DaudiAiko
JF-Expert Member
- Dec 2, 2012
- 372
- 310
Wanabodi,
Utandawazi Kwa kiasi kikubwa umebadilisha maisha ya watanzania na jinsi ambavyo wanapata taarifa kuhusu mambo tofauti tofauti. Lakini je taarifa hizi zinazopatikana kwenye mitandao ni sahihi wakati wote?. Jibu la hili swali ni hapana. Katika harakati zako za kupata taarifa kwenye mtandao wa intaneti, ni muhimu kuchuja taarifa hizi na kuzingatia vyanzo vya taarifa unazopata ili kuelimika zaidi.
Vyombo vya habari pia ni njia inayotumiwa na watanzania wengi kupata taarifa mbalimbali na hapa ndipo nataka kujadili kitu kinachoitwa propaganda. Propaganda ni mbinu ambazo hutumiwa na serikali ku-push agenda yoyote Ile kwa wananchi. Propaganda ikifanywa vizuri huweza kuteka akili za wengi na kuwafanya kufikiria katika mienendo ambayo serikali inataka ufikirie.
Kwa haraka haraka unaweza kufikiria kwamba propaganda ni kitu kibaya lakini ukweli wa mambo ni kwamba propaganda inaweza kutumika kuhimiza kitu cha muhimu kwenye jamii hatakama katika kipindi kingine hutumika kuwafumba wananchi macho kuhusu kitu fulani. Mfano wa proganda ni, “Mvua za Kwanza ni za kulima”. Huu ni msemo maarufu sana katika enzi za Mwalimu Nyerere ambao ulitumika kuchochea kilimo. Propaganda inaweza kuwa kitu chochote na sio lazima kitoke kwenye vyombo vya habari. Inaweza ikawa nyimbo, muvi au hata picha.
Kuna maovu yanayoweza kufanywa kwa kutumia propaganda lakini unaweza kujilinda usipate maradhi ya propaganda. Njia kuu ni kuwa na uelewa mpana wa masuala mengi. Hii itakuwezesha kuchuja kila unacho sikia au kuona kwa umakini zaidi bila kuegemea upande wowote bila kuwa na uelewa wa kutosha
Akili ya kuambiwa, changanya na
ya kwako
View: https://youtu.be/yONuS8TB13M?si=ygwx-qZ19q8B6ZNO