If our President has more than one wife: The question of human rights


Ndugu yangu penda usipende "HAKUNA USAWA KATI YA MWANAUME NA MWANAMKE" hii wanayosema ati haki sawa ni propaganda tu lakini ujue kutokana na Muumba alivyotuumba tofauti basi na haki zetu ni tofauti pia. muhimu ni kwa wanawake kudai haki zao zisidhulumie na wanaume lakini sio kutaka usawa ambao hautapatikana hadi kiyama kitasimama.
Hebu chukuwa mfano wa mwanaume mmoja akatembea na wanawake kumi na wote wakapata ujauzito. wakizaa watoto wote watamjua baba yao ni mmoja. sasa mwanamke akitembea na wanaume wawili tu akipata ujauzito haitakuwa rahisi kujua ni wa nani na kama mtoto akizaliwa bila ya kufanana na mmoja wao pia italeta utata kujua baba ni yupi hivyo kimaumbile tu haifai kwa mwanamke kuwa na wanaume wengi ila mwanaume anaweza bila shaka.
unajua binaadamu wa siku hizi tumezidisha sana kuharibu maadili tukijidai na utandawazi/kwenda na wakati na kutaka usawa. hebu angalia mfano hata kwa wanyama, utakuta kundi kubwa la wanyama wengi wakiwa majike na madume machache yakiwahudumia wote bila tatizo. haya ndio maumbile tusitafute usawa hapa tukaacha maumbile
 
Ni kweli wanawake sio sawa na wanaume. Wanaume wanaodhani wanawake ni sawa nao ndio wanaodhani men and women are interchangeable na matokeo yake wanaoa wanaume badala ya kuoa wanawake.

Wanawake wanapashwa kuwa na haki sawa na wanaume. Equal dignity.

Kuhusu uwiano, ukweli ni kwamba idadi ya wanawake katika nchi karibu zote inalingana, kwa karibu, na idadi ya wanaume. China ina wanaume wengi kuliko wanawake, na Botswana ina wanawake wengi kuliko wanaume.

Huu mlingano wa idadi ya wanawake na wanaume duniani ni ishara wazi, toka kwa Mwenyezi Mungu, kwamba ndoa iwe kati ya mwanamke mmoja na mwanamme mmoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…