wagombea hatki za wanawake. mbona mnaishia katikati? mbona hamsemi suala la watoto kuchukua jina la ukoo wa mwanaume ni uvunjaji wa haki za wanawake?
mbona hamsemi mume kuwa "automatic" mkuu wa nyumba ni uvunjaji wa haki za wanawake?
kwanini hampigi vita suala la kulipa mahali kama uvunjaji wa haki za wanawake?
yaani kweli watu wanaamini mtu akioa mke mmoja basi haki za wanawake zitakuwa zimelindwa! huko kwenye ndoa ya mke mmoja mbona nako pia haki zinavunjwa?
kama hamtazungumzia suala la haki za wanawake katika ujumla wake basi hili suala la kudai mke mmoja litakuwa la kinafiki na naamini wale wanaoona hii hoja ina harufu ya udini watakuwa sawa.
ni hayo tuu.
Maswali uliyouliza yanaweza kujibiwa hivi: kwanza, lazima uelewe kuvunja haki za binadamu ni kufanya nini na kumwonea mtu ni nini. Kuvunja haki za binadamu kuna maana zaidi ya vitendo viovu vinavyofanywa na vyombo vya dola au viongozi wa serikali dhidi ya raia. Mfano, polisi/askari/mgambo/viongozi wa serikali kuonea raia kwa kuwapiga, kudai rushwa, kutolipa mishahara ya wafanyakazi kwa wakti bila sababu muhimu nk - huo ndiyo uvunjaji wa haki za binadamu.
Halafu kuna uonevu kati ya mtu na mtu - kuanzia familia hadi maofisini. Huku kunaweza kuwa kuvunja sheria za nchi au kundi fulani la watu kuonea watu wengine.
Kuhusu mme kuwa kichwa cha familia: kwa 'experience' yangu mme au mke sio kichwa cha familia bali wote wawili (wazazi ndio kichwa cha familia). Ila kwa maelezo yako naweza kusema hivi: familia ninayotoka mimi, mama ndiye alikuwa "kichwa cha familia" kuliko baba. Kwa hiyo, control ya familia ilikuwa zaidi kwa mama kuliko baba.
Baadhi ya makabila, watoto ni mali ya mama na wajomba (kaka zake mama). Ndiyo wenye uamuzi wa mwisho. Mfano, mtoto wa kike akipata mchumba na anataka kuolewa, wanohusika zaidi ni hao niliowataja. Hii niliona hasa kwa Wachewa, Malawi.
Baadhi ya makabila huko Uganda, mtoto anaitwa majina matatu: Mfano, Robert-Mary Lubega. Jina la kwanza ni la mtoto; la pili la mama na la tatu la baba.
Kuvunja haki kati ya mtu na mtu ni pale mtu mmoja anapojiona ni bora zaidi au chochote anachokitaka yeye lazima kifanyike na siyo cha mwenzake.
Mimi nimeoa mke mmoja lakini msimamo wa mke wangu ni kwamba nikitaka kuoa mke mwingine au siku nitakayo mleta mke mwingine yeye atanipisha na kurudi kwao au atatafuta maisha yake mwenyewe.
Na mimi nakubaliana naye kwani sioni kwa nini nioe mke mwingine zaidi yake wakati mimi nimeridhika naye kwa yote na ndivyo nilivyoahidi wakati tukioana kuwa pamoja na kuvumiliana - wakati wa neema na mateso, raha na shida.
Wengine wanasingizia eti kuoa wake wengi ni kutimiza 'sexual urges'. Ni uongo mtupu! Kwani unadhani mwanamke anatimiziwa haja na mme mmoja tu? Mara nyingi kinachotokea kwenye ndoa ni kuwa na 'control' na hizo 'sexual urges'. Kwani nani hana? Siyo rahisi mtu kumtoshereza mwenzake hata kama mmoja ana nguvu kiasi gani kwani kumtoshereza mwingine hakuko tu kwa yule mwenye nguvu zaidi bali pia yule mwingine anajisikiaje 'under the circumstances'.
Mfano, mke anaweza kuwa anapenda safari nne lakini mme anaweza moja tu au mme anapenda zaidi na mke anasema basi/amechoka. Si lazima kutafuta tu namna ya kuvumiliana kwa hili? Lakini kumwoa mwingine ni kuongeza matatizo tu. Kwani baada ya kutoka kwa mke fulani, mwingine naye anaweza kusema anapenda. Sasa itakuwaje?
Mimi nadhani maana halisi ya ndoa ni 'complementarity/companionship'. Na kitu kinachounganisha ni upendo. Kwani kama kuna upendo kila kitu kitakuwa na maana. Lakini kama upendo haupo, kutabaki kutumiana tu na siku mmojawapo atakapoonyesha kudhoofika kingono basi ndio mwisho wa kuwa pamoja. Lakini kwa wale wanaopendana hata muda huo ukifika bado wanakuwa pamoja tu kama mke na mme.
Nakumbuka baadhi ya wazee waliooana wanaishi kila mmoja kitanda chake kwa vile 'sex' haina maana tena katika maisha yao lakini wanakuwa wakipendana na kila kitu wanafanya pamoja mpaka Mungu alipowachukua. Wasingekuwa na upendo si wangekuwa wameshaachana zamani?
Kuhusu mahari: baadhi ya makabila hapa Tanzania hawatoi mahari. Huwa nasikia Wachaga ni kabila moja wapo. Huko Malawi, Wachewa hawana cha mahari ila kuna zawadi fulani zinazopelekwa kwa mtemi (mfumu) mtu akitaka kuoa kwenye kijiji chake.
Last edited: