.Kwa mujibu wa takwimu za Wizara hiyo takribani Watanzania 31,282,331 wamejiandikisha kupiga kura katika zoezi lililoanza Oktoba 11 mpaka Oktoba 20,2024. Kwa kulinganisha na takwimu za Sensa ilizofanyika mwaka 2022 ambapo zilionesha watu wenye umri wa miaka kumi na sita na kuendelea walikua 32,988,131, kitakwimu kama tukipunguza idadi ya vifo na wale ambao mpaka wakati wa uchaguzi bado watakua na miaka 17, basi kuna uwezekano mkubwa Wizara ya TAMISEMI imeweza kuwasajili Watanzania wote wenye sifa za kupiga kura.