiyo kugeuka kuwa maegesho ya malori, kana kwamba hakuna viongozi wanaoweza kuchukua hatua kukabiliana na changamoto hiyo. Watumiaji wa barabara, hususan madereva wa magari wanaopita katika njia hiyo inayounganisha na eneo la ICD hiyo kutoka upande wa Ubungo, hulazimika kurudi nyuma au kutumia vichochoro kutokana na kuzuiwa kwa njia.

Uwepo wa bandari hiyo kavu umeongeza kero ya foleni, huku malori yakiendelea kuegeshwa barabarani kwa muda mrefu. Hali hii inazua maswali kuhusu uwajibikaji wa mamlaka zinazopaswa kuhakikisha kuwa barabara hazitumiki kama maegesho ya magari makubwa.
WhatsApp Image 2026-10-15 at 09.28.07.jpeg
WhatsApp Image 2026-10-15 at 09.29.59u.jpeg
WhatsApp Image 2026-10-15 at 09.29.58n.jpeg
Nakumbuka Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Baharini Tanzania (TASAC), ambayo ina jukumu la kusimamia masuala ya usafiri wa baharini na bandari kavu, aliwahi kueleza kuwa moja ya vigezo muhimu kwa ICD ni kuwa na eneo la kutosha la kuegesha malori ndani ya kituo husika, badala ya kuyaacha nje, hususan barabarani, na kusababisha usumbufu kwa watumiaji wengine.

Hata hivyo, katika eneo la ICD ya Bravo Mabibo, hali tofauti na maelezo hayo. Najiuliza swali; Je, TASAC haina taarifa kuhusu kinachoendelea katika ICD hiyo, au kuna sababu nyingine zinazofanya changamoto hii iendelee bila kuchukuliwa hatua?

Tunapenda kuona uwekezaji ukiendelea, lakini uwekezaji huo haupaswi kuwa chanzo cha kero kwa wananchi wala kuwanyima wengine haki ya kutumia barabara kwa uhuru. Ni muhimu mamlaka husika kuhakikisha kuwa shughuli za uwekezaji zinafanyika kwa kuzingatia maslahi ya umma, usalama na matumizi bora ya miundombinu. Hili ni muhimu zaidi kwa uwekezaji unaofanyika katikati ya jiji, ambako barabara hutumika muda wote kurahisisha usafiri na utoaji wa huduma kwa wananchi.

Bandari hiyo kavu ina takribani miezi mitano tangu ilipozinduliwa. Kwa mujibu wa Mkurugenzi na Mmiliki wa Bravo Group, Angelina Ngalula, akizungumza kuelekea uzinduzi alisema kwamba kituo hicho kitakuwa na uwezo wa kuhudumia zaidi ya tani milioni moja za mizigo ya madini inayotoka katika nchi jirani za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Zambia kwa ajili ya kusafirishwa nje ya nchi, pamoja na zaidi ya makasha 60,000 ya mizigo inayoingia nchini.

Nani alitoa vibali?
Kwa kuzingatia ukubwa wa uwekezaji huo na uwezo wake wa kuhudumia kiasi kikubwa cha mizigo, inafaa kujiuliza: TASAC na mamlaka nyingine husika zilijiridhishaje kuhusu utoshelevu wa miundombinu kabla ya kuruhusu shughuli za kituo hicho kuanza? Je, tathmini ilifanyika kubaini athari zinazoweza kujitokeza kwa barabara za jirani, ikiwemo kuongezeka kwa foleni na uharibifu wa barabara kutokana na malori kuegeshwa kwa muda mrefu?

Changamoto hii kujitokeza mapema kiasi hiki inapaswa kuwa sababu ya mamlaka husika kuchukua hatua. TASAC, Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo na taasisi nyingine zenye wajibu wa kusimamia shughuli hizo zinapaswa kueleza hatua zinazochukuliwa kuhakikisha kuwa barabara hazigeuzwi kuwa maegesho ya malori na kwamba uwekezaji huo hauendelei kuwa kero kwa wananchi.
WhatsApp Image 2026-10-15 at 09.29.58.jpeg
 
Hii ni ukweli kabisa kwa sababu hata eneo lilolokuwa linatumiwa na wanafunzi kama sehemu ya mazoezi ya mpira ijapokuwa haikuwa rasmi kwa sasa imejazwa magari yanayoingia na kutoka kwenye hiyo bandari kavu ya Bravo
 
Msururu wa malori unafika hadi ubungo muda mwingine hadi shekilango
Tena wakati mwingine foleni inaanzia ubungo maziwa inakuja hadi ubungo mataa inaendelea hadi mabibo mwisho bado mabibo mwisho ukutane na foleni ya magari mengine jumlisha na foleni kutokea mabibo mwisho hadi mabibo sokoni mtu kuja kufika shekilango almost lisaa lizima na ni sehemu ya dakika tano.
 
