The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
TAARIFA KWA UMMA
Idara ya Uhamiaji inapenda kutoa ufafanuzi wa taarifa zilizochapishwa na kujadiliwa kwenye mitandao ya kijamii na Vyombo vya Habari kuhusu kupatiwa uraia wa Tanzania wachezaji watatu wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Singida Black Stars.Wachezaji wanaotajwa kwenye taarifa hizo ni kama ifuatavyo:-
1.Emmanuel Kwame Keyekeh (Ghana),
2.Josephat Arthur Bada (Cote d'Ivoire), na
3. Muhamed Damaro Camara (Guinea).
Wachezaji tajwa waliomba na kupewa uraia kwa mujibu wa vifungu vya 9 na 23 vya Sheria ya Uraia ya Tanzania, Sura ya 357.
Kwa muktadha huo, Idara ya Uhamiaji inapenda kuutaarifu Umma kuwa watajwa ni raia wa Tanzania kwa Tajnisi.
Imetolewa na;
SSI. Paul J. Mselle
MSEMAJI MKUU WA IDARA YA UHAMIAJI
Soma pia: Singida Black Stars yawabadilisha Uraia wachezaji wanne wa Kigeni na kuwa raia wa Tanzania ili Kukidhi Kanuni