Mkuu
elvischirwa , kwanza mimi sio nabii, nabìi ni mtu wa Mungu anayemtumia kufikisha ujumbe kwa watu wake. Mimi sio nabii bali ni just a trends reader ambaye anasikiliza the voices from within, bila kuwa na uhakika and for sure ni sauti za nani, maana sijawahi kuambiwa "Mimi ni Mungu" lakini manabii wanapotokewa huambiwa "mimi ni Mungu" na kuelekezwa nenda ukawaambie watu wangu hiki na hiki na hiki, lakini sauti ninazozileta mimi ni sauti tuu ninazozisikia ndani yangu bila kuelezwa ni sauti za nani.
Sio kila sauti mtu anayoisikia kutoka ndani yake ni sauti ya Mungu!, sauti nyingine ni sauti za shetani!.
Hata ndoto, sio kila ndoto mtu anayoota anaonyeshwa maono fulani ni ndoto ya Mungu, ndoto nyingine ni ndoto za shetani!
Vivyo hivyo sio kila kifo ni kifo cha Mungu, au kazi ya Mungu, vifo vingine ni kazi ya mwovu ya shetani!.
mimi ninashindwa kuelewa kufuru ya chuki yako dhidi ya Chadema inatoka wapi! Wewe umekuwa ni mtu wa hovyo kwani nyuzi zako huwa za kuwashutumu Chadema kwa kuwaona ni magarasa na wewe ndiye mwenye akili na busara!
Kiukweli kabisa toka ndani ya nafsi yangu, mimi siichukii Chadema!. Japo mimi ni mwana CCM, it's expected nitakuwa ninaichukia Chadema hivyo nataka Chadema ife!.
Kuna wana CCM wa aina mbili, wana CCM die hard na wana CCM Contemporary.
CCM die hard ni wale wanaopenda kuona CCM lazima ishinde kwa mbinu zozote, ziwe hooks and crooks hata ikibidi to crush the opposition, just crush it, na kama ni kushinda kwa bao la mkono piga bao!. JPM was a CCM die hard!.
Sisi CCM contemporary tunapenda CCM ishinde kwa haki, hivyo kuna wana CCM Wazalendo wapenda haki hawapendi figisu zozote za uchaguzi zinazokiuka haki. Wana CCM wa type yangu wanawapenda the opposition.
Baada ya kumjua JPM ni CCM die hard, ili kuhakikisha CCM inatenda haki kuwatendea Watanzania wote, angalia mwana CCM mimi nilishauri nini kwa chama changu CCM. Kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa niliisikia sauti kuniambia kitu kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi Mkuu wa 2020, hivyo nilichokifanya ni kutimiza wajibu wangu kwa kuwaeleza wahusika
Ombi Maalum, Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa 2020, Uendeshwe kwa Ceteris Peribus, Sio Kwa Mutatis Mutandis. Tutabarikiwa! kwenye bandiko hilo nikaeleza nimeisikia sauti tufanye nini na tusipofanya nini kitatokea!.
Na kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa, baada ya kuona figisu zimeanza, nilitoa angalizo hili
Ushindi mtamu ni ushindani katika uwanja sawa, sio ule wa mezani. Magufuli, kasi yako ni ushindi wa kishindo. Ruhusu ushindani wa haki, sawa na wazi
Sasa ukiyasoma mabandiko hayo mawili ambayo yametolewa na mwana CCM kwa chama chake, kama unaamini mtu huyu anaichukia Chadema, endelea kuamini hivyo!.
Amini usiamini kuna wana CCM Wazalendo na wapenda haki wanaopenda kuona wapinzani wanaingia Bungeni. Mimi ni mmoja wao, hivyo nimetumia nguvu zangu nyingi sana za ushawishi na ushauri kuisaidia Chadema and the opposition to do the right thing!. Wengi wetu humu huishia kuandika tuu humu, lakini mimi kwenye hili nimekwenda physically Chadema pale Mtaa wa Ufipa, NCCR Mageuzi pale Ilala Boma na CUF Buguruni na kuonana na the office bearers kuwafunda how to do the right thing kwa mazingira ya siasa zake za ushindani na chama dola.
