Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Upinzani nchi hii umekomaa na kuota mizizi kiasi kwamba ni vigumu kufuta upinzani hapa nchini na ndio maana Mwendazake alifeli vibaya katika adhma yake ya kutaka kuua upinzani(kafa yeye kaacha upinzani ukiwa imara kuliko jana).
Kwasababu CCM hawako tayari na pia hawawezi kushindana na upinzani (CHADEMA) katika uchaguzi ulio huru na wa haki, option pekee waliyobaki nayo ni kuwashirikisha wapinzani (hasa CHADEMA) katika kuunda serikali huko mbeleni .
Kinachoitwa maridhiano leo hii kesho kinaweza kuwa ni mwanzo wa kufikia makubaliaona ya kuwa na serikali ya mseto kupitia katiba mpya au mabadiliko madogo ya katiba tuliyonayo leo hii.
CCM kukaa na wapinzani sio kama wanapenda, bali wanatambua nguvu waliyonayo wapinzani na hapo ndipo ule msemo wa "if you can't beat them, join them" unapopata nafasi.
Hata kama kutakuwa au kuna shinikizo la Wahisani, shinikizo hilo ni matokeo ya nguvu waliyonayo wapinzani na si vinginevyo kwani huwezi weka shinikizo kama hilo pasipo kuwa na upinzani wenye nguvu.
All in all, pamoja na kutoaminiani kuliopa saaa katika mazungumzo yanayoendelea baina ya CHADEMA, CCM na serikali, naiona serikali ya mseto ikizaliwa huko mbeleni huku Mbowe na Mama Samia wakiingia katika historia ya Taifa letu.
Muda utahibitisha.