Masamila
JF-Expert Member
- Jun 22, 2014
- 6,490
- 7,422
Nimefanya karesearch kangu private kadogo na yafuatayo ni mawazo yangu kuhusu ufugaji wa mbuzi bila kuchungwa.
Nitatumia case ya mbuzi 110 hawa nitawaterm kama "mbuzi wazalishaji" au "parent stock" ambapo miongoni mwao madume ni 10 na majike ni 100.
Nukta ya kwanza; Mbuzi jike (mbegu specific) huzaa watoto wa nne kwa mwaka katika mikupuo miwili, hivyo kwa mwaka hao "Mbuzi wazalishaji" wanazalisha vitoto mia nne(100*4=400) kila mwaka.
Nukta ya pili: naonelea kuwa itafaa kuwachinja/kuuza mbuzi hao mia nne wanaozalishwa kila mwaka punde tu watapo fikisha umri wa miezi nane kwani baada ya umri huo growth rate inapungua kwa kiasi kikubwa. Katika umri huo wa miezi nane wanakuwa na uzito wa kilo 15 na thamani yake huwa ni shilingi elfu sabini( TSH 70,000)
Nukta ya tatu: Ulaji wa mbuzi hao tokea siku ya kwanza yaani kuzaliwa hadi umri wa miezi nane ni kilo sitini (60 KGS) (ulaji utakuwa chini ya hapo, hiyo ni maximum value). Hivyo watakula tani ishirini na nne (24 MT)
Nukta ya nne: 'Mbuzi wazalishaji' kwa idadi hiyo kwa mwaka hula chakula chenye uzito wa tani ishirini (20 MT)
Nukta ya tano: Bei ya chakula kama nikichanganya kwa nguvu zangu mwenyewe inaweza kuwa ni shilingi laki tano kwa tani(NB: sijalifanyia utafiti kuhusiana na bei ya mchaganyiko wa chakula cha mbuzi ila nimerefer chakula cha kuku kama mfugaji atanunua mwenye mchanganyiko halafu akachanganya mwenyewe)
Hitimisho: Faida yake itakokotolewa hivi ; Thamani ya Mauzo ya mbuzi waliozalishwa kutoa (gharama za ulaji wa 'mbuzi wazalishaji' + gharama za ulaji wa 'mbuzi waliozalishwa') ((70,000*400) minus (500,000*44(tons)= 28,000,000-22,000,0000=6,000,000
Faida kwa mwaka ni TSH 6,000,000
Nimalizie kwa kusema kuwa Binadamu tumetofautiana kimawazo hivyo nawe msomaji unao uwezo wa kuchangia mawazo yako kuboresha idea yangu au kujazia idea inapoacha ombwe ili mwisho wa siku tufaidike wote.