Ifanyike sensa, Wazanzibar wote wanaofanya kazi zisizo za muungano bara warudishwe kwao

Tulikofikia Wazanzibar wataanza kutuchukulia poa sana hasa hasa kipindi cha Rais wa kutoka kule

Kuna speech ya Nyerere inatembea sana mitandaoni yenye maudhui kwamba yeye (Nyerere) ndiye aliyekataa muungano wa serikali moja kwa kuhofia kuonekana anataka kuimeza (kuitawala) Zanzibr

Kwa jinsi tunavyoenda ipo siku wao Wazanzibar watatutawala sisi watu wa bara na huenda hizo siku zimeshakaribia sana

Ukichunguza kwa umakini ndani ya baraza la mawaziri, ndani ya wizara, idara mbalimbali za serikali, wakurugenzi wa halmashauri mbalimbali na makatibu tawala wa mikoa na wilaya kwasasa utakutana na Wazanzibar wengi sana.

Hapa simaanishi wale waliozaliwa na kukulia huku bara (wenye asili ya Zanzibar), namaanisha wale walioteuliwa au "kupewa" ajira moja kwa moja kutokea Zanzibar na kuja kwao ni kwasababu ya cheo au kazi

Kumbuka hawa wakishateuliwa wana ndugu zao, shangazi na mjombo, mamdogo na Bamkubwa huko.

Hii inamaana kwamba fursa ndogo ndogo zinazopita mikononi mwao lazima watawawaza hao ndugu zao kwanza kabla ya chochote

Kwa mfano; hivi karibuni katika zoezi la mitihani ya Taifa, kuna wale watumishi wa NECTA huwa wanatumwa sehemu mbalimbali kufuatilia zoezi zima la ufanyikaji wa mtihani, sura nyingi zilikuwa za kutoka Zanzibar

Hapa ni rahisi sana kujumlisha na kutoa na kupata jibu kwamba huenda imekuwa rahisi kwao kupata hizo fursa kwasababu mkurugenzi wa NECTA ni Mzanzibar na ukumbuke kuwa hizi fursa mwazo hazikuwahusu kwasababu pia hata mtaala tunatofautiana (sina hakika kama elimu ni swala la muungano)

Kwa sasa wanapewa upendeleo, wakishazoea wataona ni haki yao halafu shida itaanza pale atakapokuja mwingine asiwape huo upendeleo.

Kama kuna kosa kubwa Nyerere alifanya ni kuukataa ushauri wa Karume wa kuunda serikali moja na Zanzibar kubaki kama mkoa tu,

Hata kama aliogopa mbeleni wasijeanzisha vuguvugu la kudai nchi yao lakini wazo la Karume ndio lilikuwa wazo zuri zaidi. Ndio maana halisi ya kuungana. Kinachoungana kinakuwa kimoja sio kimoja na nusu

Tusisubiri makubwa yatupate, kwa vile wanaserikali yao na wanaipenda serikali yao basi warudi kwao wakaitumikie kwa amani watuachie ya kwetu huku

Wabaki wachache wale wanaohusika na maswala ya Muungano tu au la na wa huku bara pia wawe na fursa sawa za kuteuliwa Zanzibar kwa nafasi kama hizo hizo na malalamiko yasiwepo
nakubaliana nawe
 
7/7 ni ya moto kuliko moto wenyewe vijana wana hoja na wanazisimamia mimi ni Mtanganyika
 
Tulikofikia Wazanzibar wataanza kutuchukulia poa sana hasa hasa kipindi cha Rais wa kutoka kule

Kuna speech ya Nyerere inatembea sana mitandaoni yenye maudhui kwamba yeye (Nyerere) ndiye aliyekataa muungano wa serikali moja kwa kuhofia kuonekana anataka kuimeza (kuitawala) Zanzibr

Kwa jinsi tunavyoenda ipo siku wao Wazanzibar watatutawala sisi watu wa bara na huenda hizo siku zimeshakaribia sana

Ukichunguza kwa umakini ndani ya baraza la mawaziri, ndani ya wizara, idara mbalimbali za serikali, wakurugenzi wa halmashauri mbalimbali na makatibu tawala wa mikoa na wilaya kwasasa utakutana na Wazanzibar wengi sana.

