Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
"Serikali imefikia wapi kuweka utaratibu rahisi wa urasimishaji na umilikishaji Ardhi hususani kwa wanawake? - Mhe. Rose Cyprian Tweve, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa
"Serikali inatekelezeka mradi wa kuboresha usalama wa milki ya Ardhi kupitia mradi wa LTIP kwa mkopo wa fedha kutoka Benki ya Dunia ambao unafanyika katika Mamlaka za upangaji 58 nchini. Kupitia mradi huo haki za Wanawake zimezingatiwa ipasavyo katika utoaji elimu na Uhamasishaji umiliki wa Ardhi kwa wanawake na umiliki wa pamoja baina ya mke na mume" - Mhe. Geoffrey Pinda, Naibu Waziri wa Ardhi
"Kupitia utaratibu huo, vikosi kazi vimeundwa kwaajili ya kushughulikia Uhamasishaji na utoaji wa Elimu kwa makundi Maalum ya wanawake, wazee na Walemavu katika suala la urasimishaji makazi pamoja na umiliki wa pamoja wa Ardhi. Elimu inatolewa kupitia vyama vya hiari vya kijamii, Mashirika yasiyo ya kiserikali ambapo mikutano ya elimu kwa umma kuhusu utekelezaji wa miradi umefanyika katika ngazi za mitaa, Kata na Wilaya. Jumla ya wananchi 3249 wamehudhuria mikutano hiyo wakiwemo wanaume 1518 na wanawake 1731. Mradi umewezesha kuongezeka kwa idadi ya wanawake wanaomiliki Ardhi nchini kutoka asilimia 25 hadi asilimia 41. Idadi ya hati miliki ya pamoja kati ya wanandoa zimeongezeka na kufikia asilimia 10 ya hati zilizotolewa" - Mhe. Geoffrey Pinda, Naibu Waziri wa Ardhi
"Je, Serikali haioni umuhimu wa kuyafanyia kazi ile ripoti ya mapitio ya Sheria ya kukabiliana na migogoro ya Ardhi iliyofanyika mwaka 2020 ili iweze kufanyiwa kazi na wanawake wengi zaidi waweze kamiliki Ardhi?" - Mhe. Esther Edwin Malleko, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro
"Haya yanayofanyika kupitia mradi wa LTIP yameweza kuunganisha mambo mbalimbali ikiwemo taarifa iliyotolewa ya mwaka 2020 ambayo imetupa dira kuendelea kuhamasisha wakina mama kumiliki Ardhi" - Mhe. Geoffrey Pinda, Naibu Waziri wa Ardhi.