Ifahamu Sekta ya Mafuta na Gesi Tanzania- Sehemu ya Kwanza (Utangulizi)

Ifahamu Sekta ya Mafuta na Gesi Tanzania- Sehemu ya Kwanza (Utangulizi)

Huyu countywide cjui nani,htak uzi utembee anaona wivu kuwa mwenzak ana elimu na ana share yy anayo kanyamaza hajui kuwasilisha mada, Chige kanyaga twende, hata hvyo umempa sana Airtime.
 
Hujaisoma Sera, Sheria, MPSA wala Kanuni halafu bila aibu unajigamba kujua mengi!!

Unayajuaje hayo mengi ikiwa hata sheria tu huzijui?!

VIROJA HIVI...

Unajua vitu vingi kwa kusikia mitani!
Ninafikiri kwa busara na utaalam zaidi, ungepandisha bandiko lililokamilika, kwa maana lenye kuzungumzia suala hili kama ulivoligawa katika utangulizi wako, vinginevyo hakuna cha maana cha kujadili mpaka hatua hii
Hapo kwenye Model Production Sharing Agreement ndo hasa patakapotoa au kuua maslahi yetu. Kwa sasa, MPSA iliyopo ni ya 2013 ambayo kuna taarifa zinadai kwamba Wawekezaji HAWAITAKI!
Umekimbilia kutoa hitimisho kabla hata ya kuzungumzia kuhusu hizo sheria, sera na kanuni na muhim zaidi bila hata kugusia "assumptions and basis" zilizotumika mpaka kufikita katika hiyo model ili kutoa nafasi na uwanja mpana wa majadiliano.

Nikupongeze tu kwa kuweka "data/statistics" kwa kila hoja uliyozungumzia kwa kadiri ulivoweza.
 
Ili niweze kugusia kila eneo, basi makala hii itakuwa na sehemu angalau tatu ambazo ni Utangulizi, Sera, Sheria na Kanuni zinazoongoza sekta hii, na sehemu ya mwisho fursa zilizopo.

Kwa kuanza, naweza kuiweka Gesi ya Tanzania kwenye makundi makuu mawili. Kundi la kwanza ni ile ambayo ugunduzi wake ulitokea wakati wa Awamu ya Kwanza, na kundi la pili ni ile ambayo ilianza kugundulika kwa wingi kuanzia Mwaka 2010.

Gesi ya Kundi la Kwanza inajumuisha gesi Gesi ya Songosongo kutoka mkoani Lindi, na ya Msimbati, mkoani Mtwara.

Hii Gesi ya Msimbati ndo ile ambayo ilizua kizaa zaa wakati wa JK..

Jumla ya gesi YOTE, yaani iliyogundulika Awamu ya Mwalimu na ile iliyogundulika awamu ya JK ni zaidi ya Futi za Ujazo TRILIONI 57; yaani 57 Trillion Cubic Feet (TCF).

Kati ya hizo, 7.5 Trillion Cubic Feet ziligunduliwa wakati wa Mwalimu na takribani 50 Trillion Cubic Feet ziligunduliwa wakati wa JK.

Aidha, ifahamike kwamba, kati ya zaidi ya 57.5 TCF ya gesi iliyogundulika, hadi sasa iliyoanza kuchimbwa ni ile TU ambayo Iligundulika wakati wa Mwalimu. Kwa maana nyingine, gesi ambayo ipo kwenye mzunguko wa kuzalisha umeme hivi sasa inatokana na zile 7.5 TCF, na zaidi ya 50TCF zilizogundulika wakati wa JK bado HAIJAANZA KUCHIMBWA!

Pia ifahamike kwamba, kiwango kikubwa cha gesi hii imegundulika kwenye Kina Kirefu cha Bahari. Na nikisema kina kirefu, ni kirefu hasa. Kwa ujumla, kati ya 57.5TCF ya gesi iliyogundulika, takribani 47 TCF inapatikana kwenye kina kirefu cha bahari ya Pwani ya Lindi na Mtwara.

