Idara ya uhamiaji yatoa ufafanuzi dhidi ya wachezaji wa kigeni Singida Black Stars, wote ni raia wa Tanzania kwa Tajnisi

Idara ya uhamiaji yatoa ufafanuzi dhidi ya wachezaji wa kigeni Singida Black Stars, wote ni raia wa Tanzania kwa Tajnisi

TAARIFA KWA UMMA​
Idara ya Uhamiaji inapenda kutoa ufafanuzi wa taarifa zilizochapishwa na kujadiliwa kwenye mitandao ya kijamii na Vyombo vya Habari kuhusu kupatiwa uraia wa Tanzania wachezaji watatu wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Singida Black Stars.

Wachezaji wanaotajwa kwenye taarifa hizo ni kama ifuatavyo:-
1.Emmanuel Kwame Keyekeh (Ghana),
2.Josephat Arthur Bada (Cote d'Ivoire), na
3. Muhamed Damaro Camara (Guinea).

Wachezaji tajwa waliomba na kupewa uraia kwa mujibu wa vifungu vya 9 na 23 vya Sheria ya Uraia ya Tanzania, Sura ya 357.

Kwa muktadha huo, Idara ya Uhamiaji inapenda kuutaarifu Umma kuwa watajwa ni raia wa Tanzania kwa Tajnisi.

Imetolewa na;
SSI. Paul J. Mselle
MSEMAJI MKUU WA IDARA YA UHAMIAJI

Soma pia: Singida Black Stars yawabadilisha Uraia wachezaji wanne wa Kigeni na kuwa raia wa Tanzania ili Kukidhi Kanuni

Mkuu hujaona quote ya kifungu hapo? Tafute ukisome uelewe.....sasa Gulu boy hapo anakujaje? Mbona Ngungo boy nayeye amekuja na mkeka wake anataka kuwapa uraia kina Mavambo
Screenshot_20250123-173006~2.png
 
Walilidhia kuwa raia wa nchi hii au ndo upepo tu wa kisiasa,yaani wastaafu wakae nanjilinji kulima magimbi kweli,hiyo haiwezekani, wakimaliza mission bongo watarudi kwao aminini nawaambia.
 
Hapa kuna msukumo wa kisiasa. Watu wanalitafuta kombe la AFCON kwa udi na uvumba.

Huko nyuma niliwahi kushauri hili suala kwa hiyo napata wakati mgumu kulipinga sasa hivi.

Nimewahi kusema hata wachezaji tunaowaleta kucheza ligi yetu, tukitambua wale wazuri sana halafu hawana rekodi za kuchezea timu za taifa huko watokako, tuwape uraia chap kwa haraka.

Mimi sina shida na kuwapa uraia wachezaji wenye asili ya Tanzania walioko huko nje, swali langu la msingi, wamekana uraia wao wa huko nje kama matakwa ya sheria zetu za uhamiaji zinavyotaka?

Kama tumeamua kufumba macho, kwa nini sasa tusibadili sheria za uhamiaji kama tumeona suala la uraia pacha lina faida. TFF hawana mamlaka ya kuvunja sheria za nchi.
 
Ni ukweli usio pingika kwamba sheria zimepindishwa sana ili kutoa uraia kwa wachezaji wa Singida Black Stars
View attachment 3211250

Hili swala halipaswi kuachwa lipite hivi hivi.
Sasa hapa Mwigulu anahusikaje? Hili ni jambo la kisheria. Sheria iliyotumika imenukuliwa kwenye taarifa ya Uhamiaji. Ukihitaji ufafanuzi zaidi unaweza kwenda ofisi za Uhamiaji. Kupiga kelele humu hakutasaidia.
 
Sema wabongo mna nongwa na wivu wakipumbavu sana,
Kwa kipi cha maana mumelifanyia taifa lenu ata mkapata wivu wote uwo kwa hao watu wa 3 kupewa uraia wa tz ?

Ivi uraia wa tz nao ni wa kuulilia na kuonea wivu kweli? 😄
Naomba Diarra apewe uraia
 
Uraia wa Tanzania unarejelewa kwa mujibu wa vifungu vya 9 na 23 vya Sheria ya Uraia ya Tanzania, Sura ya 357.

Hapa kuna muhtasari wa vifungu hivyo:

Kifungu cha 9: Uraia kwa kuzaliwa
Kifungu hiki kinabainisha kuwa mtu anakuwa raia wa Tanzania kwa kuzaliwa ikiwa:
  • Alizaliwa nchini Tanzania.
  • Alizaliwa nje ya Tanzania na angalau mzazi mmoja ni raia wa Tanzania wakati wa kuzaliwa kwake.

