IDF Jeshi bora kabisa duniani na MOSSAD idara bora zaidi ya ujasusi duniani!

Mzee wangu umeona udhaifu wa IDF katika kuzuia surprise atracks.Je hilo linaondoa ubora wao katika kujilinda dhidi ya mahasimu wao???
 
Yom Kippur pale Anwaar Saadat alisababisha kufeli mpaka akauwawa ,vita walikuwa wameikamata yeye akagoma kusonga mbele na moto ule ule wa mashambulizi mpaka Wapinzani wakajipanga kushambulia kwa nguvu ,kiufupi Saadat nia yake haikuwa kusonga mbele bali ni kuvunja ule ukuta wa Isarael na kuikomboa Sinai Peninsula basi.

Matokeo ya ile vita unayajua viongozi wawili Wazito yule bibi na Moshe Daiyan kujiuzulu na Egypt kurudishiwa Sinai Peninsula.
 
Nelson....
Nipo.
Nichangie nini hapa?
Yote yanasikotisha.
Kwanza shikamo mzee wangu nikutakie heri...
Mimi nilikua nahisi na wewe una misimamo ile ya wanajeshi wa IDF wakiua raia wasio na hatia unashangilia au ile ya vikosi vya HAMAS na PLFP na PLO na HIZBULAH au ISS vikiua raia wasio na hatia unashangalia.
Usisikitike sababu hii dunia uhai wa binadamu umekua ni chombo cha wanasiasa kucheza nacho.
Vita haina mshindi bali inazaa visasi kwa karne hadi karne.
Pole mzee wangu najua unaumia na kusikitika kwa uhai wa binadamu kupotea kirahisi rahisi hivyo.
Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema akutie nguvu mzee wangu.
 
Adriz,
Sadat hakusonga mbele kwa amri ya Marekani.

Nadhani Mohamed Heykal katika kitabu chake, "The Road to Ramadan," kaeleza haya.

Kitendo hiki kilimvunja nguvu Hafiz el Assad kwani Syria haiwezi peke yake kupigana na Israel.

Ikawa Wayahudi wamepata haueni kubwa.

Hapo ndipo Ikhwan Muslimon wakatoa fatwa Sadat lazima auawe kwa usaliti.

Hili lilitekelezwa.

Nimefika Yom Kippur War Memorial Cairo sehemu inaitwa Heliopolis.

Kumbukumbu hii inaeleza ushindi wa Misri katika vita vile.
 
Upo sahii kabisa na niongezee haya mkuu.Majeshi ya EGPTY yasingeweza kusonga mbele maana ile brigadia ya makomando na vifaru ilikua tayari imeshazungukwa na vikosi vya Ariel Sharon na ule mfumo wa ulinzi wa anga uliokua unawalinda wanajeshi wa EGPTY dhidi ya ndege za kivita za IDF ulikua haufanyi kazi tena.
Na hapa ndipo wale mateka wengi wa jeshi la EGPYT ndipo walipotokea baada ya wanajeshi wake kujisalimisha na ukumbuke lakini makomandoo wa jeshi la EGPYT walikua wameua karibia wanajeshi 700 wa IDF na kuchukua mateka kama wanajeshi 200 na ushee.
Lakini baada ya kuzungukwa nao IDF walichukua mateka kama 2000 na waliua wanajeshi zaidi ya 3500 ambao either walijisalimisha au walipigana mpaka kifo.
Wanajeshi wa IDF walijaribu kuingia Ismailia ili waingie Cairo,lakini jeshi la Misiri liliweka vikosi imara nje ya mji wa Ismailia na kuwarudisha nyuma IDF mpaka nje ya viunga vya mji wa Isimailia.
Mpaka wanafikia makubaliano ya kusitisha mapigano,,,vyote viwili vikosi vya EGYPT NA IDF vilikua katika sinai penisula location tofauti tofauti.Wakakubaliana pia na kubadilishana mateka na miili ya wanajeshi waliokufa vitani na vikosi vya Ariel Sharon avunje ile siege aliyokua ameviwekea vikosi vya EGYPT na atoke nje ya mji wa Isimailia.
NB: Na pia kwa kuongezea usisahau makamanda wa pande zote mbili (EGYPT NA ISRAEL) katika vitengo mbalimbali walijiuzulu kutokana na matokeo ya hiyo vita.
 
Hapa ndipo watu wanashindwa kuelewa mzee wangu na sijajua ni kwa kutojua au kuukwepa ukweli uliokuepo ndani ya uwanja wa vita.Vita ile haikua na mshindi maana wakati serikali za USSR NA USA zinawalazimisha wafanye makubaliano ya amani,tayari majeshi ya EGYPTIAN yalikua ndani kabisa ya sinai penisula na majeshi ya IDF yalikua nje ya mji wa Isimailia na yameshavuka Suez canal..Wakati huo huo vikosi maalumu vya makomandoo wa maparachuti wa Syrian defense forces vilivyokua vimeiteka Golan heights katika siku za mwanzo za vita vilikua vimerudishwa mpaka ndani kabisa ya Syria..Ungesoma pia mzee wangu kitabu cha VALLEY OF TEARS.
Vita ile haikua na mshindi na walilazimishwa na USSR na USA wafikie makubaliano ya kusitisha vita na kubadilishana mateka.
Lakini ni kweli raisi wa Syria mzee Sadat alivunjika moyo kabisa maana alikua anaanda counter offensive moja ya nguvu kwa msaada wa serikali ya Iraq.
 