Kwa mfano, ripoti zinaonesha kwamba Kitalu No. 1 kipo zaidi ya 100Km kutoka ufukweni na Kitalu No. 4 kipo takribani 200Km kutoka ufukweni.

Aidha, gesi yenyewe ipo takribani 1Km chini ya uso wa bahari (yaani, below water surface).

Pengine, hiyo ndio sababu hata gharama za ujenzi wa Kiwanda cha Kuchakata Gesi Asilia (LNG) pale Lindi ni KUBWA MNO kwa sababu, gesi inatarajiwa kuchimbwa angalau 1 Km chini ya uso wa bahari kisha kusafirishwa kwa mabomba kwa zaidi ya 100km hadi nchi kavu kitakapojengwa kiwanda cha uchakataji.

Pia, si mbaya tukifahamu vitalu vyetu vipo chini ya akina nani.

Kitalu No. 1 na No. 4 vipo chini ya Shell (exploration concession 60%), Kampuni ya Pavilion Energy (20%), na PT Medco Daya Abadi Lestari (20%).

Shell Tanzania ndie Operator wa Kitalu husika.

Ifahamike kwamba, Shell Tanzania ni Kampuni ya Kidachi, Pavilioni Energy ni kampuni tanzu ya Temasek Holdings Limited, na Temasek Holdings Limited ni kampuni ya Serikali ya Singapore!

Aidha, PT Medco Daya Abadi Lestari ni kampuni ya Kiindonesia inayomilikiwa na Familia ya The Panigoro, na mwanzilishi wa kampuni hiyo ni Arifin Panigoro ambae amefariki February 2022.

Kwa ujumla, Kitalu No.1 na Kitalu No. 4 vina takaribani 17 TCF of natural gas reserve.

Kwa upande mwingine, Kitalu No. 2 kinaendeshwa na kampuni ya Equinor na ExxonMobil.

Equinor, ambayo zamani ilikuwa inafahamika kama Statoil ni kampuni kutoka Norway huku shareholder mkubwa akiwa Serikali ya Norway yenye hisa 67%, huku ExxonMobil ikiwa ni kampuni kutoka Texas, Marekani.

Kitalu hiki No. 2 kinakadiriwa kuna na zaidi ya 20 TCF. Na kama ilivyo kwa vitalu vingine, Kitalu No. 2 kipo umbali wa takribani 100Km kutoka Pwani ya Lindi, na gesi inapatikana takribani 2Km kutoka uso wa bahari (2km below water surface)

REMEMBER: Umiliki huo hapo ni Umiliki uliotokana na leseni ya Utafutaji wa Gesi lakini kwa Mujibu wa Sheria ya Mafuta na Gesi ya Mwaka 2015, Mmiliki HALISI wa Vitalu husika ni National Oil Company (For now, TPDC).

Jambo lingine ambalo watu wanatakiwa kulifahamu ni kwamba, hadi kufikia sasa, kiwango kikubwa cha gesi kimegundulika Mkoani Lindi na sio Mtwara kama ambavyo wengi wanadhani.

Aidha, tumepata kusikia hapa na pale kwamba Gesi YOTE ameuziwa Mchina! Na kama nilivyosema hapo juu, hizo kampuni za kigeni zilipewa leseni ya Utafutaji na sio UCHIMBAJI.

Hadi hivi sasa, HAKUNA kitalu chochote KILICHOUZWA kwa ajili ya uchimbaji. Endapo utaratibu utafuatwa, Vitalu husika vitapaswa kupigwa mnada na wale watakaoshinda ndio watapewa leseni za UCHIMBAJI.

Kuhusu nani atapata nini kati ya Serikali na Mwekezaji, hilo tutajadili kwenye Sehemu ya Pili ya mada hii ambapo tutaangazia Sera, Sheria, Kanuni na Model Production Sharing Agreement.

