Ifahamu Kiundani Dini ya Kibahai

Ifahamu Kiundani Dini ya Kibahai

Online Pastor

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2017
Posts
1,948
Reaction score
1,523

Hii ni moja kati dini changa zaidi Duniani kwa sasa.

Dini ilianza karne ya 19 huko Iran ikiwa imechupikia toka dhehebu la Shia.

Waanzilishi wa dini hii ni Bab na Bahaullah!

Dini hii inaamini katika umoja wa dini zote za duniani na inayowatambua waanzilishi wote wa dini kuwa ni wamoja.

Ungana na mimi katika somo hili.

Baadhi ya Wadhihirishaji/manabii ambao wameshakuja duniani ni:Adamu,Abraham,Isaya,Zoroaster,Krishna,Buddha,Yesu Kristo,Muhammad na sasa Bahaullah.

IMANI ZA KIBAHAI
1)Wanaamini dini na Sayansi ni kitu kimoja na hivyo ni vizuri tukaitumia kutatua changamoto za dunia.

2)Wanaamini katika uvumilivu wa dini zingine kwani zote lengo lao ni kumkomboa mtu

3)Wanaamini kuwa Mungu ni mmoja ila ana majina tofauti kulingana na Jiographia na tamaduni za watu

4)Wanaamini ufufuo wa kiimani ni endelevu hivyo baada ya miaka 857 toka leo kuna nabii mwingine ataletwa na Mungu ili kuleta ufunuo utakaoendana na wakati huo.

5)Wanaamini katika usawa wa kijinsia,kitaifa na kihali

More to come!
 
Nembo ya dini ya Kibahai.
Duniani kuna wabahai wapatao millioni 7 na nchi inayongoza kuwa na wabahai wengi ni India,huku Afrika Kenya ikiwa namba moja na Tanzania ikiwa na wabahai laki moja na kitu tu!
YVL3TD9xq7B4FjD25hHlGJdqbqZcKzIZTKegGnV4q_l5yR5qhwReV2j29JZTpP6DuBE=w300.png
 
Hii ni moja ya dini changa iliyoanzishwa karne ya 19.

Ilianzia Mashariki ya Kati katika nchi ya Iran.
Waanzilishi wa dini hii ni Bab na Bahaullah.

Makao makuu ya dini hii ni Haifa nchini Israeli.

Wabahai wapo takribani millioni 7 duniani,huku nchi ya India ikiwa namba moja kwa wingi wa Wabahai wanaofikia milioni 1.
Kenya ni namba moja kwa Afrika ikiwa na waumini 522,000+ huku Tanzania ikiwa na waumini 109,000+!

Wabahai wanaamini dini zote ni sawa na waanzilishi wote wa dini zilizo duniani kuwa wanamwakilisha Mungu
Wanaani kuwa kila baada ya miaka 1000 Mungu hutuma mdhihirishaji/nabii ambaye huja duniani kuleta ujumbe wa Mungu kuwafundisha watu.

Wadhihirishaji hao ni Adamu,Abrahamu,Isaya,Buddha,Krishina,Zoroaster,Yesu Kristo,Muhammad,na sasa Bahaullah!

Hivyo baada ya miaka 1000 atatokea nabii wa kuchukua nafasi ya Bahaullah!

IMANI YA WABAHAI:

1)Wanaamini uwepo wa Mungu mmoja,
2)Wanaamini Mungu hawezi kujulikana kirahisi na kila binadamu,hivyo kila baada ya miaka 1000 hutuma mdhihirishaji au nabii kuja kuufundisha ulimwengu
3)Wanaamini dini zote ni sawa kwenu yale mambo inazofundisha yanatoka kwa Mungu
4)Wanaamini katika usawa kijinsia,kitaifa na kidini
5)Wanaamini katika utafutaji wa ukweli pasipo kufungwa na imani za uchawi au mila za jamii ulimo.
Somo linaendelea...
 
Wanatumia kitabu gani ktk madundisho yao ?
Huyo Mtume wao Bahaullah bado anaishi?
anaishi wapi ?

Mungu wao anaitwa nani ?
 
Jindal Singh sorry nilipitiwa na usingizi,ni hivi,hawaruhusiwi kujihusisha na maswala yote ya kisiasa au kiutawala,na hasa siasa zenye vyama vinavyopingana kama ilivyo CHADEMA na CCM hapa nyumbani.

Na hata kama wakiamua kujiingiza kwenye siasa,mara inakuwa pale wanapo kuwa wakipambana kujiokoa na unyanyasaji wa kidini.

Mathalani,wabahai wamekuwa wakiteswa katika nchi kadhaa duniani,hasa Iran,
Kama utakuwa haujatosheka niambie ili tuone cha kufanya!
 
Wanatumia kitabu gani kufundishia?biblia au Koran?ni swali umeulizwa hapo juu
 
Jindal Singh sorry nilipitiwa na usingizi,ni hivi,hawaruhusiwi kujihusisha na maswala yote ya kisiasa au kiutawala,na hasa siasa zenye vyama vinavyopingana kama ilivyo CHADEMA na CCM hapa nyumbani.

Na hata kama wakiamua kujiingiza kwenye siasa,mara inakuwa pale wanapo kuwa wakipambana kujiokoa na unyanyasaji wa kidini.

Mathalani,wabahai wamekuwa wakiteswa katika nchi kadhaa duniani,hasa Iran,
Kama utakuwa haujatosheka niambie ili tuone cha kufanya!
Nimeuliza Pastor,
Wanatumia kitabu gani ktk mafundisho yao?
Na umesema wanamini kila baada ya miaka 100, Mungu anamleta Nabii,
Je Nabii wao Bahaulla yupo hai ?
Naomba nijibu tafadhali.
 
Che mittoga vipo vitabu vingi,ila cha muhimu zaidi kinaitwa Kitab-i-Aqdas ambacho kiliandikwa na Bahaullah mwenyewe.

Lakini pia wabahai kwa kuwa wanaamini dini zote ni kama mti wenye shina moja ila matawi mbalimbali,husoma vitabu vya dini zote duniani.
Halafu ni kila baada ya miaka 1000 na siyo 100.

Biblia,Quran,vitabu vya Buddha,Wahindu vyote wanasoma!

Wabahai wanamwabudu Mungu mmoja,na wanasema kuwa ana majina mengi kulingana na mila na tamaduni za eneo.
Mfano Wayuhudi humwita Yahweah,Marastafari humwita Jah,Wakristo humwita Yehova/Yahweh,Waislamu humwita Allah,Wahindu humwita Krishna.

Hivyo ndivyo walivyo.
 
Back
Top Bottom