IEBC Confirms 2027 Election Date – Uchaguzi Kufanyika Agosti 10

IEBC Confirms 2027 Election Date – Uchaguzi Kufanyika Agosti 10

OwadeKuya

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2026
Posts
535
Reaction score
312
The Independent Electoral and Boundaries Commission (IEBC) imetangaza rasmi kwamba uchaguzi mkuu utafanyika Jumanne, Agosti 10, 2027. Hii ilitangazwa na Commissioner Ann Nderitu, Mwenyekiti wa Kamati ya Operesheni za Uchaguzi, wakati wa uzinduzi wa Election Operations Plan (EOP) 2025–2027.

EOP inatoa mwongozo wa shughuli muhimu za uchaguzi na imejikita katika IEBC Strategic Plan 2024–2029. Mpango huu unalenga kuhakikisha utekelezaji wa shughuli za uchaguzi kwa wakati, kukuza uwazi na uwajibikaji, na kuimarisha ushirikiano na ushiriki wa wananchi.

Kwa wale wanaotaka kugombea, afisa wa umma lazima ajiuzulu kabla ya Februari 9, 2027. Vyama vya siasa vinapaswa kuwasilisha orodha za wanachama na tarehe za mchujo ifikapo Machi 16, 2027. Wagombea huru lazima wasiwe wanachama wa vyama vyovyote ifikapo Mei 9, 2027.

Kipindi rasmi cha kampeni kitaanza Mei 29, 2027, na kumalizika Agosti 7, 2027, saa 48 kabla ya siku ya uchaguzi.
Source : Thestar.co.ke
 
Back
Top Bottom