Idadi ya wahanga wa mafuriko na maporomoko ya ardhi nchini Kenya yafikia 60

Idadi ya wahanga wa mafuriko na maporomoko ya ardhi nchini Kenya yafikia 60

Mbolabilika

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2019
Posts
2,128
Reaction score
2,867
Nakumbuka kipindi mvua zilipoanza TZ walikua wanatucheka kana kwamba ni uzembe wa serikali leo msiba umetokea kwao je serikali yao nayo haijielewi imeshindwa kuzuia majanga?

=====
1574678498873.png


Viongozi wa serikali ya Kenya wametangaza habari ya kuongezeka idadi ya wahanga wa mafuriko na maporomoko ya ardhi kuwa imefikia watu 60.

Awali Idara ya Kukabiliana na Majanga Yasiyotarajiwa nchini Kenya ilikuwa imetangaza kwamba idadi ya wahanga hao ni 37 pekee. Ijumaa iliyopita mvua zinazoendelea kunyesha nchini humo, mbali na kusababisha maafa katika eneo la Pokot Magharibi zilisababisha pia hasara kubwa kwenye miundombinu, kuharibu mashamba na makazi. Vyombo vya habari vimetangaza kwamba maporomoko ya ardhi katika eneo hilo yamesababisha kusombwa kwa daraja na kuharibiwa pia barabara na njia zinazounganisha maeneo mengine ya vijijini.

Eneo la Kaunti ya Pokot Magharibi nchini Kenya baada ya kukumbwa na maporomoko ya ardhi
Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Msalaba Mwekundu nchini Kenya, askari wa uokoaji kwa kushirikiana na jeshi la nchi hiyo, wanafanya juhudi za kufungua njia za mawasiliano katika eneo hilo la Pokot Magharibi, sambamba na kuwafikishia misaada ya kibinaadamu wahanga. Naye Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya sambamba na kutoa pole kwa familia za marehemu wa mkasa huo, amewahakikishia wahanga kwamba watapatiwa misaada yote ya lazima haraka iwezekanavyo.
 
May their souls RIP! Ila kuna fala moja lilikuwa linachekelea mafuriko ya Tanga!
 
Natoa pole kwa familia za wahanga wa maporomoko hayo.

My Deepest Condolences.
 
May their souls RIP! Ila kuna fala moja lilikuwa linachekelea mafuriko ya Tanga!
Yani ndo ujue kiasi gani wakenya wengi hawajielewi mm niliwah kumuuliza mpumbavu mmoja kwani serikali ina uwezo wa kupambana na kudra za mwenyezi mungu lilikua linasema watu waliofariki tanga eti uzembe wa serikali hawajaweka miundombinu mizur
 
Sema tuwape pole tu waliofikwa na msiba tusifate ujinga wa wakenya wa hapa jf, unatakiwa kumjali binadam mwenzio anapopatwa na matatizo usimcheke kwasababu hata yeye ajapenda ila ipo nje ya uwezo wake tu .kuna vitu vya kuleta utani kuchekana labda michezo lakini wakenya hata majanga wanawacheka binadam wenzao.
 
Back
Top Bottom