Black Butterfly
Senior Member
- Aug 31, 2022
- 130
- 368
Ndugu zangu, binfasi natambua na kuheshimu kabisa hili suala la kufanya Mazoezi ya Utayari kwa sababu lina manufaa lakini bado napata shida sababu za kutangaza matukio hayo kwenye Vyombo vya Habari tena kwa kutaja idadi ya waathirika, aina ya Chombo kilichopata ajali na eneo.
Hivi hawa watu hawaoni kuwa taarifa hizo zimekuwa zikizua taharuki bila sababu za msingi kwa wananchi hasa wenye ndugu na jamaa wanaokuwa safarini? pamoja licha ya lengo zuri la mazoezi hayo lakini sioni sababu ya kutangazia umma kuwa kuna ajali.
Hizi idara za Uokoaji na Mamlaka husika zifanye Mazoezi yao kama zinavyotakiwa na Sheria lakini watoe Taarifa zinazohusu Zoezi hilo mapema na sio Kutangaza Ajali na kisha kukanusha baada ya muda wakati wanakuwa wameshasababisha usumbufu kwa Wananchi.
Ni hayo.