Jannatul Firdaus
JF-Expert Member
- Aug 4, 2026
- 446
- 1,113
Mtangazaji, muigizaji na mtayarishaji wa filamu nchini Tanzania, Idris Sultan, amepata mwaliko mkubwa wa kuwa mmoja wa washereheshaji wa msimu wa 20 wa tuzo mashuhuri za The Future Awards Africa (TFAA) zitakazofanyika mwezi Novemba jijini Lagos, Nigeria.
Idris Sultan atajumuika kwenye jukwaa moja na watangazaji wengine wanne kutoka maeneo mbalimbali ya bara la Afrika, wakiwemo mwigizaji Genoveva Umeh (Nigeria), Priscilla Kayira (Malawi), Resego Motlhokathari (Botswana), na Claudia Nasibwa (Kenya). Hatua hii inafanya msimu huu kuwa wa kihistoria kwa kuwakutanisha watangazaji kutoka nchi tano tofauti kwenye jukwaa moja.
Tuzo hizo, ambazo mara nyingi hutajwa kama "Tuzo za Nobel kwa Vijana wa Afrika," zina lengo la kuwaenzi vijana wabunifu na viongozi wenye umri kati ya miaka 18 hadi 33 wanaofanya mabadiliko kwenye sekta za sanaa, teknolojia, ujasiriamali, na habari. Maadhimisho ya mwaka huu yataangazia mada ya "Celebrating the Redefiners: Africa's AI Generation," ikilenga kuwatunza vijana wanaotumia teknolojia na ubunifu kuleta mapinduzi barani Afrika.