Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Nelson...Kwanza shikamo mzee wangu nikutakie heri...
Mimi nilikua nahisi na wewe una misimamo ile ya wanajeshi wa IDF wakiua raia wasio na hatia unashangilia au ile ya vikosi vya HAMAS na PLFP na PLO na HIZBULAH au ISS vikiua raia wasio na hatia unashangalia.
Usisikitike sababu hii dunia uhai wa binadamu umekua ni chombo cha wanasiasa kucheza nacho.
Vita haina mshindi bali inazaa visasi kwa karne hadi karne.
Pole mzee wangu najua unaumia na kusikitika kwa uhai wa binadamu kupotea kirahisi rahisi hivyo.
Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema akutie nguvu mzee wangu.
Kitu gani kimekufanya wewe uhisi mimi nitafurahia kuuliwa kwa Wayahudi?
Nilikuwa na rafiki yangu tunasoma darasa moja St. Joseph's Canvent School.
Siku alipokuja kujiunga na darasa letu mwalimu alimleta ninapokaa mimi akamweka pembeni yangu na tukawa marafiki sana.
Jina lake akiitwa Israel na baba yake ndiye alikuwa Balozi wa Israel Tanzania.
Bahati mbaya sana sikumbuki jina la pili la Israel.
Six Day War 1967 ilipokuwa inaanza kila siku asubuhi Israel akinipa taarifa za jinsi majeshi ya Israel yalivyokuwa yanasonga mbele na kuyasambaratisha majeshi ya Misri, Syria, Iraq na Jordan.
Nilikuwa naumia sana.
Israel alinieleza mengi na kuwa yeye akirudi kwao ataingia jeshini nk. nk.
Nakuwekea picha hapo chini tuliyopiga tukiwa shule:
Kulia waliochutama: Edward Anthony Makwaia, Salma Bhatia, Asya Kharusi, Razia Bhatia, Iddi Mvule, David Gabba, Waliosimama kulia: Mwandishi, Shayo, Maximillian Mafuru. Kulia waliosimama: Gulamabbas Jivraj, Israel, Charles Mesquita