Ifahamu kwa undani Bawasiri na namna ya kujiepusha nayo

Ifahamu kwa undani Bawasiri na namna ya kujiepusha nayo

Joined
May 18, 2026
Posts
24
Reaction score
9
BAWASIRI NI NINI?
Bawasiri ni ugonjwa unaotokana na kuvimba au kupasuka kwa mishipa ya damu sehemu ya haja kubwa na kupelekea kuota kwa kinyama au uvimbe ambao ndio huitwa bawasiri.

Sababu kubwa ya mtu kupata bawasiri ni mgandamizo sehemu ya haja kubwa, ambapo mgandamizo huo hupelekea kupasuka au kuvimba kwa mishipa midogo ya damu aina ya veins sehemu ya haja kubwa, hivyo kupelekea kuota kwa kinyama, miwasho, maumivu makali na kutoa damu.

Ugonjwa huu umekuwa hatari kutokana na tabia ya wagonjwa kuficha tatizo kwa sababu ya aibu ya eneo lilipo au kuhofia jamii kuwatazama tofauti, kwani jamii nyingi hasa za Afrika Mashariki huamini kuwa ugonjwa huu ni mkosi mkubwa.

DALILI ZA MTU MWENYE BAWASIRI
  1. Kupata muwasho mkali katika eneo la juu la haja kubwa
  2. Kujitokeza kwa kinyama au vinyama eneo la haja kubwa
  3. Kutokea kwa uvimbe katika tundu la haja kubwa
  4. Kupata kinyesi chenye damu
  5. Kupata maumivu makali wakati wa kujisaidia
  6. Kupata maumivu ya tumbo au kiuno hasa bawasiri inapofikia hatua mbaya
AINA ZA BAWASIRI
Kuna aina 2 za bawasiri kama ifuatavyo:
  1. BAWASIRI YA NJE
    Ni kuota kwa kinyama sehemu ya nje ya haja kubwa ambapo kinyama huwa nje hata kama hujaenda kujisaidia haja kubwa.
  2. BAWASIRI YA NDANI
    Ni kuota kwa kinyama sehemu ya ndani ya haja kubwa. Mara nyingi huambatana na maumivu makali na damu, na kinyama hutoka wakati wa kujisaidia haja kubwa.
Bawasiri ya ndani ina hatua NNE ambazo ni:
  1. HATUA YA KWANZA
    Katika hatua hii mtu hujihisi maumivu makali, miwasho pamoja na kutokwa damu wakati wa kujisaidia, na kinyama hakionekani wakati wa kujisaidia.
  2. HATUA YA PILI
    Hii hutokea wakati wa haja kubwa na kurudi yenyewe punde baada ya kujisaidia.
  3. HATUA YA TATU
    Hii hutokea wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kurudisha ndani yeye mwenyewe ama inaweza kurudi yenyewe baada ya muda.
  4. HATUA YA NNE
    Hii ni bawasiri inayotoka na huwa ngumu kurudi baada ya kujisaidia.
VISABABISHI/MAMBO YANAYOWEZA KUSABABISHA MTU KUPATA BAWASIRI
  1. Uzito kupita kiasi (Overweight)
  2. Ujauzito
  3. Unywaji pombe
  4. Kukaa sana sehemu ngumu
  5. Kuingiliwa sehemu ya haja kubwa
  6. Kujisaidia choo kigumu. Sababu za kujisaidia choo kigumu ni:
  • Vidonda vya tumbo
  • Ngiri/Hernia
  • Ulaji duni
  • Kuwa na acid nyingi tumboni
  1. Kula sana nyama nyekundu
  2. Presha ya kupanda
  3. Kula sana pilipili
  4. Kula udongo (wajawazito na watoto wadogo)
  5. Kujisaidia kwenye vyoo vya kukaa
  6. Kuharisha kupita kiasi
  7. Kufanya kazi ngumu au kunyanyua vitu vizito
MADHARA/ATHARI ZA BAWASIRI
  1. Upungufu wa damu mwilini
  2. Kutokwa na kinyesi bila kujitambua
  3. Kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa
  4. Kupungukiwa nguvu za kiume
  5. Kupungukiwa uwezo wa kufanya kazi kutokana na maumivu
  6. Kupata tatizo la kisaikolojia
  7. Kutopata ujauzito
  8. Mimba kuharibika
  9. Kupata kansa ya utumbo (Colorectal Cancer)
  10. Mwili kudhoofika
NJIA ZA KUJIKINGA DHIDI YA BAWASIRI
  1. Kula mboga za majani na nafaka zisizokobolewa kwa wingi
  2. Kunywa maji mengi lita 2.5 hadi 3 kwa siku
  3. Acha kufanya mapenzi kwa kutumia tundu la haja kubwa
  4. Punguza kukaa chooni kwa muda mrefu kwani kunaweza kuongeza shinikizo katika njia ya haja kubwa
  5. Acha kunywa pombe
  6. Punguza kula nyama nyekundu
  7. Punguza matumizi ya pilipili
  8. Jitibie vidonda vya tumbo
  9. Jitibie ngiri
  10. Dhibiti uzito wako
  11. Jiepushe au punguza kunyanyua vitu vizito mara kwa mara
MATIBABU YA UGONJWA WA BAWASIRI
Kuna matibabu ya aina mbili katika kutibu ugonjwa wa bawasiri:
  1. MATIBABU YA KISASA
    -Matibabu ya kisasa yanahusisha matibabu ya hospitali ambapo tiba kubwa ya bawasiri ni kufanyiwa upasuaji mdogo (minor surgery) kwa ajili ya kuondoa kinyama. Changamoto kubwa ya matibabu haya ni kwamba asilimia kubwa ya wagonjwa wanaofanya upasuaji tatizo hujirudia kwa sababu upasuaji huondoa athari ya tatizo na si mzizi wa tatizo. Yaani ni sawa na kukata mti kisha ukaacha mizizi; bila shaka mti huo utachipua na kumea tena. Lakini pia upasuaji wa bawasiri huwa na maumivu makali sana na uponaji wa kidonda hufika mpaka miezi miwili. Hali hii ya kukaa na kidonda kwa muda mrefu inaweza kupelekea kupata kansa ya utumbo (Colorectal Cancer).
  2. MATIBABU KWA NJIA ASILI
    -Matibabu haya yanahusisha matumizi ya dawa zinazotokana na mimea dawa. Dawa hizi hutibu bawasiri bila kufanya upasuaji na huweza kuleta matokeo ya haraka kwa mgonjwa endapo atatumia dawa huku akijitahidi kujiepusha na visababishi vyote vinavyopelekea mtu kupata bawasiri. Zipo dawa asili nyingi na nzuri sana katika kutibu bawasiri, mfano wa dawa hizo ni Bawasiri Fluid na Bawasiri Powder. Dawa hizi zina ufanisi mkubwa katika kutibu bawasiri endapo mgonjwa atazingatia maelekezo.
ZIJUE SABABU ZINAZOWAFANYA WAGONJWA WENGI WA BAWASIRI KUTUMIA DAWA NYINGI BILA MAFANIKIO
Kwanza mgonjwa wa bawasiri anatakiwa kufahamu kwamba matibabu si dawa pekee. Watu wengi huamini kuwa matibabu ni dawa pekee, na jambo hili limepelekea wengi kuteseka na matatizo kwa muda mrefu bila mafanikio na kupelekea kukata tamaa ya kutafuta tiba, badala yake humuona kila mtoa huduma ni tapeli.

