Idea yangu kuhusu ufugaji wa mbuzi bila kuchunga (Bandani/Zero grazing)

Nipo ndugu, si unajua shilingi imekuwa ngumu kutwa kucha twakimbizana nayo lakini haikamatiki!
Aisee we acha tu yaani hadi kizunguzungu utadhani kuna mtu anatujambia but tukomae tu maana waswahili wanasema
Itakuwa haina maana kupewa umri mrefu halafu tukawa masikini itakuwa bora kwa wale waliotangulia iwapo tutaikubali shilingi iendelee kutuponyoka.
 
Tushitikishane mbinu za kuishikilia shilingi kama hivi maana hali si hali mtaani!
 
Weka namba zako za simu mkuu.
 
Tuwe tunashtuana kwa issue muhimu kama hizi!
Haina noma kama nawe ni mdau wa hii sector tutaendelea kushtuana usijali maana huyu muanzisha mada kiukweli katugusa sana japo inashangaza nyuzi nzuri km hii eti watu wanaipita tu,mi toka siku ya kwanza niliisubscribe mapema tunaenda nayo kwa kujikongoja hivyohivyo ila IMANI yangu itakolea mwendo muda si msingi.
 
Tuwe tunashtuana kwa issue muhimu kama hizi!
Haina noma kama nawe ni mdau wa hii sector tutaendelea kushtuana usijali maana huyu muanzisha mada kiukweli katugusa sana japo inashangaza nyuzi nzuri km hii eti watu wanaipita tu,mi toka siku ya kwanza niliisubscribe mapema tunaenda nayo kwa kujikongoja hivyohivyo ila IMANI yangu itakolea mwendo muda si msingi.
 
Mleta mada tunaomba mrejesho. Maana leo nimewaza sana kuhusu hii project. Kwamba hivi inawezekena kufuga mbuzi bila kuwachunga? Yaan ukawafugia bandani kwa kuwaletea chakula? So naomba mrejesho wa mafanikio yako katika hii project
 
Kiukweli kufuga mbuzi bila kuwachunga ni gharama kubwa sana! nimeona hapo juu kuna mchangiaji ameongelea kuhusu chakula cha mahindi, ila sie tuliowahi kufuga mbuzi chakula cha mahindi au pumba sio Nzuri kwa mbuzi na hupelekea kuumwa na Tumbo hasa la kuharisha! bado ufugaji mkubwa unataka sana kutafuta njia Nzuri ya malisho, na mbuzi wanasumbua sana, wakiwa na njaa watapiga sana kelele na ukiwatoa tu kama kuna Mihogo ya jirani lazima ujiandae kulipa!
Naona lililo jema ukitaka kufanya vzr ktk ufugaji huu wekeza pia kwa wafanyakazi walau wawili wenye kujitambua na wape Majukumu, weka uzio mkubwa kuzunguuka banda ili hata kama utaachia basi wazunguke mle mle ndani ya Uzio wako ambao pia unaweza kuupanda majani, wastani wa uzio uzunguuke walau ktk heka Mbili hasa kwa idadi ya Mbuzi 110.
 
Kuna taasisi ya serikali ipo Kibaha Makurunge, wanauza mbegu za nyasi za malisho ya wanyama, ukinunua ukazipanda zinashusha gharama kwa kiasi kubwa.
Ratio ya Mbezi jike kwa dume ni 1:25 yaani dume mmoja anaweza kuhudumia majike 25.
Chanjo ni muhimu uzuri ukiwapa chanjo zinachukua Kati ya mwaka mmoja na kuendeleza Hadi uwape chanjo nyingine.
 
Nikiwa na ekari moja inaweza kumudu mbizi wangapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…