Idara ya uhamiaji yatoa ufafanuzi dhidi ya wachezaji wa kigeni Singida Black Stars, wote ni raia wa Tanzania kwa Tajnisi

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
TAARIFA KWA UMMA​
Idara ya Uhamiaji inapenda kutoa ufafanuzi wa taarifa zilizochapishwa na kujadiliwa kwenye mitandao ya kijamii na Vyombo vya Habari kuhusu kupatiwa uraia wa Tanzania wachezaji watatu wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Singida Black Stars.

Wachezaji wanaotajwa kwenye taarifa hizo ni kama ifuatavyo:-
1.Emmanuel Kwame Keyekeh (Ghana),
2.Josephat Arthur Bada (Cote d'Ivoire), na
3. Muhamed Damaro Camara (Guinea).

Wachezaji tajwa waliomba na kupewa uraia kwa mujibu wa vifungu vya 9 na 23 vya Sheria ya Uraia ya Tanzania, Sura ya 357.

Kwa muktadha huo, Idara ya Uhamiaji inapenda kuutaarifu Umma kuwa watajwa ni raia wa Tanzania kwa Tajnisi.

Imetolewa na;
SSI. Paul J. Mselle
MSEMAJI MKUU WA IDARA YA UHAMIAJI

Soma pia: Singida Black Stars yawabadilisha Uraia wachezaji wanne wa Kigeni na kuwa raia wa Tanzania ili Kukidhi Kanuni

 
Ni ukweli usio pingika kwamba sheria zimepindishwa sana ili kutoa uraia kwa wachezaji wa Singida Black Stars


Hili swala halipaswi kuachwa lipite hivi hivi.
 

Attachments

  • Screenshot_20250123_165908_com.android.gallery3d.jpg
    247.1 KB · Views: 6
Weka nakala ya kibali cha uraia hapa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…