Kwanza mkuu hakuna sababu yeyote inayo weza kutumika kuhalalisha mauaji ya raia iwe upande wa Hamas au Israel.

Hamasi walizingua sana kwa kuuwa raia hasa kwenye tamasha la mziki kwa sababu pale kulikuwa na raia wengi wa kigeni ambao kimsingi sio wahusika wa mzozo huo?

Na pia Israel wamezingua sana jinsi ilivyo jibu mashambulizi ya Hamas kwa kushambulia makazi ya raia na kuwauwa hovyo hovyo najua labda wamepaniki kutokana na pigo walilo pata lakini Israel ilitakiwa ijitofautishe na Hamas kwa kufanya mambo kwa weledi na sio kiholela kwa sababu nyenzo za kufanya hivyo wanazo.
Na jua watu watakuja na hoja ya kuwa Hamas anaficha silaha kwenye makazi ya raia lakini tukiongea kwenye uhalisia hamas Sio wajinga kiasi hicho ,hawawezi kuficha silaha kwenye majengo hali ya kuwa wanajua kabisa ya kuwa zitalengwa kiurahis na Israel.

Kwa kilicho tokea juma mosi hakika Israel imepata pigo moja takatifu la kijeshi na kijasusi.
Kilicho ighalimu Israel na ambacho kitakuja kuigharimu siku zijazo ni tabia yake ya kujiamini kupita kiasi kwasababu anajiona anajeshi bora pia ana washirika wenye nguvu duniani ivyo kujiona anaweza kufanya anavyo taka,tabia ya namna hiyo ili iangusha Roma.
 
Safi sana. Huu Uzi tayari ulishauleta? Ukileta nicheck pia
 
Upo sahii mkuu kwa maelezo yako..
Nimependa ulivyodadavua
 
Takataka tuu hao wazee wa mbeleko.Kwanza nimeamini watu wa Kanda Ile ya Urudi wale ndio roho ya paka.

Ukraine
Russia
Afghanistan
Somali
Yemen
 
Algeria hawaahirikiani na Israel sasa wataanzaje
Kwa nje na kwa Akili nyepesi ya kimadrasa unaweza kuona hawashirikiani lkn nyuma ya pazia wanafanya mengi Sana.

Achana na siasa za dunia.
 
Nelson,
Soma kipande hicho hapo chini kutoka kwa Heykal, ''The Road to Ramadan'' hali ya vita siku za mwisho.

Labda itakusaidia kuelewa.

Napenda kukufahamisha kuwa hapa Marekani ilikuwa katika Nuclear Alert kuihami Israel.

Nuclear Alert ya nini ikiwa Israel ilikuwa inashinda vita?
Lakini ningependa unipe chanzo cha taariza zako ulizoweka hapo juu.
 
Nashukuru kwa mchango wako mzee wangu mpendwa ila tatizo mzee wangu wewe hauchambui kijeshi ila unachambua kwa kuipondea IDF kwa ujumla na kuegemea upande mmoja
Umeona uchambuzi wangu mimi nimesigusia na kukosoa majeshi ya pande zote tatu EGYPT NA ISRAEL NA SYRIA sijaegemea popote.
Mwandishi wa kitabu cha Road to Ramadan je alikuepo uwanja wa vita????
Na je mwandishi wa Road to Ramadan mtizamo wake kiitikadi ni upi au yupo sawia haegemei upande wowote???
Kweli mzee wangu utakataa kua IDF hawakufika nje ya mji wa Isimailia???
Au utakataa kua makomandoo wa Jeshi la anga la Syria hawakufanikiwa kuiteka Golan Heights kwa mda wa siku tatu?????
Na kuhusu suala la nyukilia ni USSR ndio walitishia kama vikosi vya IDF vitasonga mbele watatumia nyukilia kuilinda Egypt na ukumbuke kua ndege za kivita za Egyptian army na makombora ya mfumo wa SAF vilitoka USSR .Na USA ikatishia pia kutumia nyukilia kuilinda Israel sababu wakati ule kulikua na cold wars na ilipeleka kwa IDF dhana nyingi za kivita pamoja na ufaransa.
NB: Mm ni mchambuzi wa matukio ya kijeshi na sio mfuasi wa pande moja!!!
Ebu soma vitabu vingi vya yomm kippur war na utaielewa pande zote.
,kutoka kwa waandishi wa kiarabu na kiyahudi na utafute program ya Al jazeera inayoelezea hiyo vita.
Na mimi pia nitakisoma kitabu cha Road to Ramadan kwa umakini mkubwa mzee wangu
 
Nelson,
Hakuna popote nilikoegemea.

Nimetalii kitabu ambacho wewe umekikataa kwa kusema Mohamed Heykali alikuwapo uwanja wa mapambano?

Unamjua Heykal heshima yake katika wasomi wa dunia?
Wewe ulikuwapo?

Mimi nimekuomba unipe taarifa zako hizo nini chanzo chake?
Maana yangu ni ''documented?''

Taarifa za Heykal ni ''documented.''

Maana yake ziko bayana kwa dunia na zinatoka kwenye vyanzo vya kuaminika.

Ubongo wangu siku zote uko wazi kujifunza ndiyo nakuomba rejea.

Nimefika Ismailia, Suez na nimeona ilipokuwa Bar-Lev Line.
Nimefika Port Said, Cairo na Alexandria.

Nimesafiri kupitia Desert Road kutoka Cairo hadi Alexandria na kutoka Alexandria, Tanta, Mehalla El Kubra, Damieta na kwengine kwingi.

Nimejifunza mengi kuhusu Wamisri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…