Ifanye pesa isiwe ya msimu, buni vyanzo vingine vya mapato

Ifanye pesa isiwe ya msimu, buni vyanzo vingine vya mapato

Kilimo kina msimu, hilo tunalielewa, msimu wa masika, vuli, kipupwe na hata kiangazi. Pesa hazina msimu. Ukifanya kazi kwa bidii na ukizitafuta, mwaka mzima unaweza ukawa kwenye masika ya hela wakati wengine wakiugulia kwa kusema hali ngumu wewe utakuwa huelewi wanaongea kichina au kimakonde.

Huwezi kubadili majira ya mwaka kwenye kalenda, lakini unaweza kubadili majira ya pesa kwenye akaunti zako za benki.

Wengi tunaridhika na utajiri wa tarehe 30. Kila mtu anakuwa mbabe ikifika mwisho wa mwezi. Kila mtu anajiona milionea lakini zikifika tarehe kama hizi, tarehe 15-23 ya kila mwezi, yule milionea aliyekuwa ana mbwembwe sana wiki 2 tu zilizopita, hana kitu.

Na kila mwezi majira yake ni hayahaya, maji kupwa maji kujaa lakini hashtuki... Anaona ni sawa tu kuwa na hela tarehe 30 lakini apeche alolo wiki 2 baadae akihaha kukopa ili afike tarehe nyingine ya mshahara.

Je, wewe ni mmoja wao? Tajiri wa msimu ni wewe?

Tarehe 30 HR anakupa kiburi, wiki 2 baadaye unapaki gari haina wese unaanza kuomba lifti kwa co-workers wanaokaa karibu na wewe Kimara wakupitie. Je, ni wewe?

Tajiri wa mshahara, ukiona tangazo la punguzo la wafanyakazi unasikia nnya inagonga pichuchu, huna Plan B, na huna hata miaka 30 lakini akili yako imezeeka, unajiita bosslady kwa mshahara wa kila tarehe 30?

Babako aliishi kwa mshahara, akastaafu, na sasa anaishi kwa pensheni, hatumlaumu. Kipindi alichoishi hali haikuruhusu, eti na wewe, unataka uishi kama baba'ko, ili na wewe uje ustaafu uishi kwa pensheni?

Babako ameishi kwenye ujima, wewe una kila sababu ya kutoishi kama yeye kwa sababu una kila kitu ambacho yeye hakuwa nacho. The tools, the technology, the information, the education. Ukipata matokeo sawa na babako aliyeishi karne ya 20 umefeli.

Mshahara hautakupa utajiri, mshahara unapaswa ulipie luku. Bili za maji, housegirl, wese la gari na bata.

Maendeleo yako mengine yanahitaji other revenue streams ambazo huna na huonyeshi dalili za kuzitafuta. Utakufa maskini hakika au utaishi kwa pensheni ya 60,000 kwa mwezi kama mamako mstaafu wa jumuiya ya Afrika Mashariki.

Wake up now month end millionaire! You're alive so that u can challenge the status quo na sio kuishi-ishi tu kama bolizozo.

emoji23.png
emoji23.png
[emoji2

Mimi ni mdada mkuu [emoji23]
Nashukuru kwa kuliona hilo, tatizo sisi wamatumbi tunapenda kutafuniwa kila kitu.
Hapo alitaka nimtafutie na chanzo cha mapato nimkabidhi n still asingeridhika.
Ikiwezekana ajira ikupr mtaji.. Fanya kazi miaka 3 basi. Ukishazoea ajira huwezi ach..
 
umeongea vizuri lakini huu ni ushauri wa jumla sana ambao mtu yeyote anaweza kukupa, pia mtu yeyote anaweza kuelewa hili mda mfupi tu baada ya kuajiriwa...

ungetuambia kwa undani jinsi ya kuacha kutegemea mshahara au jinsi wewe umeweza kufanya hivyo ingependeza zaidi....
 
umeongea vizuri lakini huu ni ushauri wa jumla sana ambao mtu yeyote anaweza kukupa, pia mtu yeyote anaweza kuelewa hili mda mfupi tu baada ya kuajiriwa...

ungetuambia kwa undani jinsi ya kuacha kutegemea mshahara au jinsi wewe umeweza kufanya hivyo ingependeza zaidi....
Mmatumbi kwenye ubora wako 😂😂
 
Hivi we unanichukuliaje? [emoji23][emoji23]
Dada me ndo mwalimu wake.
Tuma kwanza, nitaelewa tu. Kuna utofauti nitaona, kama vya kuchemshwa ni vingi nitajua tu hapo ni wewe. Kama vipo rosted hapo nitajua ni dada[emoji23]
 
Back
Top Bottom