Idris Sultan

Idris Sultan

ukubwa jembe

Senior Member
Joined
Jan 6, 2014
Posts
101
Reaction score
25
Anaejua historia ya huyu kijana naomba anijuze kidogo maana naona watu wanadhani pesa alizoshinda ni nyingi sana ila namuona kama ni mtoto wa kisure inawezekana hizo ziko nyumbani nyingi tu.

Sasa kama kuna yoyote anaejua anijuze.
 
Hizo pesa ni ndogo kama upo kundi la escrow

Ni nyingi kama mtanzania wa kawaida unayeishi kwa $1

Na kwao z8ngekuwepo asingeenda bba
 
ila ni mtaji mkubwa kwa mwenye mawazo ya ujasiriamali
 
Keshasema anawekeza kwa filamu.

Anachemka kuwekeza kwenye filamu Bongo. Kuna watu wanaitwa akina Lukaza ambao walipiga hela ya EPA wakawekeza kwenye filamu kupitia kampuni yao ya Proin Promotions, waulize nini kimewakumba?!
Walianza kwa mbwembwe wakazindua filamu ya Foolish Age pale Mlimani City, kisha wakaja na mchakato wa kusaka vipaji nchi nzima, na baadaye wakamleta star wa movie wa Ghana, Van Vicker. Lakini sasa imebaki story.
Kuna kundi la Wahindi wameikamata hii biashara kwa kuwatia ujinga wasanii na watengeneza filamu, matokeo yake filamu imageuka kuwa biashara ya mtu mmoja tu, mwingine akiibuka atashambuliwa na wasanii wenyewe hadi afulie.
Biashara ya filamu ukiiangalia kwa juu juu unaweza kuiona kama ina mafanikio makubwa, lakini kwa uhalisia wake haina lolote. Mwambieni Idris akitaka asije kuchekwa kama Richard Bezuidenhout kwa kufilisika, basi akae chini na kufikiri upya cha kufanya lakini sio filamu.
Ova
 
Anaejua historia ya huyu kijana naomba anijuze kidogo maana naona watu wanadhani pesa alizoshinda ni nyingi sana ila namuona kama ni mtoto wa kisure inawezekana hizo ziko nyumbani nyingi tu.

Sasa kama kuna yoyote anaejua anijuze.

Ni Chalii wa hapo Kijenge Juu Arusha..
 
Duu huyu bwana asije geuka makimuga...maana bongo kukusifia ni ishu ila ukishafell utalijua jiji...hapa mjini inapendwa pesa tu
 
Mpaka anaondoka kwenda big brother idris alikuwa mfanyakazi wa graphics wa kampuni ya i-view iliyoyengeneza video ya nataka kulewa ya diamond platnumz
 
mpaka hapo nimeekewa jambo kumbe ni mgangaji mzuri labda anajua upana na urefu wa hiyo biashara
Lakini pia nimejua ni mkazi wa Arusha na nimeekewa maisha yake asilimia kubwa amekuwa Arusha.
Kama kuna la ziada tujuzane maana inaelekea kizungu anacho kiongea ni kama amekaa nje kidogo hebu anaejua anijuze
 
Nadhani unajua vizuri vijana wa arusha walivyo wazamiaji wa kuondoka nje na watalii. Halafu tofauti na watalii wengi wa kike kuondoka na vijana wa arusha pia arusha ina connection na Nairobi ambapo kiingereza in kawaida kwao. Pia fuatilia trend ya wawakilishi wengi wa big brother kutoka Tanzania wanatoka kaskazini arusha na moshi mfano richard, Julio, idris, Eliza Gupta, lotus na wengine.
 
Anaejua historia ya huyu kijana naomba anijuze kidogo maana naona watu wanadhani pesa alizoshinda ni nyingi sana ila namuona kama ni mtoto wa kisure inawezekana hizo ziko nyumbani nyingi tu.

Sasa kama kuna yoyote anaejua anijuze.

Hivi huyu jamaa ana Undugu na EDDIE SULTAN yule dogo aliyekuwa anatangaza ITV kipindi cha watoto miaka ya 90's ! Naona wamefanana hvi kidogo, mwenye kujua atujuze...!
 
