Nelson...
Kwa nini uke kuchukua vitabu kwangu?
Jaribu Maktaba Kuu ya Taifa na British Council Library.
Nakuwekea hapo chini moja ya kipande kuhusu IDF na Hizbullah katika mhadhara niliotoa University of Zanzibar mwaka wa 2017.
Nimekichagua kipande hiki kwani kilipendeza sana hadhira yangu.
Hili nilielezwa mwisho wa mhadhara:
''Vita iliyokuja kumaliza kile kilichokuwa kimeaaminika na dunia kuwa Wayahudi hawawezi kushindwa katika vita, ni vita vya mwaka wa 2006 kati ya Hizbullah na Wayahudi.
Vita vilipoanza fikra za wengi katika nchi za Kiarabu zilirejea katika Vita Vya Siku Sita vya mwaka wa 1967 na wengi waliamini kuwa Hizbullah watamalizwa kwa muda mfupi kwa kusagwasagwa na Israel.
Hili halikutokea.
Vita vilipiganwa kwa siku 34 katika mwezi wa Julai na Agosti hadi pale Umoja wa Mataifa ilipoingia kati na kuweka makubaliano ya kuweka silaha chini na kumaliza vita.
Wayahudi kwa mara ya kwanza katika historia ya mapambano yao na Waarabu walionekana katika stesheni nyingi kubwa za televisheni duniani wakirudi Israel kutoka uwanja wa mapambano wameinamisha chini vichwa vyao.
Israel ilikuwa kwa mara ya kwanza imeonja kipigo katika vita. Hapakuwa na shamrashamra ziliyozoeleka za ushindi dhidi ya majeshi ya Kiarabu.
Hizbullah ilikuwa imevunja, ‘’myth,’’ ile fikra ya kuwa Wayahudi hawawezekani. Hassan Nasrallah kiongozi wa Hizbullah alikuwa akiuliza wakati wa vita, ‘’Wako wapi askari wa Kiyahudi mbona hatuwaoni katika uwanja wa vita?
Tunachoshuhudia ni ndege za Kiyahudi wakipiga mabomu nyumba za raia.’’
Baada ya vita, ilipofika wakati wa kubadilishana mateka Wayahudi walipata fadhaa zaidi pale walipokuwa wao wanapokea majeneza ya askari wao waliouliwa vitani na Hizbullah na wao wakiwaachia huru askari hai wa Hizbullah.''