Anachemka kuwekeza kwenye filamu Bongo. Kuna watu wanaitwa akina Lukaza ambao walipiga hela ya EPA wakawekeza kwenye filamu kupitia kampuni yao ya Proin Promotions, waulize nini kimewakumba?!
Walianza kwa mbwembwe wakazindua filamu ya Foolish Age pale Mlimani City, kisha wakaja na mchakato wa kusaka vipaji nchi nzima, na baadaye wakamleta star wa movie wa Ghana, Van Vicker. Lakini sasa imebaki story.
Kuna kundi la Wahindi wameikamata hii biashara kwa kuwatia ujinga wasanii na watengeneza filamu, matokeo yake filamu imageuka kuwa biashara ya mtu mmoja tu, mwingine akiibuka atashambuliwa na wasanii wenyewe hadi afulie.
Biashara ya filamu ukiiangalia kwa juu juu unaweza kuiona kama ina mafanikio makubwa, lakini kwa uhalisia wake haina lolote. Mwambieni Idris akitaka asije kuchekwa kama Richard Bezuidenhout kwa kufilisika, basi akae chini na kufikiri upya cha kufanya lakini sio filamu.
Ova