Hapo kwenye Model Production Sharing Agreement ndo hasa patakapotoa au kuua maslahi yetu. Kwa sasa, MPSA iliyopo ni ya 2013 ambayo kuna taarifa zinadai kwamba Wawekezaji HAWAITAKI!
Bora nimepita hapa nijue mambo ya msingi kuliko hbr za kina simalenga dimela kumnaza mwanafunzi malay makofi

Njoo wew kijana UMUGHAKA ufahamu vitu hv
 
Countrywide kuwa na ADABU xcxxx wewe,mtu anakuja kwa nia njema ya kutujuza wewe unaleta ujuaji tena wakishamba.Mwache atoe yake kisha kama waona kakosea na wewe uje kwa muda wako kwa thread yako kivyako otoe yaliyo ya kweli tofauti na haya.Unaonekana unachuki binafsi na mtoa mada.Unataka uonekane mjanja na mjuaji lakini waerevu wanakuona mshamba tu na unapoteza muda katika mambo ya msingi.
 
Wew chige endeleaa na model of prodaction sharing agreememt

Ukianza kuleta uzi plz nitag mapema nifikee nisome nipata kitu kipya ambacho hapo kabla nilikuwa mweupe sijui lolote naaaam niko na wew had mwisho wa uzi
 
Umekimbilia kutoa hitimisho kabla hata ya kuzungumzia kuhusu hizo sheria, sera na kanuni na muhim zaidi bila hata kugusia "assumptions and basis" zilizotumika mpaka kufikita katika hiyo model ili kutoa nafasi na uwanja mpana wa majadiliano.
Mambo yote ningeweka pamoja thread ingekuwa ndefu sana kwa sababu kuna mengi ya kujadili. Hii sekta ina SHERIA 3 ambazo ni:-

1. Sheria ya Mafuta na Gesi ya 2015
2. Sheria ya Usimamizi wa Mapato ya Mafuta na Gesi ya 2015, na
3. Sheria ya Uwazi na Uwajibikaji ya 2015.

Pamoja na hizo sheria pina kuna MPSA na kanuni kibao.

Huwezi kuweka yote hayo kwenye thread moja kama lengo lako ni kutoa mwanga kwa kwa watu wengi, kwa sababu ukifanya hivyo, ni wachache sana watakaoweza kusoma kutokana na ukweli kwamba thread itakuwa ndefu kupita kiasi.

Ukisema ujadili japo kipengele kimoja tu cha Local Content lakini ujadili kwa undani, peke yake inaweza kuzaa thread mzima bila kugusa vitu vingine.
 
Wew chige endeleaa na model of prodaction sharing agreememt

Ukianza kuleta uzi plz nitag mapema nifikee nisome nipata kitu kipya ambacho hapo kabla nilikuwa mweupe sijui lolote naaaam niko na wew had mwisho wa uzi
NOTED!
 
Na kinachonichanganya uchumi wa gesi amshaamsha ziko mtwara kuliko lindi wenye gesi yenyewe yaani sasa na madini kwa mfano yawe congo halafu ijengeke Rwanda na sio congo
 
Una lengo zuri na jema sana na inaelekea una maarifa mengi juu ya sekta hii, hongera.

Hapo kwenye Model Production Sharing Agreement ndo hasa patakapotoa au kuua maslahi yetu. Kwa sasa, MPSA iliyopo ni ya 2013 ambayo kuna taarifa
Hiyo aya kama mleta hoja hapa imeshindwa kabisa kuweka mizani, na zaidi, haikupaswa kuwepo hapo.
 
Na kinachonichanganya uchumi wa gesi amshaamsha ziko mtwara kuliko lindi wenye gesi yenyewe yaani sasa na madini kwa mfano yawe congo halafu ijengeke Rwanda na sio congo
Sababu kubwa ni tatu...

