Ifike hatua Waafrika tuache ujinga. Hivi Nigeria maandamano yao yanataka Serikali ifanye nini ili waache?

Ifike hatua Waafrika tuache ujinga. Hivi Nigeria maandamano yao yanataka Serikali ifanye nini ili waache?

mr gentleman

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2012
Posts
3,222
Reaction score
4,689
Chanzo cha maandamano nchini Nigeria ni kuisukuma serikali ifute kitengo cha usalama cha SARS.

Serikali ya Nigeria iliwasikiliza waandamanaji na ikatangaza kufuta hiyo agency.

Ila naona Wanaijeria bado wanaandamana wanafanya vurugu na jana jeshi limeingilia na kuua baadhi ya waandamanaji.

Swali langu au nisichoelewa kama waandamanaji walipewa walichotaka kwa nini maandamano yanaendelea wanachotaka ni nini?

Au ni ile laana yetu ya asili kwa ngozi nyeusi ndio inafanya kazi huko?
 
Chanzo cha maandamano nchini Nigeria ni kuisukuma serikali ifute kitengo cha usalama cha SARS.

Serikali ya Nigeria iliwasikiliza waandamanaji na ikatangaza kufuta hiyo agency....
Hicho kitengo cha SARS kimefutwa, halafu kimeundwa kipya kinaitwa SWAT halafu wameweka watu walewale waliokuwa kwenye kitengo cha SARS. Kwa hiyo raia wameona wanafanyiwa uhuni.
 
Hicho kitengo cha SARS kimefutwa, halafu kimeundwa kipya kinaitwa SWAT halafu wameweka watu walewale waliokuwa kwenye kitengo cha SARS. Kwa hiyo raia wameona wanafanyiwa uhuni.
Wao walitaka watu wa SWAT watoke wapi?

Yaani mfano leo ukiivunja FFU unaenda kuwapata wapi watu wa unit mpya ya kuzuia vurugu?
 
Serikali ilisema inaondoa SARS lakini badala yake wanaunda agency nyingine ambayo waliainisha majukumu yao na ni namna gani askari atakua eligible kua recruited kwenye hii agency mpya.

Pia wakasema askari yeyote aliyewahi kua member wa SARS hatokua eligible kua recruited kwenye hii agency mpya. Na wakaahidi itakua transparent kuliko hii SARS.

Nahisi wanaijeria wanaona wanachezewa change quorter. Wanaona yatakua ni ya kutoa shilingi mfuko wa kushoto na kuweka mfuko wa kulia.
 
Wao walitaka watu wa SWAT watoke wapi?

Yani mfano leo ukiivunja FFU unaenda kuwapata wapi watu wa unit mpya ya kuzuia vurugu?
Ukumbuke hao SARS sio police force yote, wanaweza kuchukua askari wa kawaida na kuwapa mafunzo maalum, na serikali ndio iliahidi hivyo na kusisitiza kuwa hakuna askari wowote aliyekuwa SARS atakubaliwa kujiunga kwa ajili ya mafunzo ya kikosi kipya. Kilichofanywa ni kama kumpaka punda rangi ili ageuke kuwa pundamilia .

Establishment, Composition and Training of Nigeria Police SWAT to Replace the Disbanded SARS
 
Dina maandamano yasiokuwa na kikomo ni mapinduzi. Jeshi kazi yake ni kuzuia viashiria vyovyote vya kuipindua serikali.
Mambo haya ya kikatili tunayoendekeza ndiyo yanazidisha laana kwa waafrika. Belarus wana kama mwezi wanaandamana kila siku lakini hakuna mauaji ya binadamu.

Kwanini nyie waafrika mnaona solution ni kumwaga dam tu?
 
Back
Top Bottom