Idara ya uhamiaji yatoa ufafanuzi dhidi ya wachezaji wa kigeni Singida Black Stars, wote ni raia wa Tanzania kwa Tajnisi

Idara ya uhamiaji yatoa ufafanuzi dhidi ya wachezaji wa kigeni Singida Black Stars, wote ni raia wa Tanzania kwa Tajnisi

Sema wabongo mna nongwa na wivu wakipumbavu sana,
Kwa kipi cha maana mumelifanyia taifa lenu ata mkapata wivu wote uwo kwa hao watu 3 kupewa uraia wa tz ?

Ivi uraia wa tz nao ni wa kuulilia na kuonea wivu kweli? 😄
Hauko timamu kichwani, Yaani akili zako zinawaza Leo tu. Vipi timu zote za ligi kuu au daraja la Kwanza zikifuata huo utaratibu wewe unaona itakuwa Sawa Tu.
 
Inawezekana wamepewa kwasababu ya vipaji vyao,acha watusaidie nashno timu maana sisi wenyewe hatujiwezi . Mbumbumbu na wao hawataki kupitwa na huu upepoView attachment 3211254
Ninavyofahamu maombi ya uraia wa Tanzania anatakiwa kuomba mhusika mwenyewe.
Pili anayetoa uraia wa Tanzania ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na siyo Kamishna Jenerali wa Uhamiaji. Sasa hawa Simba (kama hii barua imetoka kwao) hawana mwanasheria awasaidie kuwaleza kuhusu utaratibu wa kisheria wa kuomba uraia wa Tanzania? Au wamesukumwa na mihemko tu.
 
Kwamba izo timu za ligi zote wakiomba hao raia wakigeni wapewa uraia ndo wataijaza tz yenu ama mtathirika na nin labda? Acheni roho mbaya
Kwa hiyo hatuna haja ya kuwa na idara ya uhamiaji , hivyo mtu yeyote aruhusiwe kuwa raia wa TZ kisa tuna maeneo ya kutosha? Yaani unafikiri itaishia Kwa timu za mpira tu ikiwa itakuwa rahisi tu kuwa raia wa hii nchi. Kwa hiyo na wale wakimbizi wawe wanapewa uraia kisa tuna maeneo ya kutosha?
 
TAARIFA KWA UMMA​
Idara ya Uhamiaji inapenda kutoa ufafanuzi wa taarifa zilizochapishwa na kujadiliwa kwenye mitandao ya kijamii na Vyombo vya Habari kuhusu kupatiwa uraia wa Tanzania wachezaji watatu wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Singida Black Stars.

Wachezaji wanaotajwa kwenye taarifa hizo ni kama ifuatavyo:-
1.Emmanuel Kwame Keyekeh (Ghana),
2.Josephat Arthur Bada (Cote d'Ivoire), na
3. Muhamed Damaro Camara (Guinea).

Wachezaji tajwa waliomba na kupewa uraia kwa mujibu wa vifungu vya 9 na 23 vya Sheria ya Uraia ya Tanzania, Sura ya 357.

Kwa muktadha huo, Idara ya Uhamiaji inapenda kuutaarifu Umma kuwa watajwa ni raia wa Tanzania kwa Tajnisi.

Imetolewa na;
SSI. Paul J. Mselle
MSEMAJI MKUU WA IDARA YA UHAMIAJI

Soma pia: Singida Black Stars yawabadilisha Uraia wachezaji wanne wa Kigeni na kuwa raia wa Tanzania ili Kukidhi Kanuni

Wawape na akina Max jamani.
 
Kwamba izo timu za ligi zote wakiomba hao raia wakigeni wapewa uraia ndo wataijaza tz yenu ama mtathirika na nin labda? Acheni roho mbaya
Shida ni kwamba unakuta mchezaji mwenyewe siye aliyeomba bali kuna msukumo wa kisiasa maana Singida BS wana wachezaji wengi sana wa kimataifa zaidi ya idadi inayohitajika.

Ko career yake ya mpira ikiisha hawezi baki bongo.

