Unajua maana ya kukataa kumkubali Yesu Kristo kama Bwana na Mwokozi wako?
Maana yake wewe unakana huruma ya Mungu ya kuuokoa ulimwengu baada ya dhambi kuingia duniani
Ni sawa na wewe uamue kwenda kumlipia mwanao fedha alizokopa ili asipelekwe jela,lakini ili zile pesa zipokelewe kule unakoenda kuzilipa inatakiwa tu kauli ya mwanao kukubali wewe mzazi wake kumlipia na watazipokea na kumfutia mwanao mashitaka,yeye anakana na kudai kuwa hataki hilo
Unadhani nini kitatokea kama sio kuja kukamatwa na kipelekwa jela?
Hivi unaweza kuuliza "hivi unadhani kama mwanangu akikana kukubali mimi kumlipia fedha anazodaiwa ataenda jela kweli" wakati unajua kabisa majibu yake?
Ili umpate Yesu hutakiwi kulipa hela wala hataki chochote cha kidunia kutoka kwako bali yeye anataka kukuepusha la laana ya milele,alijitoa bila wewe kuomba bali ni kwa upendo wake tu ili wewe usiaibike milele,mkubali tu na utaona maisha yako yakibadilika kuanzia sasa na utazijua siri nyingi sana za Mungu ambazo kuna watu wanakesha JF kuzitafuta,na utazipata bila kulipia hata senti moja
Welcome to the Kingdom of God!