Jamani mambo mengine tuwe tunachunguza badala ya kulipuka nayo tu kwenye mitandao kushambulia watu. Hii njia mimi napita kila siku kwenda Chuo cha NIT. ICD ya Bravo haina shida. Tatizo lipo kwa mjenzi Mchina wa barabara ambae amefunga barabara zote ya kuingia hapo kwenye ICD ya Shekilango na Makaburini kwa ajili ya Ujenzi. Na hiyo El nino ikija sijui itakuwaje.
2a27113a-e729-4de9-bed3-7dd36f44bfc0.jpeg

Bandari Kavu (ICD) ya Bravo Ubungo, inayotumika kama kituo cha kuhudumia mizigo ya makontena, iliyopo Mabibo Kisiwani, katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, nyuma ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), imekuwa kero kwa watumiaji wa barabara zilizopo pembezoni mwa eneo hilo.

Kwa sasa, malori yanapaki hadi barabarani na mengine kukaa hapo kwa siku nzima. Hali hiyo imeifanya barabara hiyo kugeuka kuwa maegesho ya malori, kana kwamba hakuna viongozi wanaoweza kuchukua hatua kukabiliana na changamoto hiyo. Watumiaji wa barabara, hususan madereva wa magari wanaopita katika njia hiyo inayounganisha na eneo la ICD hiyo kutoka upande wa Ubungo, hulazimika kurudi nyuma au kutumia vichochoro kutokana na kuzuiwa kwa njia.

Uwepo wa bandari hiyo kavu umeongeza kero ya foleni, huku malori yakiendelea kuegeshwa barabarani kwa muda mrefu. Hali hii inazua maswali kuhusu uwajibikaji wa mamlaka zinazopaswa kuhakikisha kuwa barabara hazitumiki kama maegesho ya magari makubwa.
Nakumbuka Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Baharini Tanzania (TASAC), ambayo ina jukumu la kusimamia masuala ya usafiri wa baharini na bandari kavu, aliwahi kueleza kuwa moja ya vigezo muhimu kwa ICD ni kuwa na eneo la kutosha la kuegesha malori ndani ya kituo husika, badala ya kuyaacha nje, hususan barabarani, na kusababisha usumbufu kwa watumiaji wengine.

Hata hivyo, katika eneo la ICD ya Bravo Mabibo, hali tofauti na maelezo hayo. Najiuliza swali; Je, TASAC haina taarifa kuhusu kinachoendelea katika ICD hiyo, au kuna sababu nyingine zinazofanya changamoto hii iendelee bila kuchukuliwa hatua?

Tunapenda kuona uwekezaji ukiendelea, lakini uwekezaji huo haupaswi kuwa chanzo cha kero kwa wananchi wala kuwanyima wengine haki ya kutumia barabara kwa uhuru. Ni muhimu mamlaka husika kuhakikisha kuwa shughuli za uwekezaji zinafanyika kwa kuzingatia maslahi ya umma, usalama na matumizi bora ya miundombinu. Hili ni muhimu zaidi kwa uwekezaji unaofanyika katikati ya jiji, ambako barabara hutumika muda wote kurahisisha usafiri na utoaji wa huduma kwa wananchi.

Bandari hiyo kavu ina takribani miezi mitano tangu ilipozinduliwa. Kwa mujibu wa Mkurugenzi na Mmiliki wa Bravo Group, Angelina Ngalula, akizungumza kuelekea uzinduzi alisema kwamba kituo hicho kitakuwa na uwezo wa kuhudumia zaidi ya tani milioni moja za mizigo ya madini inayotoka katika nchi jirani za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Zambia kwa ajili ya kusafirishwa nje ya nchi, pamoja na zaidi ya makasha 60,000 ya mizigo inayoingia nchini.

Nani alitoa vibali?
Kwa kuzingatia ukubwa wa uwekezaji huo na uwezo wake wa kuhudumia kiasi kikubwa cha mizigo, inafaa kujiuliza: TASAC na mamlaka nyingine husika zilijiridhishaje kuhusu utoshelevu wa miundombinu kabla ya kuruhusu shughuli za kituo hicho kuanza? Je, tathmini ilifanyika kubaini athari zinazoweza kujitokeza kwa barabara za jirani, ikiwemo kuongezeka kwa foleni na uharibifu wa barabara kutokana na malori kuegeshwa kwa muda mrefu?

Changamoto hii kujitokeza mapema kiasi hiki inapaswa kuwa sababu ya mamlaka husika kuchukua hatua. TASAC, Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo na taasisi nyingine zenye wajibu wa kusimamia shughuli hizo zinapaswa kueleza hatua zinazochukuliwa kuhakikisha kuwa barabara hazigeuzwi kuwa maegesho ya malori na kwamba uwekezaji huo hauendelei kuwa kero kwa wananchi.

Bandari Kavu (ICD) ya Bravo Ubungo, inayotumika kama kituo cha kuhudumia mizigo ya makontena, iliyopo Mabibo Kisiwani, katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, nyuma ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), imekuwa kero kwa watumiaji wa barabara zilizopo pembezoni mwa eneo hilo.