Mwigulu aache ubabaishaji na tai yake ya kitapeli.
 
Kwa Maafisa Elimu Kata zote, Wakuu wa Shule za Serikali za Msingi na Sekondari, Moshi Manispaa, Kilimanjaro

Mkurugenzi wa Manispaa, Mwajuma Nasombe, kwa mamlaka aliyonayo, anawataka watumishi wote kuchangia fedha kwa ajili ya "Get Together" ya Watumishi Wote wa Moshi Manispaa, ikiwa ni sherehe ya kuukaribisha Mwaka 2025. Sherehe hii itafanyika tarehe 01.02.2025.

Kiwango cha Kuchangia

Wakuu wa Idara na Vitengo, Waratibu Elimu Kata, Wakuu wa Shule za Sekondari, na Walimu Wakuu wa Shule za Msingi: Tsh 50,000/-
Walimu Wote: Tsh 30,000/-
watumishi wengine: Tsh 20,000/-

Mwisho wa kuchangia ni siku ya 26.01.2025 bila kukosa.

Angalizo

Hata hivyo, ni muhimu kuwajulisha watumishi kuhusu baadhi ya masuala yanayohusiana na zoezi hili la kuchangia fedha:

1. Ushirikishwaji: Watumishi wengi hawajashirikishwa kabla ya tangazo hili. Ushirikishwaji wa awali ni muhimu ili kuhakikisha kuwa kila mmoja anafahamu lengo la michango hii.

2. Kamati ya Kuratibu: Hakuna kamati iliyoundwa kwa ajili ya kuratibu zoezi hili. Kukosekana kwa kamati kunaleta hofu miongoni mwa watumishi kuhusu matumizi ya fedha zao.

3. Muda wa Tangazo: Tangazo hili limetolewa muda mfupi sana, kuanzia tarehe 23.01.2025 na mwisho wa kuchangia ni tarehe 25.01.2025. Hii inapunguza nafasi ya watumishi kupanga na kujiandaa kwa michango yao.

4. Mshahara na Madeni: Watumishi wengi wamepokea mshahara wao na tayari wameshatumia kwa kulipa madeni wanayodaiwa. Hali hii inawafanya wengi kuwa na wasiwasi kuhusu kutoa michango zaidi.

5. Kujulishwa kwa Mkuu wa Wilaya: Mkuu wa Wilaya hajajulishwa kuhusu ukusanyaji huu wa fedha za michango, jambo ambalo ni muhimu ili kuweza kufuatilia matumizi ya fedha hizo.

6. *Kuchoshwa na Mkurugenzi:*Watumishi wengi wanasema wanachoshwa na mkurugenzi huyu, kwani mara kwa mara anaitisha michango. Wengi wanahisi kuwa huenda hii ni sehemu ya fedha za kampeni yake kuelekea kwenye uchaguzi wa ubunge.

Ombi

Kwa kuzingatia masuala haya, tunaomba zoezi hili lisitishwe hadi pale ambapo itakapofanyika mabadiliko yanayohitajika ili kuhakikisha kuwa watumishi wanashirikishwa ipasavyo na michango inakusanywa kwa njia ya uwazi na uaminifu.
Hii itasaidia kujenga uhusiano mzuri kati ya watumishi na uongozi wa manispaa.

Tunatumai kuwa maelezo haya yatasaidia katika kueleweka kwa sababu za kutokubali michango hii na kutafutwa kwa suluhisho la kudumu litakalowafaidi watumishi wote wa Moshi Manispaa.

Ahsanteni.
 
Nadhan wee dish limeyumba kwan taratbu ya uraia wa Tanzania ukoje?
Ngoja nikupuuzie tu, ili maisha yaendelee. Endapo utajibu hii, mimi sitakujibu chochote tena kuhusu hili.
Kumbuka: Mtu yeyote anayetanguliza matusi na maneno ya kuudhi anapojenga hoja yake........lazima kutakuwa na walakini kwenye akili yake.
 
Stop engine wewe.....watchu talkin bout .....Mwigulu in the building



yeah babyyyyyyyu
 
Back
Top Bottom