Naomba nijibu kadri mungu atakavyonijalia......mtaji ukitoa meza,jiko, karai, sahani ,vikombe , na vifaa vingine,basi mtaji ni mdogo tu, pweza wanauzwa kwa kilo ,kilo moja haizid buku kumi,inategemea na siku hiyo, so inategemea na kilo unayoitaka, kachori mtaji wake hauzid 10000, hapo toa mafuta na mkaa.
Kuhusu pilipili,kule kule zinauzwa uliza pilipili ya pweza,kuna babu anauza hiyo pilipili,na ndio maana unakuta maeneo mengi pilipili zinafanana kwa utamu. location nzuri has a ni sokoni au stend ya basi au kwenye mkusanyiko wa watu wengi. kuhusu mchuzi,unaponunua pweza kule feri,vuka upande wa pili wakati unatoka nje,utaona kunasehemu wanachemsha na kukaanga hao pweza,so wanachemsha kwanza kisha unapata mchuzi unaweka kwenye kidumu chako,kisha unamkaanga kwa gharama ndogo tu........pia kuna wengine wanaweka na samaki hapo hapo kwenye meza so integemea na maamuzi yako........
NB sijawahi kufanya hii baishara ila nilitaka kufanya ,hivyo nikafanya research kwanza kujua ABC zake.,......... ila kwa wenyewe wanasema inafaidaa, so Mimi hii biashara niaifahamu kwenye makaratasi,so ukichukua ushauli wangu,usije kunihumu huko baadaye..........tuendelee kuombea ndege yetu waiyachieeeee.