Kwa sasa, malori yanapaki hadi barabarani na mengine kukaa hapo kwa siku nzima. Hali hiyo imeifanya barabara hiyo kugeuka kuwa maegesho ya malori, kana kwamba hakuna viongozi wanaoweza kuchukua hatua kukabiliana na changamoto hiyo. Watumiaji wa barabara, hususan madereva wa magari wanaopita katika njia hiyo inayounganisha na eneo la ICD hiyo kutoka upande wa Ubungo, hulazimika kurudi nyuma au kutumia vichochoro kutokana na kuzuiwa kwa njia.

Uwepo wa bandari hiyo kavu umeongeza kero ya foleni, huku malori yakiendelea kuegeshwa barabarani kwa muda mrefu. Hali hii inazua maswali kuhusu uwajibikaji wa mamlaka zinazopaswa kuhakikisha kuwa barabara hazitumiki kama maegesho ya magari makubwa.
Nakumbuka Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Baharini Tanzania (TASAC), ambayo ina jukumu la kusimamia masuala ya usafiri wa baharini na bandari kavu, aliwahi kueleza kuwa moja ya vigezo muhimu kwa ICD ni kuwa na eneo la kutosha la kuegesha malori ndani ya kituo husika, badala ya kuyaacha nje, hususan barabarani, na kusababisha usumbufu kwa watumiaji wengine.

Hata hivyo, katika eneo la ICD ya Bravo Mabibo, hali tofauti na maelezo hayo. Najiuliza swali; Je, TASAC haina taarifa kuhusu kinachoendelea katika ICD hiyo, au kuna sababu nyingine zinazofanya changamoto hii iendelee bila kuchukuliwa hatua?

Tunapenda kuona uwekezaji ukiendelea, lakini uwekezaji huo haupaswi kuwa chanzo cha kero kwa wananchi wala kuwanyima wengine haki ya kutumia barabara kwa uhuru. Ni muhimu mamlaka husika kuhakikisha kuwa shughuli za uwekezaji zinafanyika kwa kuzingatia maslahi ya umma, usalama na matumizi bora ya miundombinu. Hili ni muhimu zaidi kwa uwekezaji unaofanyika katikati ya jiji, ambako barabara hutumika muda wote kurahisisha usafiri na utoaji wa huduma kwa wananchi.

Bandari hiyo kavu ina takribani miezi mitano tangu ilipozinduliwa. Kwa mujibu wa Mkurugenzi na Mmiliki wa Bravo Group, Angelina Ngalula, akizungumza kuelekea uzinduzi alisema kwamba kituo hicho kitakuwa na uwezo wa kuhudumia zaidi ya tani milioni moja za mizigo ya madini inayotoka katika nchi jirani za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Zambia kwa ajili ya kusafirishwa nje ya nchi, pamoja na zaidi ya makasha 60,000 ya mizigo inayoingia nchini.

Nani alitoa vibali?
Kwa kuzingatia ukubwa wa uwekezaji huo na uwezo wake wa kuhudumia kiasi kikubwa cha mizigo, inafaa kujiuliza: TASAC na mamlaka nyingine husika zilijiridhishaje kuhusu utoshelevu wa miundombinu kabla ya kuruhusu shughuli za kituo hicho kuanza? Je, tathmini ilifanyika kubaini athari zinazoweza kujitokeza kwa barabara za jirani, ikiwemo kuongezeka kwa foleni na uharibifu wa barabara kutokana na malori kuegeshwa kwa muda mrefu?

Changamoto hii kujitokeza mapema kiasi hiki inapaswa kuwa sababu ya mamlaka husika kuchukua hatua. TASAC, Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo na taasisi nyingine zenye wajibu wa kusimamia shughuli hizo zinapaswa kueleza hatua zinazochukuliwa kuhakikisha kuwa barabara hazigeuzwi kuwa maegesho ya malori na kwamba uwekezaji huo hauendelei kuwa kero kwa wananchi.
 
Mimi nipo hapa Mabibo eneo la tukio hali yenyewe ndiyo kama hii. Hapa kosa la TASAC ni lipi?
 
Attachments

  • 6a00561b-6889-4584-b1d9-ffecd465a576.jpeg
    6a00561b-6889-4584-b1d9-ffecd465a576.jpeg
    181.1 KB · Views: 6
Bosi wa Bravo si ndio kapewa Uraisi wa Shirikisho la Sekta Binafsi Tanzania,basi tulieni.
 
Mimi nipo hapa Mabibo eneo la tukio hali yenyewe ndiyo kama hii. Hapa kosa la TASAC ni lipi?
 
Attachments

  • 6a00561b-6889-4584-b1d9-ffecd465a576.jpeg
    6a00561b-6889-4584-b1d9-ffecd465a576.jpeg
    181.1 KB · Views: 6
Mzenji wala hajari kwakua yy anapita n msafara tu.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Dah! Nipo hapa muda huu kumefanya nawaza mambo mengi mno, kiukweli kuzaliwa Bongo ni mistake kubwa mnoooo🙌
 
Back
Top Bottom