Kuna magonjwa matatu ya virusi ambayo huwashambulia mbuzi sana na hivyo Kupunguza uzalishaji na wewe kama mfugaji utahitaji kuwakinga mbuzi wako kwa kuwapa chanjo dhidi ya magonjwa hayo ambayo ni;
1. Pesti des petis ruminants (PPR)
Mbuzi hupewa akiwa na miezi 6+ na chanjo hii huwa ni ya maisha hakuna haja ya kurudia kuchanja tena
2. Caprine pox
Hupewa chanjo hii wakiwa na umri na miezi 6+ na chanjo hii hudumu kwa miaka 2 tu baada ya hapo utatakiwa kurudia tena
3. Contagious caprine pleuro pneumonia
Huchanjwa wakiwa na miezi 6+ na chanjo hii hurudiwa baada ya mwaka mmoja....
Hitimisho:
Kila baada ya miezi mitatu ni muhimu kuwapa dawa ya minyoo (Albendazole) hapa mbuzi watakuwa na afya na mwonekano mzuri
Kwa huduma hizi za chanjo tusisite kutafutana kwa wakazi wanaokaa dar na pwani tu. Karibuni sana