1. Majority wakisikia Kusini moja kwa moja akili yao wanaipeleka Mtwara,

2. Sakata la "Gesi Itatoka au Haitoki" lilitokea Mtwara kwavile gesi husika ni ya huko. Kutokana na hilo, watu wakaanza kuhusisha suala zima la gesi na Mtwara!

3. Wakati issues za gas zimepamba moto (wakati wa JK), ikabidi zianze jitihada za kuboresha Bandari ya Mtwara kwa sababu sio tu ndio bandari inayotegemewa kutumika for export lakini pia ndio ilitarajiwa ingetumika kuingiza vifaa vya ujenzi wa LNG Plant, na uchimbaji.

Sasa shughuli za uboreshaji wa bandari ndo zikaichangamsha zaidi Mtwara.

NOTE: Pamoja na Lindi na Mtwara, pia kuna zaidi ya 2.3 Trillion Cubic Feet of gas iliyogundulika Mkuranga na Mambakofi (kwenye Bonde la Mto Ruvu) lakini wengi wanafahamu kuhusu Kusini peke yake.

Na kuna uwezekano wa kuwepo gesi Ziwa Tanganyika.
 
Huyu chige ni mtu wa ajabu. Ananikazania nikasome kanuni, ikiwa nazijua zote. Yeye anahisi hizo kanuni na sheria zitainufaisha Tanzania.

Nimekueleza vizuri tu kuwa hata Magufuli alikuwa anapoteza muda na yale mapambano yake kwenye madini.

Same na kwenye gesi, huwezi kufanya majadiliano ya faida kwa taifa na watu ambao wanakuamria hata kuishi tu uishi vipi.

Watu wamekuja kuwekeza trillion 90 kwenye gesi, unafikiri watakuambia watachukua miaka mingapi kurudisha pesa yao?

Kwenye madini hakukua na uwekezaji mkubwa Kama huu wa gesi, Ila bado hatukupata chochote mwaka wa 60 huu
Wee jamaa ni mshamba alafu mjingaa sana ingekuwa busara na wewe ungatoa mada yako ya malezi ya watoto au jinsi ya kumfikisha mkeo siyo kumkosoa MTU ili umtoe kwenye lengo lake
 
Yeye ameanzisha uzi ili sisi wengine tuelimike, sasa kama wewe kuna unachojua huwezi kuchangia bila kupiga vijembe?
Hii ID lengo la kuifunguaa unaijua, hakuna jina lingine zaid ya wewe ni mjinga
 
Wee jamaa ni mshamba alafu mjingaa sana ingekuwa busara na wewe ungatoa mada yako ya malezi ya watoto au jinsi ya kumfikisha mkeo siyo kumkosoa MTU ili umtoe kwenye lengo lake
Humu wajinga mpo wengi sana na kwa bahati mbaya hamjifichi
 
Una lengo zuri na jema sana na inaelekea una maarifa mengi juu ya sekta hii, hongera.

Hiyo aya kama mleta hoja hapa imeshindwa kabisa kuweka mizani, na zaidi, haikupaswa kuwepo hapo.
Sijui kuna uhusiano gani Kati ya ID mpya na ujinga
 
Wew chige endeleaa na model of prodaction sharing agreememt

Ukianza kuleta uzi plz nitag mapema nifikee nisome nipata kitu kipya ambacho hapo kabla nilikuwa mweupe sijui lolote naaaam niko na wew had mwisho wa uzi
Wajinga ni wengi sana, alafu kwa nn wajinga wengi mmejiunga jf 2022??
 
Huyu countywide cjui nani,htak uzi utembee anaona wivu kuwa mwenzak ana elimu na ana share yy anayo kanyamaza hajui kuwasilisha mada, Chige kanyaga twende, hata hvyo umempa sana Airtime.
Najua ni kazi sana kumtoa mtu ujinga alionao. Hata hivyo chige ameshafahamu tupo werevu wachache hivyo ataacha ujinga wake.
 
Back
Top Bottom