Pre GE2025 Idadi kubwa ya wapiga kura ndilo kaburi la CCM

Pre GE2025 Idadi kubwa ya wapiga kura ndilo kaburi la CCM

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Duniani kote hakuna kitu kinachoogopwa na serikali dhalimu kama idadi kubwa ya wapiga kura.

Baada ya Tume inayosimamia uchaguzi TAMISEMI kudanganya idadi halisi ya waliojiandikisha, kazi iliyo mbele yao kwa sasa ni namna gani watabadilisha hiyo idadi ziwe kura.

Kwa mfano; Mwanza, Sensa ya 2022 idadi ilikuwa 1.95M zaidi ya nusu wakiwa ni watoto chini ya miaka 14, leo wameandikisha 2,08M. Siku ya kupiga kura watawatoa wapi hao watoto waje kupanga foleni wapige kura, mashuleni au mitaani?

Kwa hali halisi ilivyo mitaani na vijijini, chuki ya wananchi kwa CCM na viongozi wake wa mitaa na vitongoji ni kubwa sana, hasira ya ugumu wa maisha kwa wananchi hasa vijana wataimalizia kwenye sanduku la kura.

Mbali na hiyo chuki ya wananchi, ndani ya CCM kwenyewe kuna makundi hasimu yanayotaka mgombea wao apite hivyo kugawa kura.

Kwenye chaguzi zilizopita CCM ilikuwa inasingizia wananchi hasa vijana hawajitokezi kujiandikisha, walitoa hicho kisingizio kwa vile ilionekana vijana wengi walikuwa wanaviunga mkono vyama vya upinzani, safari hii takwimu zinaonesha vijana wengi wamejiandikisha.

Ukichukulia hali hii na idadi kubwa ya waliojiandikisha iwapo wote wataamua kujitokeza kupiga kura, basi CCM watakuwa na kazi kubwa ya kuiba zaidi ya nusu ya kura kitu ambacho ni next to impossible.

Kati ya kura 1,000,000 unaweza kuiba kura laki moja (100,000) lakini siyo laki tano (500,000), hilo likitokea basi utakuwa ni wizi mkubwa kuwahi kutokea na utaweka historia Tanzania.

Kwa idadi hii nadiriki kusema CCM wamejichimbia kaburi lao wenyewe kinachotakiwa kwa vyama vya upinzani sasa ni kuhamasisha watu hasa vijana wajitokeze kwa wingi siku ya kupiga kura.
Huku ni kunidanganya aisee CCM haiwezi kuondolewa kwa kura hawa watu ni wezi aisee
 
Kwa hizo takwimu maana yake ambao hata hatujafika kujiandikisha tayari tushaandikishwa kilazima. Kiufupi wamiliki wote wa card za CCM wameshaandikishwa maana ziko electronically controlled.
Sawa, hilo liko wazi tatizo ni process ya kuyabadili hayo majina yawe kura ni ishu,

hapo ni mwendo wa kukimbia na maboxi, kuficha madaftari ya wapiga kura, kuingia na chupa za chai zenye kura ndani, kuzima taa wakati wa kuhesabu, wanawake kuficha kura kwenye nguo zao za ndani, yaani ni kazi kweli kweli.
 
Mwisho wa siku CCM itashinda kwa zaidi ya 80%

Kama vijana ndiyo wapiga kura wa upinzani then inakuwaje wapinzani walalamike wanafunzi kuandikishwa?
 
Mwisho wa siku CCM itashinda kwa zaidi ya 80%

Kama vijana ndiyo wapiga kura wa upinzani then inakuwaje wapinzani walalamike wanafunzi kuandikishwa?
Kwa hiyo mtoto wako alikuletea kitu cha wizi huwezi kumuuliza.

Wapinzani wanalalamikia ukiukwaji wa kanuni na taratibu za uchaguzi whether inawa faver wao ama la.
 
Sawa, hilo liko wazi tatizo ni process ya kuyabadili hayo majina yawe kura ni ishu,

hapo ni mwendo wa kukimbia na maboxi, kuficha madaftari ya wapiga kura, kuingia na chupa za chai zenye kura ndani, kuzima taa wakati wa kuhesabu, wanawake kuficha kura kwenye nguo zao za ndani, yaani ni kazi kweli kweli.
Ugomvi utakuwa mkubwa hayo yakifanyika na nahisi Chadema watatumia style ya Mwabukusi kulinda sanduku la kura awamu hii😁
 
Huku ni kunidanganya aisee CCM haiwezi kuondolewa kwa kura hawa watu ni wezi aisee
Nilishaliona hilo miaka kadhaa nyuma, CCM itaondoka kwa machafuko kuna kila dalili. Equation ni mbili tu hakuna namna ingine...
Raia+Strike=CCM out
Raia+Kura= CCM wins
Kupingana na hizi equation ni kujipotezea muda na kujipa false hopes.
 
Kama una knowledge kidogo ya takwimu hizo data za Dar na Mwanza zina maana gani, kama huwezi ku interpolate data achana na mambo ya takwimu tuendelee na siasa taka.

View attachment 3133885
maana yake kuna udhaifu mkubwa mno wa kitakwimu kwenye hayo mabadiliko ya takwimu zako za mezani na kwenye computer, tofauti na mabadiliko halisi kule field kwenye maeneo husika🐒
 
acha upotoshaji gentleman,

Idadi kubwa ya wanachama wa CCM waliojiandikisha kupiga kura ndio hasa chachu na msingi wa ushindi wa kishindo kwa kila uchaguzi ambao CCM wanashiriki na si vinginevyo..

