LGE2024 Idadi ya Wapigakura katika daftari la Wakazi haiakisi Takwimu ya Sensa hii ni dosari kubwa ya kubatisha uchaguzi

LGE2024 Idadi ya Wapigakura katika daftari la Wakazi haiakisi Takwimu ya Sensa hii ni dosari kubwa ya kubatisha uchaguzi

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Zoezi la sensa ilikuwa funika kombe maana sio wote walihesabiwa.

Wa tz ni zaidi ya ile idadi mzee so sensa sio kipimo, ziada IPO ila uongo nao upo maana wengi hawakujiandikisha
 
Sensa ilikua mwaka 2022 uandikishaji umefanyika 2024 kuna miaka mieili ya ziada hapo ambao walihesabiwa watoto (chini ya miaka 18) mwaka 2022 mwaka huu baadhi yao wametimiza miaka 18 hivyo kuwa na sifa ya kuandikishwa kupiga kura. Tatuzo liko wapi hapo? Mbona ni logic tu hata ya elimu ya msingi inatosha kuelewa....
Wewe ndo bado haujaelewa logic. Hoja ni hizi;

1. Hata kama tangu 2022 hadi 2024 wangeongezeka kutoka ktk idadi ya watoto waliokuwa na miaka 17 tu bado hawawezi kufika milioni mbili.

2. Katika idadi ya watu wazima milioni 30 walio ktk sensa ya 2022 toa waliofariki, wagonjwa na wengine ambao hawakujiandikisha kwa sababu zao.

3. Kwa kuzingatia hoja ya 1 na 2 ndipo huibuka mashaka ya idadi ya tamisemi wa wapiga kura milioni 31.

4. Tafsiri ya idadi hii ya tamisemi ni kwamba watu wote waliokuwa zaidi ya miaka 18 wa mwaka 2022 wamejiadikisha hata waliofariki na wagonjwa. Pia kwamba kuna zaidi ya watoto milioni 2 ktk miaka miwili wote bila ya waliokufa Wala kuumwa wamejiandikisha. Hii ni ngumu ktk hesabu za kawaida. Kwa msaa kachambue idadi ya waliokuwa na miak 17 mwaka 2022 hawafiki laki sita.
 
.Kwa mujibu wa takwimu za Wizara hiyo takribani Watanzania 31,282,331 wamejiandikisha kupiga kura katika zoezi lililoanza Oktoba 11 mpaka Oktoba 20,2024. Kwa kulinganisha na takwimu za Sensa ilizofanyika mwaka 2022 ambapo zilionesha watu wenye umri wa miaka kumi na sita na kuendelea walikua 32,988,131, kitakwimu kama tukipunguza idadi ya vifo na wale ambao mpaka wakati wa uchaguzi bado watakua na miaka 17, basi kuna uwezekano mkubwa Wizara ya TAMISEMI imeweza kuwasajili Watanzania wote wenye sifa za kupiga kura.
 
Back
Top Bottom