IET na ERB zinatuangusha wahandisi

IET na ERB zinatuangusha wahandisi

Hakuna wanachowasaidia

SEAP programe is a disaster

Wapo waajiri wengi hawaajiri tena wanachukua Trainee na ama hawawalipi na kuwafanyisha kazi wakitegemea walipwe na ERB kupitia SEAP programme au wanawalipa kidogo.

Kilichotakiwa ni taasisi hizi kushauri serikali kutunga kanuni zinazowezesha graduates kuajiriwa.

mfano kwa hapa tulipofika tunahitaji kuona vizazi tofauti vya kihandisi makazini, tunahitaji kuona shughuli za mtaani kwenye jamii zikiingizwa wataalamu.

serikali ikiwatengenezea fursa kupitia kanuni wataajirika na kuingia makazini na sio utaratibu wa sasa wa kuwapa uzoefu bila kutazama saturation ya fursa zilizokuwepo
Erb wanajitahidi sana ila wanaotuangusha ni serikali na wamiliki wa viwanda na makampuni mbalimbali, hamna sheria inayo wabana, muhimu kutunga sheria ambayo itawabana waajiri ambayo itakuwa lazima wachukue vijana kwa ajili ya kupata ujuzi , walipwe hata na serikali , kwa hivyo erb haitakiwi kulaumiwa serikali ndo inamatatizo.
 
Erb wanajitahidi sana ila wanaotuangusha ni serikali na wamiliki wa viwanda na makampuni mbalimbali, hamna sheria inayo wabana, muhimu kutunga sheria ambayo itawabana waajiri ambayo itakuwa lazima wachukue vijana kwa ajili ya kupata ujuzi , walipwe hata na serikali , kwa hivyo erb haitakiwi kulaumiwa serikali ndo inamatatizo.
lawama ziende kwa ERB

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wahandisi tutoke vipi? taasisi ambazo zingekuwa zinatusaidia tupige hatua zimesinzia kabisa.

Kazi yao ni kuandaa safari za kutalihi tu kwenye miradi.

Mimi nilitegemea labda tusikie taasisi hizi zikipendekeza namna gani jamii inaweza kuwatumia wataalamu

Mimi nilitegemea kusikia labda wakipendekeza kwa serikali itunge sheria za kuwa na vizazi tofauti makazini kwamba ni lazima kuwe na wazoefu na wanaotafuta ujuzi.

Vijana wanamaliza na kukaa mitaani na hakuna anayeweza kushauri cha kufanya kwa serikali.

Je, waache kufundisha vijana wapya au ubunifu wa namna ya kuwaingiza vizazi vipya?

Wenye dhamana ya kusimamia taaluma hizi wamesinzia FOFOFO
Erb wanchojua ni kukusanya hela zetu za usajili na membership fee ..
Hawana msaada wowote kwa graduate..
Inauma sana chama kipo kipo t
 
Kuna Shida sana kwenye kushauri mambo ya kihandisi, Angalia Tanroads wamejipa U-Mungu MTU na kuwa chanzo cha kuwa na design Mbovu za barabara zetu!! Wanafanya usanifu bila kushirikisha akili zao, Angalia usanifu was barabara ya Kimara to Kibaha, huu ni kati ya usanifu wa hovyo kuwahi kutokea duniani!! Unavunjia watu mita 243, unajenga barabara katikati kama uwanja wa mpira bila kuzingatia watumiaji wengine wa barabara!?!? Aibu!! Sasa wanaona aibu kutoa mapipa kwani ajali zitazidi!!! Wazo Tanroads waangaliwe kwa ukaribu sana!! Na kitengo chao cha TEKU wavujaji wakubwa wa kodi zetu
 
Back
Top Bottom