Idris Ni mtoto wa Naima, alikuwa anakaa na babu yake na bibi pale Ngarenaro zile nyumba za manispaa zilizobomolewa, si mtoto wa kisure kiviile maisha kawaida sana.... Ila mama yake Mtu wa Bata sana
 
Anachemka kuwekeza kwenye filamu Bongo. Kuna watu wanaitwa akina Lukaza ambao walipiga hela ya EPA wakawekeza kwenye filamu kupitia kampuni yao ya Proin Promotions, waulize nini kimewakumba?!
Walianza kwa mbwembwe wakazindua filamu ya Foolish Age pale Mlimani City, kisha wakaja na mchakato wa kusaka vipaji nchi nzima, na baadaye wakamleta star wa movie wa Ghana, Van Vicker. Lakini sasa imebaki story.
Kuna kundi la Wahindi wameikamata hii biashara kwa kuwatia ujinga wasanii na watengeneza filamu, matokeo yake filamu imageuka kuwa biashara ya mtu mmoja tu, mwingine akiibuka atashambuliwa na wasanii wenyewe hadi afulie.
Biashara ya filamu ukiiangalia kwa juu juu unaweza kuiona kama ina mafanikio makubwa, lakini kwa uhalisia wake haina lolote. Mwambieni Idris akitaka asije kuchekwa kama Richard Bezuidenhout kwa kufilisika, basi akae chini na kufikiri upya cha kufanya lakini sio filamu.
Ova
Nitafuatilia hili la Team Lukaza kuchemka manake jamaa ana all necessary resources na alipoingia kwenye movie, nikajipa matumaini kwamba kidonda kimepata mkunaji kwa maana ya mtu mwenye mtaji wa kutosha! Hata hivyo, nilikuwa disappointed na Proin mara walipoanza coz' hawakuleta kitu kipya zaidi ya kuachana na mtindo wa Part I & I... mambo mengine, yakabaki business as usual.

Kuhusu mafanikio, you're right... hususani kwa waigizaji, hakuna cha maana wanachopata with exception of the few wale wenye majina! Other crew members, ndo hamna kitu kabisa... wengi wao ni vile tu heri ya nusu shari kuliko shari kamili! Wanaopata kidogo ni producers na hawa ni kwavile wanawanyonya other crew members hususani actors/actress ambao majority pay per scene yao ukiambiwa unaweza kuzimia!
 
Kweli kabisa mkuu, isitoshe hata hawa waigizaji wakubwa wa kike hulazimika kutoa ngono kwa Directors ili wawakumbuke kwenye casting. Ndio maana karibu kila movie Director hutumia chumba kimoja na star wa kike wa movie husika.
Kwenye filamu kuna hali mbaya sana, wengine hawataamini kama Kanumba alikufa huku akiwa hana hata filamu moja ambayo ni ya kwake kwa maana ya mali yake binafsi, kama ilivyo kwa JB, angalau Ray anayo moja.
Umasikini walionao waigizaji wa kike na aina ya maisha wanayotaka kuishi ndio inayowasukuma kuwa mama huruma, kuna waigizaji wa kike wanaouzwa kwa wanaume kwa laki mbili, na wengine hutoa ngono kwa kuazimwa magari ya kutembelea.
Hanspope aliingia kwenye filamu, labda kitu pekee alichoambulia ni kulala na Wolper, lakini hasara aliyoipata utashika kichwa nikikuambia, na ndio kama Lukaza pengine faida waliyopata ni kulala na Lulu, lakini wamepata hasara ya billions.
Biashara imevurugwa sana, na hata heshima ya waigizaji imeporomoka, waliobahatika kuona kambi zao za kushoot movies watakuwa mashahidi, yaani ni zaidi ya wanawake kujiuza.
Si ajabu Rais aliwakatalia ghafla kuwafturisha kama alivyowafturisha wanamuziki.
Ova
 
mpaka hapo nimeekewa jambo kumbe ni mgangaji mzuri labda anajua upana na urefu wa hiyo biashara
Lakini pia nimejua ni mkazi wa Arusha na nimeekewa maisha yake asilimia kubwa amekuwa Arusha.
Kama kuna la ziada tujuzane maana inaelekea kizungu anacho kiongea ni kama amekaa nje kidogo hebu anaejua anijuze

Nadhani unajua vizuri vijana wa arusha walivyo wazamiaji wa kuondoka nje na watalii. Halafu tofauti na watalii wengi wa kike kuondoka na vijana wa arusha pia arusha ina connection na Nairobi ambapo kiingereza in kawaida kwao. Pia fuatilia trend ya wawakilishi wengi wa big brother kutoka Tanzania wanatoka kaskazini arusha na moshi mfano richard, Julio, idris, Eliza Gupta, lotus na wengine.

Idris sio mkazi wa Arusha ni mzaliwa wa Arusha... ila wanaishi Dar na familia yake
 
Back
Top Bottom