Ifahamu propaganda

Ifahamu propaganda

DaudiAiko

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2012
Posts
372
Reaction score
310
Wanabodi,

Utandawazi Kwa kiasi kikubwa umebadilisha maisha ya watanzania na jinsi ambavyo wanapata taarifa kuhusu mambo tofauti tofauti. Lakini je taarifa hizi zinazopatikana kwenye mitandao ni sahihi wakati wote?. Jibu la hili swali ni hapana. Katika harakati zako za kupata taarifa kwenye mtandao wa intaneti, ni muhimu kuchuja taarifa hizi na kuzingatia vyanzo vya taarifa unazopata ili kuelimika zaidi.

Vyombo vya habari pia ni njia inayotumiwa na watanzania wengi kupata taarifa mbalimbali na hapa ndipo nataka kujadili kitu kinachoitwa propaganda. Propaganda ni mbinu ambazo hutumiwa na serikali ku-push agenda yoyote Ile kwa wananchi. Propaganda ikifanywa vizuri huweza kuteka akili za wengi na kuwafanya kufikiria katika mienendo ambayo serikali inataka ufikirie.

Kwa haraka haraka unaweza kufikiria kwamba propaganda ni kitu kibaya lakini ukweli wa mambo ni kwamba propaganda inaweza kutumika kuhimiza kitu cha muhimu kwenye jamii hatakama katika kipindi kingine hutumika kuwafumba wananchi macho kuhusu kitu fulani. Mfano wa proganda ni, “Mvua za Kwanza ni za kulima”. Huu ni msemo maarufu sana katika enzi za Mwalimu Nyerere ambao ulitumika kuchochea kilimo. Propaganda inaweza kuwa kitu chochote na sio lazima kitoke kwenye vyombo vya habari. Inaweza ikawa nyimbo, muvi au hata picha.

Kuna maovu yanayoweza kufanywa kwa kutumia propaganda lakini unaweza kujilinda usipate maradhi ya propaganda. Njia kuu ni kuwa na uelewa mpana wa masuala mengi. Hii itakuwezesha kuchuja kila unacho sikia au kuona kwa umakini zaidi bila kuegemea upande wowote bila kuwa na uelewa wa kutosha

Akili ya kuambiwa, changanya na
ya kwako

View: https://youtu.be/yONuS8TB13M?si=ygwx-qZ19q8B6ZNO
 
Mfano kuaminishwa lissu ni mtu mbaya na hatari kumbe hapana anachukiwa na WALA keki ya nchi sasa wao wanaofaidi keki ya nchi wanataka nasisi tumchukie lissu while in real sense we have nothing to lose na wao wanacho cha kupoteza lissu akishika nchi.
 
Lissu ana record safi na inayojulikana na ambayo Iko well documented inavyoonyesha harakati zake za kiwatetea wanachi wanyonge kule migodini nyamongo Toka mwaka 1992 unlikely Hawa wanaojifanya leo ni wazalendo ambapo hatujui hata wametokea wapi mpaka leo ndio eti wazalendo dhidi ya lissu uongo mtupu.
 
Mfano wa proganda ni, “Mvua za Kwanza ni za kulima”
Binadamu wanaolima wanalijua hilo tokea Mwanadamu alipoanza kilimo takriban miaka 7000 iliyopita,ni sawasawa na kuwaambia "giza likiingia laleni" hii ni Propaganga kwa ajili ya watu wajinga.

Propaganda nyingi za Nchi za Kikomunisti ni mbaya za kuwafanya wananchi wao wawe watumwa wa madikteta.
 
Lissu ana record safi na inayojulikana na ambayo Iko well documented inavyoonyesha harakati zake za kiwatetea wanachi wanyonge kule migodini nyamongo Toka mwaka 1992 unlikely Hawa wanaojifanya leo ni wazalendo ambapo hatujui hata wametokea wapi mpaka leo ndio eti wazalendo dhidi ya lissu uongo mtupu.
Kura ndio zinaamua nani awe Mwenyekiti, siyo sifa za mgombea. Wapiga kura kila mmoja ataamua apige kwa vigezo vyake, idadi itatuambia nani mshindi.
 
Binadamu wanaolima wanalijua hilo tokea Mwanadamu alipoanza kilimo takriban miaka 7000 iliyopita,ni sawasawa na kuwaambia "giza likiingia laleni" hii ni Propaganga kwa ajili ya watu wajinga.

Propaganda nyingi za Nchi za Kikomunisti ni mbaya za kuwafanya wananchi wao wawe watumwa wa madikteta.
Huko Zanzibar nasikia mwenye watumwa anarudi hivi karibuni kuangalia watumwa wamezaliana kiasi gani.

Na sijui ataamua nini kuwaachia wawe huru au atawarudisha aliko wanunua?

Eti wao wanamuita Sultan.
 
Huko Zanzibar nasikia mwenye watumwa anarudi hivi karibuni kuangalia watumwa wamezaliana kiasi gani. Na sijui ataamua nini kuwaachia wawe huru au atawarudisha aliko wanunua?
Eti wao wanamuita Sultan.
Badala ya kuwaalika hata ndugu zake na Hayati Jemadari Brother Ndugu Mhe. John Okello waje tuwafanyie Sherehe kubwa sana na kuwapa uraia wa Tanzania wa Heshima ndugu zetu huko visiwani watasema tunamkaribisha "Kafiri".

Ndio ujue Utumwa wa Mwarabu ule wa kutufunga minyororo umeisha uliobakia ni Utumwa wa fikra ambao inaonekana huenda tumeshindwa na Mwarabu.

Siku tukijikomboa na Utumwa wa kifikra tulioachiwa na Mwarabu huo ndio ukombozi wa kweli.
2683325.jpg

Hayati John Okello ajengewe sanamu kubwa Zanzibar na Dar ili kukumbuka rasmi mchango wake.
 
View attachment 3187695
Hayati John Okello ajengewe sanamu kubwa Zanzibar na Dar ili kukumbuka rasmi mchango wake.
Huyo hawamtaki wanamuona kama Jiwe, Wanasahau huyo ndiye aliyewasaidia kukata minyororo ya utumwa, labda mpaka leo wangekuwa bado wansafirishwa na mashua kupelekwa Oman, na sehemu zingine huko uarabuni kuosha vyombo, kuwapikia, kuwafulia, kuwasafishia na kuwafanyia kazi zingine.

Wako uhuru halafu hawataki kumshukuru aliye waokoa wakawa huru.

Wanashangili Sultan kurudi, shauri yao anaweza kufika akawasafirisha wote kuwarudisha shinyanga , na tabora, alafu kisiwani akafuga ng'ombe na Mbuzi.
 
Back
Top Bottom