Kifungu cha 23: Uraia kwa njia ya kujiunga
Kifungu hiki kinatoa mchakato wa mtu anavyoweza kupata uraia wa Tanzania kwa njia ya kujiunga, ambayo inaweza kujumuisha:
  • Kuomba uraia baada ya kuishi nchini kwa kipindi fulani.
  • Kuthibitishwa kuwa na tabia njema.
  • Kufuata taratibu zinazohusiana na ombi la uraia.

Kifungu cha 9 cha sheria hiyo kimetumikaje , kama sio uhamiaji unawazuga watanganyika???
 
Hakuna shida, tupo watu 60M+wakiongezeka watstu kuna shida gani? Ardhi yetu ipo kibao, lakini ukiuliza, wangapi wanamiriki hata Robo heka!aibu! Waje tu
 
TAARIFA KWA UMMA​
Idara ya Uhamiaji inapenda kutoa ufafanuzi wa taarifa zilizochapishwa na kujadiliwa kwenye mitandao ya kijamii na Vyombo vya Habari kuhusu kupatiwa uraia wa Tanzania wachezaji watatu wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Singida Black Stars.

Wachezaji wanaotajwa kwenye taarifa hizo ni kama ifuatavyo:-
1.Emmanuel Kwame Keyekeh (Ghana),
2.Josephat Arthur Bada (Cote d'Ivoire), na
3. Muhamed Damaro Camara (Guinea).

Wachezaji tajwa waliomba na kupewa uraia kwa mujibu wa vifungu vya 9 na 23 vya Sheria ya Uraia ya Tanzania, Sura ya 357.

Kwa muktadha huo, Idara ya Uhamiaji inapenda kuutaarifu Umma kuwa watajwa ni raia wa Tanzania kwa Tajnisi.

Imetolewa na;
SSI. Paul J. Mselle
MSEMAJI MKUU WA IDARA YA UHAMIAJI

Soma pia: Singida Black Stars yawabadilisha Uraia wachezaji wanne wa Kigeni na kuwa raia wa Tanzania ili Kukidhi Kanuni

Hii nchi ina vituko sana. Sasa Kayeke kweli ndo amepelekea sheria ivunjwe? Mbona kama nchi tuna wachezaji wengi wazawa wenye vibaji kumzidi? Kama inshu ilikua kupata wachezaji wa Timu ya Taifa, mngeenda kitafuta wachezaji wanaocheza ligi kubwa Ulaya. Imagine Uhamiaji walimzingua Ilankunda anayechezea Fc Bayern Munich, huku wanawapa Uraia hao wacheza chandimu. Hii ni nini?

Mh. Rais anahujumiwa sana. Nitashangaa kama hatawashughulikia wote waliohusika na saga hilo.
 
Dr. Anna P. Makakala, Commissioner General wa UHAMIAJI, amechoka tangu enzi ya JPM.
Hata itumbi ,kule chunya ,wachina wengi wamenunua uraia wa Tanzania,na wamepewa uraia
 
TAARIFA KWA UMMA​
Idara ya Uhamiaji inapenda kutoa ufafanuzi wa taarifa zilizochapishwa na kujadiliwa kwenye mitandao ya kijamii na Vyombo vya Habari kuhusu kupatiwa uraia wa Tanzania wachezaji watatu wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Singida Black Stars.

Wachezaji wanaotajwa kwenye taarifa hizo ni kama ifuatavyo:-
1.Emmanuel Kwame Keyekeh (Ghana),
2.Josephat Arthur Bada (Cote d'Ivoire), na
3. Muhamed Damaro Camara (Guinea).

Wachezaji tajwa waliomba na kupewa uraia kwa mujibu wa vifungu vya 9 na 23 vya Sheria ya Uraia ya Tanzania, Sura ya 357.

Kwa muktadha huo, Idara ya Uhamiaji inapenda kuutaarifu Umma kuwa watajwa ni raia wa Tanzania kwa Tajnisi.

Imetolewa na;
SSI. Paul J. Mselle
MSEMAJI MKUU WA IDARA YA UHAMIAJI

Soma pia: Singida Black Stars yawabadilisha Uraia wachezaji wanne wa Kigeni na kuwa raia wa Tanzania ili Kukidhi Kanuni

Majibu mafupi sana!
 
Back
Top Bottom