Zifuatazo ni sababu zinazowafanya wagonjwa wengi kuteseka na bawasiri kwa muda mrefu licha ya kutumia dawa mbalimbali:
  1. Kutopata dawa sahihi
    -Si kila dawa inayotangazwa kutibu bawasiri inaweza kutibu bawasiri, bali dawa yenye ufanisi ndio inaweza kutibu bawasiri.
  2. Kutofuata ushauri wa daktari
    -Usipofuata yale ambayo daktari anakuelekeza ili kupata suluhisho la tatizo lako, ni ngumu kupona.
  3. Kutoziacha sababu zilizopelekea upate bawasiri
    Katika hili wengi wamefeli kwani haiwezekani ukapona bawasiri ikiwa sababu zilizopelekea upate bawasiri hutaki kuziacha, mfano:
  • Pombe
    • Uzito mkubwa
    • Ulaji mbovu
    • Kuingiliwa kinyume
    • Kula sana pilipili
    • Kukaa sana sehemu ngumu
    • Kunyanyua vitu vizito
    • Kutotibu magonjwa kama ngiri na vidonda vya tumbo
    • Kutokula vyakula vya kulainisha choo kama mboga za majani na matunda
    • Kula udongo (wajawazito)
    • Kujisaidia kwenye vyoo vya kukaa
    • Kuharisha mara kwa mara
    • Kujisaidia choo kigumu
Hata utumie dawa zaidi ya 100, usipoziacha utaona watu ni matapeli kumbe sababu ni wewe mwenyewe kutofuata miongozo, maelekezo na ushauri kutoka kwa daktari.

Ukizingatia hayo utapona bawasiri kwa muda mfupi sana (wiki 1 mpaka 3) Biidhnillaah, japo wapo wanaopona kwa siku 5 licha ya kukaa na bawasiri kwa miaka kadhaa.
 
Back
Top Bottom