Hapa simaanishi wale waliozaliwa na kukulia huku bara (wenye asili ya Zanzibar), namaanisha wale walioteuliwa au "kupewa" ajira moja kwa moja kutokea Zanzibar na kuja kwao ni kwasababu ya cheo au kazi

Kumbuka hawa wakishateuliwa wana ndugu zao, shangazi na mjombo, mamdogo na Bamkubwa huko.

Hii inamaana kwamba fursa ndogo ndogo zinazopita mikononi mwao lazima watawawaza hao ndugu zao kwanza kabla ya chochote

K

wa mfano; hivi karibuni katika zoezi la mitihani ya Taifa, kuna wale watumishi wa NECTA huwa wanatumwa sehemu mbalimbali kufuatilia zoezi zima la ufanyikaji wa mtihani, sura nyingi zilikuwa za kutoka Zanzibar

Hapa ni rahisi sana kujumlisha na kutoa na kupata jibu kwamba huenda imekuwa rahisi kwao kupata hizo fursa kwasababu mkurugenzi wa NECTA ni Mzanzibar na ukumbuke kuwa hizi fursa mwazo hazikuwahusu kwasababu pia hata mtaala tunatofautiana (sina hakika kama elimu ni swala la muungano)

Kwa sasa wanapewa upendeleo, wakishazoea wataona ni haki yao halafu shida itaanza pale atakapokuja mwingine asiwape huo upendeleo.

Kama kuna kosa kubwa Nyerere alifanya ni kuukataa ushauri wa Karume wa kuunda serikali moja na Zanzibar kubaki kama mkoa tu,

Hata kama aliogopa mbeleni wasijeanzisha vuguvugu la kudai nchi yao lakini wazo la Karume ndio lilikuwa wazo zuri zaidi. Ndio maana halisi ya kuungana. Kinachoungana kinakuwa kimoja sio kimoja na nusu

Tusisubiri makubwa yatupate, kwa vile wanaserikali yao na wanaipenda serikali yao basi warudi kwao wakaitumikie kwa amani watuachie ya kwetu huku

Wabaki wachache wale wanaohusika na maswala ya Muungano tu au la na wa huku bara pia wawe na fursa sawa za kuteuliwa Zanzibar kwa nafasi kama hizo hizo na malalamiko yasiwepo
Naanza na kichwa cha habari. Musijekunung'unika mbeleni. Juzi tu kuhusu mahotelini mulisems sana lkn awali mulikuwa munadai Wabara hawaajiriwi Zanzibar, kumbe ni uongo.
Ukichunguza kwa umakini ndani ya baraza la mawaziri, ndani ya wizara, idara mbalimbali za serikali, wakurugenzi wa halmashauri mbalimbali na makatibu tawala wa mikoa na wilaya kwasasa utakutana na Wazanzibar wengi sana.
Lete hizo takwimu, vinginevyo wewe ni mwongo.
Kwa mfano; hivi karibuni katika zoezi la mitihani ya Taifa, kuna wale watumishi wa NECTA huwa wanatumwa sehemu mbalimbali kufuatilia zoezi zima la ufanyikaji wa mtihani, sura nyingi zilikuwa za kutoka Zanzibar
Inaelekea hata taasisi za muungano huzijui. NECTA huzijui status yake, halafu unakurupuka!!
Kama kuna kosa kubwa Nyerere alifanya ni kuukataa ushauri wa Karume wa kuunda serikali moja na Zanzibar kubaki kama mkoa tu,
Unajidanganya. Unadhani hata ikiwa serikali moja, Zanzibar itakuwa mkoa? Nasikia mumesoma! Huku ndio kusoma?
Tusisubiri makubwa yatupate, kwa vile wanaserikali yao na wanaipenda serikali yao basi warudi kwao wakaitumikie kwa amani watuachie ya kwetu huku
Nakubaliana nawe. Hata wale wanaotoka kwenu warudi kwao waitumikie serikali yao. Kumbuka: ukimunyooshea mtu kidole kimoja, vitatu vinakurejea mwenyewe. Kuwa makini sana na maneno.
 
Hao ni watanzania! Lakini wewe sio mzanzibar! Zanzibar ya wazanzibar. Tanzania ni ya wazanzibar na watanganyika
Shirika sio la muungano.

Zanzibar nao wana shirika lao huko, linalofanya kazi sawa na la huku bara. Wao wameajiriwa la huku bara wakati nao kule kuna shirika lao.
 
Back
Top Bottom