Ni upotoshaji wa kiwango cha juu zaidi kulinganisha matokeo ya sensa ambayo ambayo hayana kampeni wala sera na ambayo hufanyika katka kipindi cha zaidi ya miaka 10 na uchaguzi mkuu au wa serikali za ambao ni hufanyika kila baada ya miaka mi5.

Na ndiyo maana mara zote tunasema humu jukwaani na waTanzania wote wanajua, kwamba mchujo wa kura za maoni ndani ya CCM huwa una hamasa na shauku kubwa zaidi ya uchaguzi mkuu wenyewe, kwasababu, ndani ya chama hicho ndiyo waTanzania huamua mustakabali wa uongozi wa nchi yao.

Hata hivyo,
uchaguzi mkuu hua ni kukamilisha ratiba ya uchaguzi, taratibu za kisheria na kikatiba tu, kwasabb tayari wananchi wameshaamua mustakabali wao kupitia CCM 🐒
sensa 2022 raia wa mwanza ni around 2M ambao zaid nusu yaan 1M ni watoto , je ndan ya miaka 2 (2024) Mwanza imetripple idad ya watu wazima kutoka 1M hadi 2M yaan wale watoto ( 1M ) wote wamekuwa watu wazima ?

WAJINGA NDO MTAJI WA CCMU , UNAPOTETEA JAMBO TUMIA NA AKILI KDG
 
upotoshaji ni kazi nzito sana,

infact,
kwa mkoa uloutaja,
waliofikia na watakaofikia umri wa miaka 18, hadi kufikia Oct 2024 wanaweza kufikia 1.5 achilia mbali waliojiandikisha kwaajili ya kupiga kura 🐒
 
Kwa CCM hilo siyo tatizo! Tunavyosema sasa hivi huenda matokeo yameshatengenezwa!
 
Wakili Moses John Basila atoa maoni yake kuhusu zoezi la uandikishwaji daftari la mpiga kura 2024

View: https://m.youtube.com/watch?v=D0s8QGXsdV4

Aelezea uzoefu wake kuhusu mchakato mzima kumuuandaa hadi kufikia siku ya kupiga kura aliyejiandikisha...

Mchakato kuingiliwa .... watanzania tuna kasumba fulani na kutekwa na mambo mepesi. Kiasi kujua ukweli kamili inakuwa shida ... kanuni ya 7 ya uchaguzi wa TAMISEMI inatamka wazi nani mwenye sifa cha nani anaweza kupiga kura ...

Matangazo ni mengi sana kuhamasisha yalikuwepo mengi, kiasi wakaazi waliojitokeza (turn up) kujiandikisha katika daftari la mpiga kura mitaani, vijijini, vitongoji imekuwa kubwa sana na hili linastahili pongezi ...
 
Duniani kote hakuna kitu kinachoogopwa na serikali dhalimu kama idadi kubwa ya wapiga kura.

Baada ya Tume inayosimamia uchaguzi TAMISEMI kudanganya idadi halisi ya waliojiandikisha, kazi iliyo mbele yao kwa sasa ni namna gani watabadilisha hiyo idadi ziwe kura.

Kwa mfano; Mwanza, Sensa ya 2022 idadi ilikuwa 1.95M zaidi ya nusu wakiwa ni watoto chini ya miaka 14, leo wameandikisha 2,08M. Siku ya kupiga kura watawatoa wapi hao watoto waje kupanga foleni wapige kura, mashuleni au mitaani?

Kwa hali halisi ilivyo mitaani na vijijini, chuki ya wananchi kwa CCM na viongozi wake wa mitaa na vitongoji ni kubwa sana, hasira ya ugumu wa maisha kwa wananchi hasa vijana wataimalizia kwenye sanduku la kura.

Mbali na hiyo chuki ya wananchi, ndani ya CCM kwenyewe kuna makundi hasimu yanayotaka mgombea wao apite hivyo kugawa kura.

Kwenye chaguzi zilizopita CCM ilikuwa inasingizia wananchi hasa vijana hawajitokezi kujiandikisha, walitoa hicho kisingizio kwa vile ilionekana vijana wengi walikuwa wanaviunga mkono vyama vya upinzani, safari hii takwimu zinaonesha vijana wengi wamejiandikisha.

Ukichukulia hali hii na idadi kubwa ya waliojiandikisha iwapo wote wataamua kujitokeza kupiga kura, basi CCM watakuwa na kazi kubwa ya kuiba zaidi ya nusu ya kura kitu ambacho ni next to impossible.

Kati ya kura 1,000,000 unaweza kuiba kura laki moja (100,000) lakini siyo laki tano (500,000), hilo likitokea basi utakuwa ni wizi mkubwa kuwahi kutokea na utaweka historia Tanzania.

Kwa idadi hii nadiriki kusema CCM wamejichimbia kaburi lao wenyewe kinachotakiwa kwa vyama vya upinzani sasa ni kuhamasisha watu hasa vijana wajitokeze kwa wingi siku ya kupiga kura.
Hawahitaji kura kushinda. Hata mhesabu kura hana umuhimu sana. Ushindi ni tangazo tu la mtangaza matokeo.
 
hayo ni maoni na mitazamo wako potofu ambao ni haki na uhuru wako..

ukweli ni kwamba walioandikishwa kote nchini, ni wale tu wenye sifa na vigezo vya kikatiba vya kupiga kura na si vinginevyo 🐒
Acha kuchanganyikiwa. Hakuna mtu mwenye haki ya kupotosha facts. Mtu kakupa takwimu rasmi za kitaifa, wewe unaiziita maoni na mitazamo yake?!
 
Back
Top Bottom