Jana usiku nilikua na drive nje ya mji...nikaona dot 2 zinawaka kwa mbele, hatimaye nikagundua ni fisi amechill pembeni ya barabara... TAPETUM LUCIDUM ni layer yenye asili ya mng'ao iliyopo nyuma ya retina katika jicho la kiumbe hai. Sio viumbe wote wanayo, hii wamepewa viumbe baadhi ambao wapo active at night kama,fisi,simba,chui,bundi lakini binadamu hatujaumbwa na hii kitu. Layer hii inafanya kazi pale mwanga unapotua katika jicho, huakisiwa na kurudi ulipotoka hivyo kumsaidia kiumbe kuona vizuri katika mwanga hafifu..