Idara ya Uhamiaji mmewaruhusu vipi akina Ladwa kumiliki ardhi ikiwa mnakiri wao siyo raia

Idara ya Uhamiaji mmewaruhusu vipi akina Ladwa kumiliki ardhi ikiwa mnakiri wao siyo raia

Uhamiaji kweli watakuwa wanahusika.
Ushahidi wote huu,hakuna tamko,wala hatua zozote zilizochukuliwa!
 
Lakini Mimi mpaka Leo passport nimenyimwa na nimezaliwa hapa nimesomea hapa wazazi wote tz yani ukoo .kisa rushwa sababu kutokea kigoma.MAGUFURI lala salama vijana huku tunaumia
Endelea kusubiri watu wanaweka kitita mezani hati ya kusafiria wanaipata chini ya saa 72 maana ofisi za umma nazo zina vishoka.
 
Kuna taarifa zinasambaa mitandaoni kwamba familia ya kihindi ya Ladwa inatumia hati za kusafiria za Tanzania na Uingereza. Vyombo vya habari na baadhi ya watu wameenda mbali zaidi kusambaza nyaraka hizo mitandaoni.

Idara ya Uhamiaji katika kujibu hoja hii wameeleza kwamba watajwa walikoma kuwa RAIA wa Tanzania na sasa wanaishi nchini kama RAIA wa kigeni wakiwa na vibali halali.

Nimeangalia pia pasipoti zinazosambaa mitandaoni na naomba nikubaliane na Uhamiaji kwamba pasipoti inayosambaa mitandaoni ya Tanzania inaonekana ilitolewa zamani kabla ya pasipoti ya Uingereza jambo ambalo linaashiria kwamba hawa walikuwa RAIA wa Tanzania wakaukana utanzania na kupata uraia wa Uingereza

Kwa upande mwingine naomba niombe uhamiaji watoe pia ufafanuzi, hawa RAIA wa uingereza ambao awali walikuwa RAIA wa Tanzania wanaendeleaje kumiliki mali kama Watanzania wakati katiba na sheria zinakataza?

Ardhi wanayomiliki wanatumia uraia gani? Kama wanatumia uraia wa Tanzania kumiliki ardhi ,Uhamiaji na wizara ya ardhi awaoni kama haya ni makosa?

Malalamiko yanasema wanafukuza wapangaji kwenye nyumba za NHC, ni lini wageni wamepewa mamlaka yakufukuza wapangaji katika nyumba za shirika la umma? NHC mnawezaje kumvumilia mgeni aje atawale mali za umma na kuwafundisha wananchi namna ya kuzitumia? Kiburi wanatoa wapi?

Waziri wa mambo ya nje, hawa akina Ladwa ndio tuliowatungia sheria ya kuwapa hadhi maalumu? Na je hadhi maalumu itawapa nguvu hawa wahindi kutawala?
Kwanza kuna ubabaishaji katia hayo maandiko, hakuna anaemiliki ardhi Tanzania, iwe ni Mtanzania au mgeni.

Hakuna sheria ya kumiliki ardhi Tanzania. Tuwekana sawa hapo kwanza.
 
Kuna Watanzania wenzetu wanatuuza kimaficho kwa wageni, huko kuvunja katiba lazima kuna baraka za watu wakubwa waliopewa rushwa kubwakubwa siyo bure
Msidanganywe na fitina za huyo mtu, wapi kaonesha umiliki wa ardhi kwa Laswa au mwengine yeyote?

Tanzania hakuna mwenye kumiliki ardhi.

Hata kanisa Katoliki lenye kuhodhi ardhi kubwa baada ya serikali haliimiliki hiyo ardhi.
 
Msidanganywe n afitina za huyo mtu, wapi kaonesha umiliki wa ardhi kwa Laswa au mwengine yeyote?

Tanzania hakuna mwenye kumiliki ardhi.

Hata kanisa Katoliki lenye kuhodhi ardhi kubwa baada ya serikali haliimiliki hiyo ardhi.
Kwani nyie bakwata/waislam mmezuiwa kuhodhi ardhi

Ova
 
Back
Top Bottom