Idara ya Uhamiaji Kakonko yatoa Elimu ya Uzalendo kwa Wanafunzi wa Jeshi la Akiba

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876

‎
‎Idara ya Uhamiaji Wilaya ya Kakonko mapema wiki hii imeendesha mafunzo ya ki-uhamiaji kwa wanafunzi wa Jeshi la Akiba katika Kata ya Kasanda iliyopo Wilaya ya Kakonko Mkoa wa Kigoma kupitia kampeni ya "Mjue Jirani Yako".

‎
‎Mafunzo haya yalilenga kuwajengea wanafunzi uelewa juu ya majukumu yao kama raia katika kulinda usalama wa Taifa na kushiriki katika mapambano dhidi ya wahamiaji haramu.

‎
‎Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji - Victor Adam alitoa elimu ya uraia, akieleza wajibu wa kila raia katika kuhakikisha ulinzi na usalama wa jamii.

‎
‎Sajinitaji Rajabu Kheir alitoa somo mahsusi juu ya umuhimu wa kutoa taarifa kwa mamlaka kuhusu watu wasiofahamika, hasa wahamiaji haramu, kwa lengo la kuimarisha usalama wa mipaka yetu.

‎
‎Aidha Konstebo- Clara William alieleza kwa kina kuhusu matumizi sahihi ya hati za kusafiria, yaani Pasipoti na hati ya dharura ya kusafiria, na umuhimu wake kwa raia wanaosafiri nje ya nchi.

‎
‎Wanafunzi hao wa Jeshi la Akiba walielezwa pia manufaa juu ya masuala ya usalama wa taifa, umuhimu wa uzalendo, na nafasi yao katika kusaidia mamlaka za usalama.

‎
‎ Elimu hiyo imewawezesha kuwa mabalozi wa amani na ulinzi na Usalama ndani ya jamii zao.

‎
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…