Ifahamu bangi na madhara yake

Ifahamu bangi na madhara yake

Wakili

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2017
Posts
531
Reaction score
657
Habari wapendwa,

Napenda leo tuzungumzie hili zao aina ya bangi ambalo kwa kiasi kikubwa limekuwa likioteshwa kwa siri maporini huko.

Bangi inakemikali hatari mno inayofahamika kwa jina la THC ambayo unapoitumia kwa wale wavutaji basi huleta hallucinations, ambayo ni hali ya kusikia na kuona sauti na vitu ambavyo in real world havina uhalisia.

Bangi pia husababisha kumbukumbu kupotea, kansa ya mapafu na viuongo kukakamaa. Kwa mataifa makubwa kama Marekani katika jimbo la California wameruhusu matumizi ya mmea huu hatari, lakini athari zake zimekua ni siri ya watumiaji, huku drug lords wakiogopwa kutajwa kwa watu kuhofia kuuawa.

Bangi ni hatari na mimi kama mtumiaji niliyeacha imeniacha na athari chache na zingine nakabiliana nazo kwa dawa maalumu kama Haloperidol na Carbamazipine.

Bangi ni hatari mno, inatia huruma kuona jinsi wasanii wa Bongo Fleva wanavyoisapoti katika video zao na wengine kudiriki kuisifia kabisa kitu ambacho ni kosa kubwa mno.

Serikali na jeshi la polisi viingilie kati suala hili ili kukilinda kizazi hichi cha watoto wasio na uelewa wowote juu ya bangi na madhara yake.

Asanteni nakaribisha maswali.

images.jpeg
 
Bangi ni mbaya mno mimi nimetumia toka mwaka 2018 nikianza kwa kuvuta bila rizla nilikua nakula stick nzima,mpaka hatua ya kunyonga mwenyewe kwenye rizla.Bangi nimbaya mno nakushangaa wewe ndugu yangu unaisifia ulishawahi itumia ukaona madhara yake?
Wewe ulipata madhara gani?
Leta scientific evidence acha taarabu za bure.
 
Kama kichwa chako hakijavutishwa bangi ni kama kimevutishwa, kikivutishwa ndio hivyo hautaacha kuona vitu visivyokuwa na uhalisia..achana nayo. Inazo faida nyingi kuliko hasara kama ikitumika vizuri!
Bangi haiangalii kichwa,ni ubongo unaoathirika,bangi ni hatari mno,kumbuka mwili wa binadamu especially mapafu ni a very delicate organ isiyotaka inhaling of smokes,sasa wewe unajigamba hapa tuambie yale ya sirini kuhusu bangi.
 
Nyie mnakoelekea mtatuambia kufanya ibada ni dhambi...

Ganja ni ibada,kuvuta bangi ni sawa na kufanya ibada,ndio maana bangi huwa inataka utulivu..
Mjinga mkubwa wewe tangu lini bangi ikawa chanzo cha kufanyia ibada, yaani hizo dini zenu za mtaani(rastafarians) ndio unaitumia kama hoja?Punguani mkubwa wewe lete fact sio ujinga wa dini za wahuni kama kina Bob Marley za uvutaji wa sumu mwilini.
 
Rubbish gani wewe sema ni mteja wa bangi na bado unavuta kwa siri kinyume na hapo utakua keyboard warrior unayetafuta umaarufu humu.
Umeanzisha thd ya jambo ambalo huna elimu nalo,hujaandika chochote cha maana zaidi ya bla bla tu,
Mbona hujaongelea Sigara? Vipi kuhusu vilevi vinavyounguza maini?

Nimekwambia weka hapa Scientific evidence,hapa ni JF sio Tik tok.
 
Bangi ni mbaya mno mimi nimetumia toka mwaka 2018 nikianza kwa kuvuta bila rizla nilikua nakula stick nzima,mpaka hatua ya kunyonga mwenyewe kwenye rizla.Bangi nimbaya mno nakushangaa wewe ndugu yangu unaisifia ulishawahi itumia ukaona madhara yake?
Umeanza kuvuta bangi 2018?? Kojoa ukalale bangi sio kwa kila mtu
 
Kama kwenye familia yako mna historia ya magonjwa ya akili,
Achana na Bangi kabisaaaaa utawehuka
Sio familia tu, bangi ina athiri ubongo kitu ambacho ni organ muhimu kuratibu matendo yote ya mwili. Sasa wewe unajaza uchafu kwenye ubongo unategemea usiwe kichaa? Lazima utapata kichaa na zaidi ya kichaa.
 
Habari wapendwa,

Napenda leo tuzungumzie hili zao aina ya bangi ambalo kwa kiasi kikubwa limekuwa likioteshwa kwa siri maporini huko.

Bangi inakemikali hatari mno inayofahamika kwa jina la THC ambayo unapoitumia kwa wale wavutaji basi huleta hallucinations, ambayo ni hali ya kusikia na kuona sauti na vitu ambavyo in real world havina uhalisia.

Bangi pia husababisha kumbukumbu kupotea, kansa ya mapafu na viuongo kukakamaa. Kwa mataifa makubwa kama Marekani katika jimbo la California wameruhusu matumizi ya mmea huu hatari, lakini athari zake zimekua ni siri ya watumiaji, huku drug lords wakiogopwa kutajwa kwa watu kuhofia kuuawa.

Bangi ni hatari na mimi kama mtumiaji niliyeacha imeniacha na athari chache na zingine nakabiliana nazo kwa dawa maalumu kama Haloperidol na Carbamazipine.

Bangi ni hatari mno, inatia huruma kuona jinsi wasanii wa Bongo Fleva wanavyoisapoti katika video zao na wengine kudiriki kuisifia kabisa kitu ambacho ni kosa kubwa mno.

Serikali na jeshi la polisi viingilie kati suala hili ili kukilinda kizazi hichi cha watoto wasio na uelewa wowote juu ya bangi na madhara yake.

Asanteni nakaribisha maswali.

Sukari ni hatari kuliko Bangi.
 
Back
Top Bottom