Online Pastor
JF-Expert Member
- Sep 7, 2017
- 1,948
- 1,523
Hii ni moja kati dini changa zaidi Duniani kwa sasa.
Dini ilianza karne ya 19 huko Iran ikiwa imechupikia toka dhehebu la Shia.
Waanzilishi wa dini hii ni Bab na Bahaullah!
Dini hii inaamini katika umoja wa dini zote za duniani na inayowatambua waanzilishi wote wa dini kuwa ni wamoja.
Ungana na mimi katika somo hili.
Baadhi ya Wadhihirishaji/manabii ambao wameshakuja duniani ni:Adamu,Abraham,Isaya,Zoroaster,Krishna,Buddha,Yesu Kristo,Muhammad na sasa Bahaullah.
IMANI ZA KIBAHAI
1)Wanaamini dini na Sayansi ni kitu kimoja na hivyo ni vizuri tukaitumia kutatua changamoto za dunia.
2)Wanaamini katika uvumilivu wa dini zingine kwani zote lengo lao ni kumkomboa mtu
3)Wanaamini kuwa Mungu ni mmoja ila ana majina tofauti kulingana na Jiographia na tamaduni za watu
4)Wanaamini ufufuo wa kiimani ni endelevu hivyo baada ya miaka 857 toka leo kuna nabii mwingine ataletwa na Mungu ili kuleta ufunuo utakaoendana na wakati huo.
5)Wanaamini katika usawa wa kijinsia,kitaifa na kihali
More to come!