Idea: Tunatafuta watu waliokimbia

Idea: Tunatafuta watu waliokimbia

Old Member (Retired)

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2012
Posts
3,401
Reaction score
1,610
Nimefikiria sana nikagundua hii ni moja ya fursa iliyo wazi kabisa.

Wasichana wengi wa kazi wamekuwa wakitoroka kwa maboss zao wakiwa wameiba, wafanyakazi pia wamekuwa wakiiba kwenye maofisi na wakikimbia. Hili tatizo limekuwa likizidi kukuwa hivyo mimi ninataka kuja na suluhisho

Nataka kufungua kampuni ambayo itakuwa na kazi ya kutafuta hawa watu waliokimbia kwa makusudi kwa gharama nafuu.

Ninachotaka kukifanya ni kutumia njia kama wanazotumia wanasiasa kutrack mawasiliano ya mtu, hivyo huyo mtu aliyekimbia nitahitaji namba yake ya simu na mchezo utakuwa umekwisha.

Karibu kwa michango katika kuboresha wazo hili, kama umelipenda hili wazo na unadhani we can do it karibu pia.
Ninahitaji masaada mkubwa sana hapo pa ku track mawasiliano ya mtu au kama unaweza kunipa connection ya mtu mwenye ujuzi huo..
 
Sio mahausigeli tu hata wadeni tutakua tunawatafta
 
naona tunaelekea pazuri, watu wamekuwa wabunifu sana. subiri wazoefu na wenye ujuzi wakupe mawazo
 
Ni wazo zuri sana,inabidi uwe mtaalam wa IT, Uingie ubia na makampuni ya simu,polisi kuwe ni kwako kwaajili ya kupata RB.......
 
Ni wazo zuri sana,inabidi uwe mtaalam wa IT, Uingie ubia na makampuni ya simu,polisi kuwe ni kwako kwaajili ya kupata RB.......
Asante mkuu, asahv nipo kwenye mchakato wa kukusanya mawazo kwakuwa naona challenge kubwa iliyo mbele yangu ni jinsi ya kupata mawasiliano yake huyo mtu kutokana na ukiritimba wa TCRA pamoja na polisi
 
Penye nia pana njia utafanikiwa tu, zaidi tafuta upenyo wa elimu au habari juu ya hayo mambo kuanzia TCRA,makampuni ya simu na polisi hakikisha katika vitengo hivyo unapata rafiki.
 
ni wazo zuri sana,tena kwa hapa Dar utapata wateja wengi sana.
 
wazo nzuri ila sidhani kama ni vilaza hivo,mtu atoroke halafu asibadili namba ya simu?
 
Ongea na wanausalama uone kama kuna uwezekano wa kufungua kampuni Binafsi ya Upelelezi, vinginevyo utakumbana na vikwazo vingi kisheria, ukikutana na wahalifu wenye nguvu/akili watakufunga wewe mwenyewe. Nilishawahi kuwaza kitu kama hicho, na hata sasa nina wazo zuri sana tofauti na hilo tatizo linahitaji pesa nyingi na nahofia nikiliwasilisha sehemu kwa ajili ya funding litaibiwa tu.
 
wazo nzuri ila sidhani kama ni vilaza hivo,mtu atoroke halafu asibadili namba ya simu?

UMEBUGI! kubadili namba hakufuti trail yako mkuu, nakukamata asubuhi mapemaa!
 
Ongea na wanausalama uone kama kuna uwezekano wa kufungua kampuni Binafsi ya Upelelezi, vinginevyo utakumbana na vikwazo vingi kisheria, ukikutana na wahalifu wenye nguvu/akili watakufunga wewe mwenyewe. Nilishawahi kuwaza kitu kama hicho, na hata sasa nina wazo zuri sana tofauti na hilo tatizo linahitaji pesa nyingi na nahofia nikiliwasilisha sehemu kwa ajili ya funding litaibiwa tu.
Pesa nyingi sh ngapi mkuu?
 
TCRA sio tatizo wala polisi unachohitaji polisi wakupe tu kibali cha kuweza kumtafuta huyo mtu basi usiwategemee polisi kwa lengine lolote ama kuhusu taarifa za simu unahitaji kuwa na ukaribu na makampuni ya sim wao ndo huwa wanatoa call records na IMEI na BTS location hapo ndo kimbembe kinapoanzia huwa hawapo cooperative kaabisaaa utaomba hizo info mpk ukipewa mtu kashaondoka hilo eneo kabisa.

Imei itakusaidia kujua huyo simu imewekwa line nyingine ama la na utajua pia namba ya hio line, ila hizi info kuzipata ni rahsi km telecom operators watakuwa cooperative ambayo ni nadra sana kwao kila mmoja atakwambia Imei haitumii tena line ya tigp kachek na other operators ambao kila mmoja atakuwa anamrusshia mwenzie mpira. Anyway jaribu hizo ni challenge tu nakupa taarifa zitakukuta, m mwenyewe nitafurah kukiwa na hio kampuni ni ndugu yangu kapotea mwezi ss na hatujampata .
 
Mouramo

Asante sana mkuu, nitafanyia kazi ushauri wako. Ndugu yako amepotea au amekimbia? alikuwa na akili timamu (samahani)? alikuwa na simu?
 
Last edited by a moderator:
Kibongobongo utapambana na changamoto nyingi sana mana mtu kubadili simu au laini ni jambo jepesi sana.....
 
CHIPS DUME

Huwa akili.zinamruka lkn kw mwaka mara moja ss hatujui alipoondoka alikuwa na akili zake ama laa
 
Last edited by a moderator:
Ongea na wanausalama uone kama kuna uwezekano wa kufungua kampuni Binafsi ya Upelelezi, vinginevyo utakumbana na vikwazo vingi kisheria, ukikutana na wahalifu wenye nguvu/akili watakufunga wewe mwenyewe. Nilishawahi kuwaza kitu kama hicho, na hata sasa nina wazo zuri sana tofauti na hilo tatizo linahitaji pesa nyingi na nahofia nikiliwasilisha sehemu kwa ajili ya funding litaibiwa tu.

mkuu hizo funds huwa mnatafuta wapi?..... i have a lot of business idea but finance ndo inanirudisha nyuma
 
Back
Top Bottom