Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Idara ya Uhamiaji Wilaya ya Kakonko mapema wiki hii imeendesha mafunzo ya ki-uhamiaji kwa wanafunzi wa Jeshi la Akiba katika Kata ya Kasanda iliyopo Wilaya ya Kakonko Mkoa wa Kigoma kupitia kampeni ya "Mjue Jirani Yako".
Mafunzo haya yalilenga kuwajengea wanafunzi uelewa juu ya majukumu yao kama raia katika kulinda usalama wa Taifa na kushiriki katika mapambano dhidi ya wahamiaji haramu.
Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji - Victor Adam alitoa elimu ya uraia, akieleza wajibu wa kila raia katika kuhakikisha ulinzi na usalama wa jamii.
Sajinitaji Rajabu Kheir alitoa somo mahsusi juu ya umuhimu wa kutoa taarifa kwa mamlaka kuhusu watu wasiofahamika, hasa wahamiaji haramu, kwa lengo la kuimarisha usalama wa mipaka yetu.
Aidha Konstebo- Clara William alieleza kwa kina kuhusu matumizi sahihi ya hati za kusafiria, yaani Pasipoti na hati ya dharura ya kusafiria, na umuhimu wake kwa raia wanaosafiri nje ya nchi.
Wanafunzi hao wa Jeshi la Akiba walielezwa pia manufaa juu ya masuala ya usalama wa taifa, umuhimu wa uzalendo, na nafasi yao katika kusaidia mamlaka za usalama.
Elimu hiyo imewawezesha kuwa mabalozi wa amani na ulinzi na Usalama ndani ya jamii zao.