If you can't beat them, join them: Naziona dalili za CCM kuja na wazo la Serikali ya mseto huko mbeleni

Penye udhia na njaa penyeza rupia, halafu koroga
 
CCM hii hii iliyokua inaingiza kura zilizopigwa tayari kwenye vikapu,bahasha na mabegi.?

You must be joking dude.!
 
Nakushangaa unapokiri CCM ni chama bora kabisa lakini unaunga mkono maridhiano, haya maridhiano unayofurahia ni ya nini kama CCM ni chama bora?

Ok, unataka ili wafunge magoli magoli safi, kumbe mpaka sasa unajua huwa wanafurahia ushindi wa magoli ya offside!, basi tukubaliane CCM hawana ubora wowote, umeandika uongo.
 
Naunga mkono maono haya. SSM wamepoteza siasa za ushawishi wamebaki kuangalia msaada wa vyombo vya dola tu. Wakati ukianangalia vizuri hawa chadema harakati zao zinaendelea nchi nzima pamoja na magumu wanayopitia. Pia malalamiko hapa nchini kwasasa ni mengi sana kiasi kwamba ni rahisi kwa mtu kujoin kwenye hizi movement za wapinzani kwa uwazi au kwa siri kutokana na madhira na maonezi wanayopitia. Na wakati mwingine kumekuwa na matukio makubwa yanayo onyesha kukanyagwa kwa katiba waziwazi pia utekelezaji wa sheria za nchi kwa double standard. Hivyo Chadema ndiyo wamejipambanua kwa wananchi kuwa ndiyo wapigania haki za watz waliyobaki kwa sasa , na ndiyo sababu ya kupata support kubwa na ccm kuonekana wana siasa wepesi.
 
Ni mawazo yako tu ya kimbowe mbowe ya kilaghai. Mkiambiwa siasa hamziwezi mnaanza kulialia.
 
Umeilewa hoja ya mleta mada?

Hakuna chama bora wala kisicho bora. Vyama vyote ni sawa na ni bora ktk mizani yao. Wewe unaiona CCM ni bora. Mwingine anaiona CHADEMA ni bora. Na mwingine NCCR M na mwingine ACT W...

Sasa rudi kwenye hoja ya mleta mada..

Kwamba ipo possibility ya kuwa na "serikali ya mseto" huko kwa sababu alizozitaja. Wewe unaonaje..?

Mimi nakubaliana naye. Zanzibar ilikuwa hivi hivi. Na suluhu kwa kiasi chake ikawa ni serikali shirikishi mseto kwa kufanya marekebisho madogo ya katiba yao. Mambo kiasi chake yakatulia japo uharibifu kidogo ukatokea mwaka 2015..

Narudia tena kukuuliza maoni yako. Wewe unaonaje?
 
Hawezi kukupa majibu au mtazamo wake. Hata hoja ya mleta mada anaweza kuwa hajaielewa. Wapo wa aina yake wamejaa huko bungeni hawawezi kujenga hoja, walipelekwa tu kwa wizi wa kura uliofanywa na mwendazake. Hawa wote hawawezi kuelewa kuhusu maridhiano au hawataki hata kufikiri habari ya serikali ya mseto hapo baadaye.

Cc Azizi Mussa
 
Aah mimi hata sijui ndugu..! Kumbe huyu Azizi Mussa ni mbunge wa CCM..!!??

Looh, ila mjanja kweli. Anauma na kupuliza. JAmbo moja zuri kwake ni moja tu , hutumia lugha ya ustaarabu ktk mijadala inayoficha unafiki na ukada wake...

NB:
Nje ya mada. Ni dakika ya 45+, Manchester City FC ameshapigwa goli moja na Aston Villa FC . Taji la ubingwa wa EPL linataka kumponyoka mdomoni. Mpinzani wake Liverpool FC na Wolverhampton FC mpaka sasa ni 1 kwa 1...!!

Ndugu Azizi Mussa, life is very unpredictable..
 

CCM sio chama bora, bali ipo ilipo kwa sababu za kihistoria. Na sasa imedhihirika pasi na shaka kuwa CCM haiwezi tena kushindana bila mbeleko ya vyombo vya dola, na ushahidi uko wazi. Kimsingi CCM sio chama cha kizazi hiki, ndio maana kanatumia dola kubaki madarakani kwa shuruti. Leo hii ukiweka ushindani sawa wa kisiasa, CCM italala kaburi moja na ilipolala KANU ya Kenya.
 
CCM wengi hawana akili kama mashabiki wa yanga
 
Hakuua ila aliukomaza upinzani uko ndani ya mioyo. Ni kama mapenzi.

Alitumia police, usalama, mahakama, magereza na Jeshi kudidimiza upinzani.

Baada ya kufa angalia shangwe iliyopo kuanzia mtaani mpaka maofisini.

90% ya watanzania walifurahia kifo chake na ndo upinzani wenyewe sasa.
 
"ccm hawashindi kwa sababu ya sera,no, ila kwa sababu ya kuiba uchaguzi".
Hapo ndipo mnapofeli kuamini kuwa ccm inashinda sababu ya wizi wa kura,upinzani mnabweteka sana, badala ya kupambania maslahi ya wananchi mnapambania maslahi ya chama,. Uku mkiacha wananchi wajipiganie wao wenyewe.
 
Mmm upo serious au umeamua tu na wewe uongee?
 
Kwa kiburi walichonacho viongozi wa CCM na hasa ukizingatia wanacomand dola (polisi na usalama wa Taifa) kamwe haiji kutokea labda tukipata katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi!

Kwa kiburi hicho hicho, viongozi wa CCM watakubaliana tu na katiba mpya na tume huru ya uchaguzi zinazowahakikishia kubaki na madaraka makubwa ya Rais - watered down versions.

Wapinzani hasa CHADEMA wajiandae kwa hiyo vita kubwa ya katiba. Wakilegea tu, status quo inarejeshwa kijuaji huku wakipongezwa kwa “ushirikiano wao wa kipekee” kwa maslahi ya taifa.
 
Kama ungeniuliza Mimi ningejibu kwamba kama serikali ya mseto au ya umoja wa kitaifa imewezekana sehemu moja ya muungano basi hata sehemu ya pili ya muungano inawezekana pia !! Ila Mimi naomba kufahamishwa je serikali za namna hiyo huwa ni kwa faida ya wananchi wote au kwa viongozi tu ?? AULIZAYE ATAKA KUJUA !!
 

Upinzani ungekufa kabisa, sawa. Usiishie kuwa naïve, endelea ujiulize, CCM ingekuwa na hali gani? Watanzania wangekuwa vipi? Taifa lisilo na upinzani hakika haliko hai. Ni kama kufikiri mwili wa binadamu unaweza kuwa hai bila kuwa na bacteria hata mmoja!

Wote tulijionea mwondoko wa JPM. Ni kujiidanganya kufikiri kuna ambaye angebaki salama na kuishia kula kuku nchini baada ya upinzani kuuawa na Magufuli kibabe.

Have no illusions about the mindset of tyrants. Hawana rafiki wala teamwork. Wana relatives, sycophants na stooges, basi. Nina hakika in the near future kilio na kusaga meno kingewafikia watanzania wengi sana. Pengine ingesaidia kurejesha akili za wengi kuelewa madhara ya kuendekeza ubazazi kwenye utawala wa nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…