Idea; kuanzisha kituo cha mafuta ya kula

Idea; kuanzisha kituo cha mafuta ya kula

Kajeba

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2020
Posts
1,057
Reaction score
2,364
Wakuu

Nimekaa natafakari nianzishe biashara gani ambayo itakuwa unique kwa kiasi fulani na kuniwezesha kupiga pesa bila purukushani na kabla ya ushindani kuwa mkubwa

Nimeona nije na wazo hili pia nawaomba wanajukwaa kushauri zaidi na kuliboresha pia

Nimefikiria kutoka na WAZO LA KITUO CHA MAFUTA YA KULA, ndio nafikiria kuanzisha kituo cha mafuta ya kula tu pasipokuchanganya na bidhaa zingine

Hapa nitachanganya mafuta ya kula ya aina zote na yatauzwa kwa bei ya chini kidogo tofauti na wauzaji wengine wa rejareja

Biashara hii naona naweza kuifanya maeneo mengi ya jiji la Dar es salaam yenye mzunguko mkubwa wa watu

Nachowaomba wanajukwaa ni yafuatayo;
1.wapi nitatunua mafuta ya jumla yanayokuwa yamepakiwa kwenye madumu ili nikiyapata niyauze rejareja kuanzia robo lita

2. Kiwango cha mtaji ninachoweza kuanza nacho ni milion 2, je kinatosha kuanza biashara hii?

3. Faida katika biashara hii inaweza kuwa kiasi gani pia risks zake ziko vipi

Nawasilialsha
 
Mafuta ya kula ya aina gani..yale yatokanayo na mimea kama alizeti..karanga..ufuta..korosho..mawese ama parachichi ama mafuta ya tokanayo na wanyama.??

Wazo jema sana..kila la kheri.

#MaendeleoHayanaChama
 
Mafuta ya kula ya aina gani..yale yatokanayo na mimea kama alizeti..karanga..ufuta..korosho..mawese ama parachichi ama mafuta ya tokanayo na wanyama.??

Wazo jema sana..kila la kheri.

#MaendeleoHayanaChama
Nafikiri mafuta ya alizeti na yanayofanana na hayo katika mapishi
 
[emoji23][emoji23]
Wazo unalo na ni wajibu kulifanyia utafiti kwanza kabla ya kuwauliza wengine. Kwa mfano, fatilia utanunua mafuta ya jumla na kwa bei gani, wenzako wanaouza wrejareja wanauza kwa bei gani na wewe utauza bei gani. Umesema bei yako itakuwa chini kidogo, kwa tofauti gani na je itakupa faida? Location uliyochagua umeitafiti kuwa yatakuwa yanatoka na hakuna competition kubwa?. Tafiti yote hayo alafu leta mrejesho tukushauri, kwani hilo ni wajibu wako ili upate ushauri sahihi.
 
Mkuu inamaana kuna mashine kabisa inakuwepo eti?

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
Yes, hizo bidhaa zote nilizoziweka ziko kwenye ATM machine. Kama ni maziwa fresh pale Bomang'ombe unakuja na dumu la size yako, unalipa, jamaa anabonyezabonyeza kama "sheli", unakunywa hapohapo. Kituo cha Mawasiliano Dar hivyohivyo. Unakinga maji yako unapeleka home unakunywa sawa na aliyenunua Uhai/Afya/Hill water n.k
 
Back
Top Bottom