Idea: Mama Samia njoo na ‘Fturu na Mama’ kwa watu wenye uhitaji

Cantona fundi mkuu

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2023
Posts
295
Reaction score
313
Mko poa wakuu

Nmepata wazo nimeona niwape mumpelekee mama au watu wake wa karibu..

Njooni na iftari ya FTURU NA MAMA..
Hii iwe km give back tu commonly..
Ifanyike kwny chungu cha 28 au 29.

Wahusika wa iftari hii wawe watu wenye uhitaji maalumu km yatima, walemavu wasiojiweza kiuchumi, na maskini..
Kuna makundi na mashirika mbali mbali wanaowajua hao watu hivyo wapewe mualiko wa kula ftari na raisi..

Hii kwanza kiimani ni atapata swawabu pia kisiasa jamii italipokea vzur sana hili na kuona ni raisi anaejali watu wote.

Pia baada ya ftari kuwe na give back tu commonly. Wahitaji hao wapewe Mchele,nyama na vitu mbali mbali kwa ajili ya skukuu hata zile gesi wapewe hao ndo wanauhitaji sana kuliko wale mnaowapa..

Onyo msije mkaalika watu maarufu na matajiri kama wengi wanavyo fanya.
Pia kusiwe na mashati ya kijani..

Kusema ukwel mama mtaani akubariki ki ivyoooo.. ila akija na hii FTURU NA MAMA wale wote waliokuwa wanampinga lazma watamsifia kwa kuwafturisha watu wenye uhitaji.

Naomba kuwasilisha wazo langu mengne mtajazia wenyewe..
Pia hata makampuni mnaweza mkaandaa kitu km icho alafu mkamuita mama awe mgeni rasmi..

Ukisema huu Uzi kwa jicho la upinzani au uchadema chadema lazma povu likutoke bila sababu za msingi.
Ila kwa jicho la tatu hili jambo Lina utu ndani yake.



Kwa mahitaji ya;
content creator
Videographer
Photographer
Graphic designer
Digital marketer

0692477610 Whatsapp
 
Fturu na ftari ndo nini
 
Mawazo mfu
Kufuturisha ni ibada ya mtu kutokana na feeling yake juu ya jambo fulani moyoni mwake, huwezi kumpangia mtu sehemu ya kutoa sadaka yake, tofautisha hamasa na ibada
 

Ubepari ulioasisiwa na Azimio la Zanzibar chini ya utawala wa Mzee ruksa ni mbaya sana .

Ubepari unatoa mwanya kwa watawala wachache kuiba mali za umma kwa kushirikiana na wageni kisha kugeuka na kuwa malaika wa nuru kwa kutoa misaada na sadaka kupitia pesa zilizotakiwa zijenge taasisi za umma.

Hivi pesa za TASAF zinasanufaisha wafanyakazi wa TASAF au maskini .
Miaka zaidi ya 20 TASAF ipo lakini kaya maskini kamwe hazijawahi kuinuka zaidi ya Familia zenyewe kujiinua kwa kupambana na kilimo na elimu kwa watoto wao kusoma kwa bidii . Lakini kwa miaka yote wafanyakazi wa Tasaf wanaoneemeka na pesa za Tasaf ukilinganisha na walengwa ni mbingu na ardhi .

Simina tu ya kuwatambua maskini inafanyika karibu mwezi mzima kila mwaka halafu Watu wanalipana posho kubwa kila siku kuliko pesa anayopewa huyo maskini kwa mwaka mzima .
Ubapari ni unyama .
Bandari yetu imeuzwa na sasa TANESCO kuna dili litapigwa huku elfu kumi ikifyatuliwa mpya na dili kupigwa halafu watu waliofunga kwa umri wa zaidi ya miaka 40 wanapewa tende na uji wa siku moja kwa pesa walizotakiwa walipwe kutokana na makusanyo ya bandari ya Mungu ,mlima Kilimanjaro wa Mungu ,fukwe za bahari ya Mungu ,mauzo ya samaki wa Mungu ,mauzo ya wanayama wa Mungu ,mauzo ya madini ya Mungu ,mauzo ya gesi ya Mungu inayoitwa ya asili na umeme wa nishati ya Mungu ya maji n.k
Hiyo ndiyo keki ya Taifa inapaswa kugawiwa kwa kila mtu kila mwezi hata kama ni elfu 20 na sio wachache kujilimbikizia mali kwa mgongo wa umma kisha wanajifanya ni miungu wa kutoa chakula cha mana kwa wana wa Israel au kugawa samaki na mikate kimiujiza kwa wana wa Israel kama Yesu .
Uchaguzi ukifika wanaua watu na kuongeza kura kwenye sanduku ili aonekane amepata kura nyingi za kishindo .
Rushwa utoe ,
Futar utoe ,
Bahasha utoe
Ujenge misikiti
Ujenge makanisa
Uwape viongozi wa dini pesa
Mabango nchi nzima tangu kuingia ikulu .
Kubambikizia kesi wapinzani .
Vitisho na kuteka na kuua .
Bado tena uongeze kura za wizi.
Bado kuengua wagombea .
Kutangaza kwa nguvu aliyeshindwa .

Halafu Machawa wanasema ,Mama anakubalika sana .
Labda anakubalika zaidi kuzimu na kwenye familia za Kifreemason na mawakala wao kama wanamziki wa Singeli 😂😂😂😂😂Na wale wanaoeneza ujinsia moja moja kwa moja .
 
Kweli we ni kuku
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…