View attachment 1461124
Mchekeshaji huyu alikuwa akishikiliwa katika Kituo cha Polisi Oysterbay kwa takriban siku 8 akifanyiwa mahojiano.
Haijajulikana ni mashtaka gani atasomewa lakini kwa wa mujibu wa Polisi, walikuwa wakimuhoji kwa tuhuma za kujaribu kuharibu ushahidi na makosa mengine ya Kimtandao.
Endelea kufuatilia....
UPDATES
Mchekeshaji Idris amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu pamoja na mwenzake Innocent Maiga na kusomewa mashtaka yao
Katika shtaka la kwaza, Idris pekee anatuhumiwa kutumia laini yenye namba 0753 617621 ambayo haijasajiliwa kwa jina lake bali kwa jina la Innocent Maiga
Katika shtaka la pili, Innocent pekee anatuhumiwa kushindwa kuripoti ubadili wa umiliki wa laini hiyo baada ya Idris kuanza kuitumia
UPDATE
Idris amepata dhamana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kutumiza masharti yakuwa na wadhamini wawili na bond ya TZS 15,000,000/-
Kesi itatajwa tena Juni 09, 2020