Angalia ushauri huu ni wa lini
Elections 2015 - Kuelekea 2015: CHADEMA, Don't Miss the Target, Adui Mkubwa sio CCM Bali ni ... sasa ushauri kama huu ni wa mtu anayeichukia Chadema?.
Sasa chama kinachoshauriwa the right thing to do, kinapoendelea kufanya madudu, lazima mtu ukasirike!.
Uchaguzi 2020 - Je, Tanzania tuna upinzani makini, upinzani wa kweli wa kuing'oa CCM madarakani au bado sana? Nilichoshuhudia leo uzinduzi CHADEMA, kiukweli...
Nimefika mahali naona unaamini wao wamezaliwa na wazazi wa hovyo ndiyo maana wako hovyo na wanaccm wamezaliwa na wazazi waliotukuka ndiyo sababu wanabusara na akili! Wewe kwa kujiona kwako unaakili na busara kuliko wanachadema wote kunanifanya nikuone haufai hata kuwa wakili kama Lakha.
Wewe wasema!.
Mzee Mandela na wenzake waliteswa na kuumizwa kuliko unavyofikiria, lakini walifika mahali wakasema yaliyotokea yalitokea hebu tuoongee na wstesi wetu tuone kama watakuwa tayari kuishi nasi kama binaadamu wenzao, wakaongea wakaaminiana yakaisha! Nyie majuha wa siasa hapa husema walilamba asali! Mmezoea mizozano isiyo na mwisho na mnaipenda hivyo.
Wewe wasema!.
Nakushauri Paskali shuka chini waone wanachadema ni watu(chadema ni chama)tu kama wewe na wapo waliokuzidi akili na busara na si mazezeta kama unavyoamini wa kupokea ushauri wote toka kwako,
Nimepokea ushauri.
unapomkosoa mwenzako kwa kila jambo alifanyalo hata utafunaji wake wa dona, basi wewe utakuwa na kasoro kubwa.
Hili pia nimelipokea na kujifanyia tathmini, inawezekana mimi ndio mwenye matatizo na sio Chadema.
Ila pia sii kweli kuwa naikosoa Chadema kwa kila kitu, Chadema na viongozi wake wakifanya vizuri huwa nawapongeza na hizi ni baadhi ya pongezi zangu kwa Chadema
- Pongezi Nancy Mwenyekiti CHADEMA California
- Kwa Hili! Hongera Sana Chadema, Hongera Mhe. Mbowe!, Sasa Muwege Mnasikilizaga Ushauri!
- Hongera ITV kumhoji Tundu Lissu. Hongera sana Tundu Lissu kuzungumza kistaarabu kwa lugha za staha. Ruksa kuhisi chochote, sio fair kutaja majina!
- Tundu Lissu kama JPM, ni mtu mkweli. Asema ukweli jinsi ukomo wa uongozi ulivyoyeyuka CHADEMA
- Uchaguzi 2020 - Clouds 360, leo imemtendea haki Tunda Lissu, imeitendea haki Chadema, imewatendea haki Watanzania, hongera sana, mbarikiwe sana!
- Mhe. Tundu Lissu, Please Acha Kumsulubu Spika Wetu! Unammaliza Kabisa Hadi Ameshindwa Kazi!
- Mwana CCM anayemuuliza Mwenyekiti wake swali kama hili Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli ili kuwatetea wapinzani, mtu kama huyu anaweza kweli kuwa na chuki na upinzani?.
- Au mwana CCM anayekiambia chama kitu kama hiki CCM sio tu ni chama tawala, bali pia ni chama Dola! anaweza kuwa anauchukia upinzani?.
Mapenzi ya kweli hukaa ndani ya moyo wa mtu, na chuki vivyo hivyo. Maadam mimi najijua ndani yangu naionaje Chadema, wanaonoana kuwa ninaichukia Chadema kwa kuieleza ukweli mchungu kuhusu udhaifu wao, be it!.
P